Leo naomba mniulize chochote kuhusu mimi

Kuacha kazi nafikiria nikifika 50 au 55. Kuacha kazi kugumu sana ukiwa na madaraka. Pia kazi ndio inaniwezesha kukopa na kufungua miradi wacha nikabe kotekote
 
Mtoa mada unamiliki gari aina gani??
Je hilo unalomilik ni dream car yako?? Na je unamagari mangap??
Gari za kutembelea nazo 3, Prado ya 2008, Harrier New model ya 2005 na Vitz ya 2000 (my favorite). Kwenye biashara nina magari pia na matreka na mashine ya kuvunia mpunga.

Gari za kutembelea zote sio dream car zangu. Niliachana na magari baada ya kugundua kuwa hayana mchango mkubwa sana kwenye uwekezaji niliwekeza sana kwenye makazi yangu ya Dar ndio sehemu inayonipa furaha. Napenda sana kuishi nyumba nzuri na hiyo ni nadhiri nilijiwekea toka mdogo
 
Kuacha kazi nafikiria nikifika 50 au 55. Kuacha kazi kugumu sana ukiwa na madaraka. Pia kazi ndio inaniwezesha kukopa na kufungua miradi wacha nikabe kotekote
Ahsante sana mkuu kwa jibu zuri

Je! Una ushauri gani kwa kijana km mimi ambaye nakaribia miaka 33 lakini similiki kitu chochote cha thamani na maisha yamenipiga fimbo balaa?
 
Ahsante sana mkuu kwa jibu zuri

Je! Una ushauri gani kwa kijana km mimi ambaye nakaribia miaka 33 lakini similiki kitu chochote cha thamani na maisha yamenipiga fimbo balaa?
Bado una muda wa kujipanga pia nenda kijijini ukatafute mtaji ukiwa na malengo utatoboa usikae tu mjini bila kazi. Kaa chini andika unachotaka kukifanya kisha weka mpango mkakati ukisimamie mpk utimize.

Duniani hakuna aliyezaliwa na burungutu la pesa mkononi, wote tumezaliwa uchi vingine vyote tunatafuta. Amka jitambue utatoka tu
 
Mkuu katika matrekta yako;; embu niazime mmoja nirudi kijijini kwa babu yangu nikapambane na shamba. Nimechoka maliza sori ya kiatu changu kuzunguka mjini posta na bahasha ya kaki bila mafanikio.
 
Mpaka sasa hivi hapo ulipo umeshatembelea nchi ngapi duniani?na je kuna funza dume la jike,au funza yoyote anemuwahi mwenzake jike kwa wakati huo anaofanywa?na je we umeshawahi kuwahiwa na funza mwenzako?maana unajiita funza dume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…