Lengo la kuwa na saving ya milioni 20 ifikapo mwaka 2022 mwezi Oktoba

Huu ushauri ni mzuri na salama kuliko kuweka pesa kama pesa
 
Unauzungumziaje mfuko wa BOND fund
 
Usi-save. Mwisho mwa 2022 hio 22 million inaweza ikawa haina thamani. Vifaa vya ujenzi vinapanda bei mara mbili mfano mwanzoni mwa 2021, nondo ya 10mm ilikuwa tshs 15,000. December 2021 ikawa tshs 22,000. Sasa hapo uki-save na hii inflation utaumia. Kila ukipata hela iweke kwa ujenzi.. usisubiri uwe na hela nyingi.
 
Unauzungumziaje mfuko wa BOND fund
Bond fund iko structured kumfaa zaidi mtu aliye na kiasi fulani kikubwa, anaweka kwenye mfuko huo - halafu sehemu ya faida inatumika kumlipa kila mwezi au kila kipindi fulani anachochagua. Mfano anayestaafu aweza kuweka milioni 100 halafu akawa na income ya around 800,000 kila mwezi.
 
Ni kweli kabisa,lkn maneno ya huyo jamaa sio dogma.
 
Elimu ya uwekezaji inahitajika sana. Wengi wetu hatuelewi kabisa mambo ya hisa, hati fungati, mambo ya UTT ndio kabisaaaa.

Natamani mitaala ingeboreshwa haya mambo na ujasiriamali (ijikite kwenye finance) yakapigwa hata kwa utangulizi tu.
Ni sahihi kabisa Mkuu,hiyo Elimu murua kabisa wengi hatuna.
 
Haya mawazo ya mzee ambaye hana nguvu za kufikiri wala kufanya kazi. Achana na millioni 100 kutengeneza 800k.
Kwa kijana mwenye nguvu za mwili na uwezo wa kufikiri vzri ukiwa na tsh mill 10 unaweza kutengeneza 1M net profit!
 
Mkuu, uwe unaeleza pia risk ya kupoteza hiyo pesa yote - kwani si kila mtu mwenye nguvu anaweza kufanya biashara kwa mafanikio.

Pia hata wengi waliofanikiwa sana katika biashara na wana nguvu tosha, huweka sehemu ya fedha zao kwenye mifuko hii wakizingatia risk yake ndogo.
 
Savers are losers

1. Sasa hivi Vitu vimepanda Bei mara 100% toka uzi wako Uweke

2. Hela ulizotunza Zishashuka Thamani yake

3. Bati Na Cement vimepanda Bei

4. Mafuta Yamepanda Bei

Mil 20 ya Kipindi unaweka uzi ni mil 17-18 sasa hivi
 
Kweli iyo kabisa
 
Kweli kaka mambo yamekuwa magumu , Ngoja nimpigie Hangaya anioe hata 10000
 
Hii pia inawahusu wale walioacha maboma yao site bila kuyapaua huku wakiendelea kusave ili kunununua bati,nawashauri nunueni bati taratibu mzihifadhi mahal i kwani bei inaongezeka kila mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…