Jana tarehe 21 Oktoba ilikuwa ni siku ya kuapishwa kwa Mawakala wote wa vyama lakini zoezi Hilo liliibua sintohamu kiasi Cha kupelekea Mawakala 5 wa CHADEMA kupoteza uhai!
Kwamba Kuna maelekezo toka juu yalitolewa Jana hiyohiyo kubadilisha vituo vya Kuapishwa kutoka Kata kwenda Tarafa, Halmashauri na Jiji. Hii ilikuwa ni katika mbinu za NEC WAKISHIRIKIANA NA CCM na SERIKALI yao kuwanyima fursa MAWAKALA WA UPINZANI KUAPISHWA......!!!
Chanzo Cha haya yote ni kauli TATA YA RAIS MAGUFULI YA KUSEMA: Nukuu, MKURUGENZI YETOTE ATAKAYE MTANGAZA MPINZANI KUSHINDA NITAMFUKUZA KAZI.SIWEZI KUMPA MSHAHARA MKUBWA NA GARI ZURI HALAFU AMPE USHINDI MPINZANI"
Kwa hiyo kinachoonekana kwa sasa ni kila MSIMAMIZI(Mkuregenzi Jiji/Halmashauri) kuhakikisha Mawakala wa Upinzani hawaapishwi ili kurahisi wizi wa kura kwa CCM ili iwe rahisi kwao kuwatangaza Wagombea wa CCM kwa kura za kishindo!!
Kwa Hakika hili ndilo litakalo leta vurugu kubwa sana kwene Uchaguzi Mkuu wa 2020! Chochote kitakacho tokea siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi lawama zote atazibeba Magufuli, NEC na CCM.