Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbuka huyo anayelipwa 800k kila mwezi ni profit guaranteed, hata itokee nini kisheria lazima laki 8 yake ilipwe mpaka mkataba utakapoisha na millioni 100 zake atarudhishiwaHaya mawazo ya mzee ambaye hana nguvu za kufikiri wala kufanya kazi. Achana na millioni 100 kutengeneza 800k.
Kwa kijana mwenye nguvu za mwili na uwezo wa kufikiri vzri ukiwa na tsh mill 10 unaweza kutengeneza 1M net profit!
Very true bora awe ananunua hata Viwanja kuliko kuweka hela tuuSavers are losers
1. Sasa hivi Vitu vimepanda Bei mara 100% toka uzi wako Uweke
2. Hela ulizotunza Zishashuka Thamani yake
3. Bati Na Cement vimepanda Bei
4. Mafuta Yamepanda Bei
Mil 20 ya Kipindi unaweka uzi ni mil 17-18 sasa hivi
iCOBS Ni sehemu Tulivu ya kutunza pesa zako na kufanya maendeleoSalaam sana wakuu,
Tunamshukuru Muumba wa mbingu na nchi kwa kutufikisha disemba hii 2021 ambapo tunapata nafasi mtawalia ya kutafakari kwa kina malengo tuliyojiwekea kwa mwaka 2021 huku tukijipanga kwa ajili ya mwaka mpya 2022. Binafsi nina lengo la kufanya savings ifike milioni 20 ifikapo mwaka 2022 mwezi Oktoba. Maandalizi kwa ajili ya kufanikisha lengo langu hilo nimeshayaanza kwani mpaka sasa nimeshafungua akaunti ya kufanya savings hiyo. Vile vile kuna kijikazi nakifanya (tofauti na kazi yangu rasmi ya mshahara) kwa hiyo nitakuwa na inflow fulani hivi ambayo kwa miezi tarajiwa mpaka Oktoba 2022 ninaweza kufikia kiwango hicho cha milioni 20.
Lengo kuu la savings hiyo ni kuwezesha ujenzi wa banda langu la kujifichia hapa jijini Dar es Salaam kwani maisha ya upangaji ni magumu na kwa vijana wengi tunajua kuwa wakati wa kutafuta nyumba zetu ni sasa ili kupunguza mzigo wa kodi ya nyumba pale utakapokuwa na familia maana sisi hatuna utegemezi wa kurithi mali za wazazi wetu.
Niko hapa mbele yenu ili nipate uzoefu kwa wale waliowahi kujiwekea malengo ya kufanya savings kwa kipindi fulani cha miezi na hata miaka wanipe uzoefu ni kwa namna gani walifanikiwa kufikia malengo yao sambamba na changamoto walizokutana nazo jambo linaloweza kuwa chachu ya mafanikio sio kwangu tu bali hata kwa wenzangu waliopo katika jukwaa hili kwani changamoto za savings hakuna asiyezijua na isitoshe hakuna mtu asiye na matumizi ya pesa ikiwepo kuruka mitego kadhaa ya maombi ya ndugu, jamaa, marafiki pamoja na watoto wa mjini (hasa wa kike) si mnajua wanavyovutia wakuu ";;;;;;. . . .
Naomba kuwasilisha wakuu . . .
Naomba maelezo zaidi bossV
iCOBS Ni sehemu Tulivu ya kutunza pesa zako na kufanya maendeleo
Una mawazo ya kimasikini sanaKumbuka huyo anayelipwa 800k kila mwezi ni profit guaranteed, hata itokee nini kisheria lazima laki 8 yake ilipwe mpaka mkataba utakapoisha na millioni 100 zake atarudhishiwa
Wewe na millioni 10 yako ukianzisha biashara itahitaji usimamizi wako 100% ndo upate profit 1M (japo sijui umezungumzja biashara gani). Ukiumwa, ukisafiri au kwa namna yoyote ile biashara ikakosa usimamizi mzuri basi huwezi fikisha lengo lako
Ukifanya biashara mwenyewe kuna 50/50 upate faida au hasara. Bond haina hasara ni 100% profit(japo faida yaweza kuwa kubwa au ndogo inategemea na kiasi ulichoweka)
Pia, kama umemuelewa vizuri mchangiaji hapo juu ametoa mfano mzuri kabisa wa mzee aliyestaafu. Alimaanisha basi kusema hivyo:-
1. Wazee hawana nguvu za kusimamia biashara kama walivyo vijana, hivyo basi itakosa usimamiz mzudi UNLESS hiyo biashara alianzisha tangu zamani (akiwa mdogo au kijana) hivyo biashara yake inaweza kujisimamia
2. Wazee hawataki purukushani nyingi
NOTE :
Uliyoyasema ni sahihi na sijakupinga nimejaribu tu kufanya comparison kati ya kijana atakayeanzisha business yake kwa 10M na mzee atakayenunua Bonds kwa 100M
Uwe na jioni njema
Nawasilisha,
Hesabu zako ziko sawa kweli?Weka standing order kukata milioni 1 kila mwezi kwenye mshahara
Na hio side business kila mwezi chukua 1m peleka benki
Kwa mwaka 24M hiooo
Acha ama punguza anasa
Inawezekana
Milion 2 kwa mwezi *12 inaleta ngapi huko?