Leo ndio najua David Mwakyusa bado yupo kwenye siasa

Lazima awe intelligent zingatia yafuatayo.

1.Alikuwa bosi wa muhimbili yote.
2.Alikuwa Dr wa baba wa taifa.
3.Yupo umweweni mpaka Leo.
4.Alikuwa waziri wa afya.
5.Ni profesa wa kusoma sio desa.

Je atakuwa kilaza?
Aliomba kutopewa uteuzi
 
Namba 4 & 5 kama zinabeba ujumbe mkubwa wa Siri!
 
Lazima awe intelligent zingatia yafuatayo.

1.Alikuwa bosi wa muhimbili yote.
2.Alikuwa Dr wa baba wa taifa.
3.Yupo umweweni mpaka Leo.
4.Alikuwa waziri wa afya.
5.Ni profesa wa kusoma sio desa.

Je atakuwa kilaza?
Hakuwa Mkurugenzi wa Muhimbili yote bali Mkurugenzi wa Administration.
Mkurugenzi wakati huo ni Prof Mgaya au Mbaga ambaye Ali take over from Prof Sarungi, na baada ya Hapo ni Prof Shija etc .
 
Kuhusu maendeleo ya Jimbo, nafikiri alikuwa anawaza ki haki haki , na kwamba serikali itafanya inachotakiwa bila yeye kutumia influence yake.
Ndio maana siasa ilimshinda
 
Du Wanyakyusa ...mkiwa na isingizi mlale!

Mwenzako katupotosha ...wewe unatudanganya ,hebu pitia vizuri Uzi wako na fact ulizoweka!

Upotoshaji xUongo+ kimbelembele=!
Kwenye uwaziri wakati wa Mkapa kweli kapotosha ila mengine yote ni kweli tupu.
 
Huyu ni miongoni mwa wale maprofesa wa Muhimbili waliopeana uprofesa kwa mtindo wa "annual increment" bila kuwa na PhD. Hana PhD huyu, lakini ni profesa! Wenzake kama yeye ni pamoja na akina Sarungi, hata huyu Mkurugenzi wa sasa wa Muhimbili anaitwa Museru na wengine wengi wa Muhimbili mnaosikia wakiitwa maprofesa hawana PhD. Wapo wachache wenye PhD, hasa wale waliopitia mkondo wa social sciences (kama vile Dr Semakafu, mwalimu wa DS) na wale wa maabara (hasa upande wa madawa, yaani pharmacy). Wale wa tiba waliamua kujikweza na kujiwekea kasheria kao ka annual increment, unapanda cheo kila baada ya miaka 3 hadi unakuwa profesa!
 
Huyu Mzee anaheshimika sana halafu mkimya sana.
Kuna hafla fulani tuli hudhuria Jumba jeupe huyu Mzee alikuwepo, ilikua kipindi cha kaka Ben.
Asee Mawaziri na wazito wengine wao ndio walikua wanamfuata kumpa mkono...yeye hana shobo.
 
Kuna wilaya moja tu ya Rungwe yenye majimbo mawili ya uchaguzi - Rungwe (awali Rungwe Magharibi) na Busokelo (awali Rungwe Mashariki) kama ulivyobainisha. Busokelo ni halmashauri tu ndani ya wilaya ya Rungwe, si wilaya!

Na kwahiyo wilaya ya Rungwe ina halmashauri tatu: halmashauri ya wilaya ya Rungwe, halmashauri ya Busokelo na halmashauri ya Mji Mdogo Tukuyu.
 
Hatuna jimbo la Rungwe West tokea 2015, na Mwakyusa si mbunge kwa sasa. Fuata taarifa sahihi na rasmi za Tume ya Uchaguzi, sio za Wikipedia!
Ni msabato? Sikufahamu hilo. Kwa iyo siyo mmbunge? Mbona kwenye google Wikipedia wanamtambua kama mbunge wa sasa Rungwe west. Msaada please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…