Leo ni Bunge la Wanaume watupu, wabunge wanawake wanahudhuria mkutano wa Rais Samia

Leo ni Bunge la Wanaume watupu, wabunge wanawake wanahudhuria mkutano wa Rais Samia

2025 Hakuna atakaerudi bungeni wakizidi Sana 10 wengi ni chaguo la tume
 
Ina maana hata wale covid 19 wamekwenda huko...
 
Bunge la 12 Mkutano wa 3 Kikao cha 47 kinaendelea leo bila uwepo wa wabunge wanawake ambao wameelekea ukumbi wa Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa Wanawake wote bila kujali itikadi na Rais wa JMT mh Samia.

Hakuna kupigiana makofi waka mbwembwe zozote ni moja kwa moja kwenye mada.

Pia soma > LIVE - Dodoma: Rais Samia kufanya mkutano na Wanawake ukumbi wa Jakaya Kikwete
Mama Samia alisema wanawake ni wambea kuliko wanaume. Tena wa ccm ndiyo wadaku sana. Tegemea makofi na mipasho ya kutosha leo toka bungeni
 
Lini MATAGA mtakaa kuleta pendekezo la kumuongeza Samia muda hadi achoke mwenyewe?
 
C yanduane tu yenyewe kwa yenyewe hayo Mapiga porojo
 
We mwanamke ee
Kumbe wanaopigaga makofi na mbwebwe za furaha nyingi ni wabunge wanawake, naona pia bunge limekosa harara, kumetameta, haliko charged kivile, jamani jinsia moja kumbe haifai katika kuleta chachandu na shamrashamra, yaani sawa na wali bila nazi.. Basi tuwaunge mkono sanaaa wanawake walau wafikie hata 50/50 ikishindikana hata 40%/60%.. Wanawake muhimu sanaaaa sanaaa nimeona leo aisee.. Bunge liko kama Baba yuko pekee yake nyumbani, mama kasafiri, basi ukimyaaaa umetawala, nuru haiko kivilee, kumepoozaa.. Hakika wanawake Mungu kawapa mpako wa kipekeee, wanaume sio kitu kabisaa bila wanawake. Mungu mbariki sana Rais wetu na Mama yetu Samia Suluhu Hassan na wabariki wanawake wote dunia nzima. Amen. 🔰💛💚👏👏🙏🙏🙏 Kazi iendelee
 
Back
Top Bottom