Leo ndio najua David Mwakyusa bado yupo kwenye siasa


Kuweka kumbukumbu sahihi

Profesa David Mwakyusa alikuwa waziri wa afya kwenye awamu ya nne ya mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kutoka mwaka 2005 mpaka 2010 sio kwa Rais Mkapa kama ulivyosema

Pia Busokelo sio wilaya, bali ni halmashauri ndani ya wilaya ya Rungwe

Ndani ya wilaya ya Rungwe kuna halmashauri mbili
1. Halmashauri ya Rungwe

2. Halmashauri ya Busokelo

Pia ndani ya wilaya ya Rungwe kuna majimbo mawili ya uchaguzi

1. Jimbo la Busokelo

2. Jimbo la Rungwe
 

..lakini taratibu zote zina advantage na disadvantage zake.

..wanaotibu wagonjwa, kwa maana ya clinical work, na kufundisha, wana umuhimu sawasawa na wale wanaofanya utafiti / research na hatimaye kutunukiwa PhD.
 
Hakuwa Mkurugenzi wa Muhimbili yote bali Mkurugenzi wa Administration.
Mkurugenzi wakati huo ni Prof Mgaya au Mbaga ambaye Ali take over from Prof Sarungi, na baada ya Hapo ni Prof Shija etc .

..wakurugenzi ninaowakumbuka ni Prof.Swedi Mwankemwa, Prof.Philemon Sarungi, Prof.Gabriel Mwaluko, Prof.Iddi Mmbaga, Prof.David Mwakyusa [ kaimu mkurugenzi], Prof.Masele..wakati huo ilikuwa ni Shirika la Afya Muhimbili.
 


Halmashauri mbili au tatu?
 
..lakini taratibu zote zina advantage na disadvantage zake.

..wanaotibu wagonjwa, kwa maana ya clinical work, na kufundisha, wana umuhimu sawasawa na wale wanaofanya utafiti / research na hatimaye kutunukiwa PhD.
Wala sio sawa. Hata vyuo vingine kuna wataalamu wanaofanya taaluma zao (mfano sheria) na kufundisha lakini hawapewi uprofesa kwenye silver platter kama walivyopeana akina Mwakyusa. Hii ni magumashi ya kujikweza tu.
 
Hakuna la maana walilofanya
 
Na huyu PhD holder mwenye thesis special yeye ni msomi wa aina gani na ngeli halipandi?
Huyu alipewa desa la mwanafunzi wa miaka ya nyuma na Dr Akwilapo aliyekuwa msimamizi wake akakopi mpk jina.

Ndiyo maana unaona Dr Akwilapo akalamba ukatibu mkuu wa wizara ya elimu kama shukurani.
 
Wala sio sawa. Hata vyuo vingine kuna wataalamu wanaofanya taaluma zao (mfano sheria) na kufundisha lakini hawapewi uprofesa kwenye silver platter kama walivyopeana akina Mwakyusa. Hii ni magumashi ya kujikweza tu.

..wahadhiri ambao wamejikita kwenye kutibu wagonjwa wodini na kwenye theatre ni muhimu.

..wahadhiri ambao wanajishughulisha na masuala ya utafiti / research work nao ni muhimu.

..kumbuka kwamba lengo la kitivo husika ni kutoa wahitimu watakaofanya kazi za wodini na theatre, pamoja na wahitimu watakaojikita kwenye utafiti / research.
 
Wala sio sawa. Hata vyuo vingine kuna wataalamu wanaofanya taaluma zao (mfano sheria) na kufundisha lakini hawapewi uprofesa kwenye silver platter kama walivyopeana akina Mwakyusa. Hii ni magumashi ya kujikweza tu.
Unapo fanya many research projects and publications katika professional journals eg; lancet etc unapewa uzito zaidi kuliko anaefanya thesis moja na kupata PhD. Na hasa uzito wa chozen synopsis. Peer reviewer wanaweza kufanya research findings reviews zikatikisa.
 
Watu kutoka Mbeya waliofanya utopolo ni mwakiyembe na Tulia ackson
 
Kumbe wasabato nao ni wanasiasa? Sikujua
 
Watu kutoka Mbeya waliofanya utopolo ni mwakiyembe na Tulia ackson

Tuwe na heshima kwa viongozi wetu wa sasa na wastaafu

Dr Harrison Mwakyembe na Dr Tulia Ackson wote wamefanya mambo makubwa kwa wakati wao kwenye sehemu mbalimbali walizotumikia taifa hili, kuanzia chuo kikuu cha Dar es salaam mpaka kwenye bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
Wala usipate tabu tumeshaelewa kwamba unamalizia muda wa bando kabla kampuni ya simu hawajakata ndo maana unajiandikia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…