Siku inaanza saa kumi na moja alfajiri kwa nyuzi za kujimwambafai.
Raia wanaanzisha mada za "Niko Five star hotel Dubai..nakunywa capuchino ya Brazil huku nawaza ninunue kiwanja gani wiki hii." Kumbe ukweli ni kwamba mleta mada amejifunika shuka la neti huku aking’atwa na mbu, na capuchino yenyewe ni ile ya mia mbili ya kijiweni.
Watoa maoni hawachelewi kumpiga spana: "Kaka, plasta imebubujika hapo ukutani kwako, jenga kwanza kabla ya kuwaza Brazil!"
Mchana: Soko la Kupigwa Chabo
Saa nne asubuhi hadi saa sita mchana, jukwaa linageuka kuwa chumba cha...