Leo Desemba 31, 2024 ni mwisho kwa Taasisi za Umma zinazohudumia zaidi ya Watu 100 kutumia Mkaa na Kuni Tanzania

Leo Desemba 31, 2024 ni mwisho kwa Taasisi za Umma zinazohudumia zaidi ya Watu 100 kutumia Mkaa na Kuni Tanzania

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa amezikumbusha Taasisi na mashirika yote ya Serikali yaliyopo kote nchini Tanzania ambayo yanahudumia watu zaidi ya 100, kutekeleza bila shuruti agizo lake la kuitangaza Disemba 31, 2024 kuwa siku ya mwisho kwa matumizi ya Mkaa na Kuni kwenye shughuli za Mapishi.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo mapema Leo Jumanne Disemba 31, 2024 wakati akihutubia wananchi kwenye Tamasha la Azimio la Kizimkazi 2024, linalofanyika kwa mara ya pili Ruangwa Mkoani Lindi ikiwa ni mara baada ya kuzinduliwa kwake mapema mwaka huu na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kizimkazi Visiwani Zanzibar.

Waziri Mkuu amezitaja taasisi zinazohusika na agizo hilo kuwa ni pamoja na Taasisi zote zenye kuhudumia watu zaidi ya mia moja ikiwemo Majeshi mbalimbali, Shule za bweni za Binafsi na za serikali, Magereza pamoja na Wazabuni wanaopika vyakula vya zaidi ya watu 100.
 
Hii itaongeza gharama kwenye baadhi ya tasisi kama shule na hoteli, na hivyo kuongeza gharama kwa wateja.
 
Yani nchi hii mpaka unajiuliza are these leaders serious? Yani gesi gharama ndo inazidi kupanda alaf wanataka tuhamie huko. Umeme wao sio wa uhakika.

Kufanya instalation ya mitambo ya gesi gharama zake sio masihala. Mimi walikuja kwangu niliwafukuza, nikawambia hamjajipanga..

Ni upuuzi upuuzi upuuuzi
 
Mwenye kumbukumbu vzr ataelewa kuwa haya maneno sio magen kwa mwenyeji wa Tz lbd kwa mgeni wa nchi
 
Na huku oldonyosambu tununue gesi kuwapikia Hawa wanafunzi hizo gharama serikali mtatusaidia au mnajua Tanzania yote ipo kama dar
 
Back
Top Bottom