Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Nyerere au Magufuli?

wacha ujinga wewe.
 
Ikifika March 17 tunaelekea Butiama. We always loose focus hatuna Habare!!!
 
Unashangazwaje kwa ufafanuzi ambao umekwisha kutolewa?!!!

Wameamua kuuzima mwenge Chato kwa ajili ya pia kumkumbuka hayati JPM....

HASTA LA VICTORIA EL COMANDANTE JKN🙏
... kumbukumbu zina utaratibu na cycle zake. Huwezi kujiamulia tu from nowhere kufanya kumbukumbu. Kwa mfano, leo Jpm anakumbukwa siku ya kifo chake? Ya kuzaliwa kwake? Au?
 
Duuuh, hii haikuwa sawa hata Kidogo.

Yule mtu alijijenga sana kwenye kila idara kupitia watu wa nyumbani.

Hili liwe fundisho kwa taifa ,Katiba tuliyo nayo inajenga viongozi madikteta. Wanaamua wanachotaka bila kuzuiwa wala kumsikiliza mtu.
Yule mtu aliyeondoka awamu ya tano alifanya mambo mengi mazuri lakini angefanikiwa kukalia kiti na meza kwa miaka kumi nchi hii ingekua na ukabila mbaya sana.

Tunahitaji Katiba Mpya inayoweza kumpata kiongozi na sio mtawala .
Hata akitoka kabila kubwa asiwe na fursa ya kujijenga kikabila au kidini au kijinsia.
Katiba hii inatoa mwanya kwa Mkuu wa jamii Kujijenga ama Kikabila au Kijinsia au Kirafiki au Kidini bila kuzuiwa na mtu au chombo chochote.

Kwa Katiba hii ipo siku nchi hii itapata inachokitafuta yaani Dikteta kamili. Na dikteta huyo ataumia ama Ukabila,au udini au jinsia.


Miaka yote Mwenge unazimwa Butiama Leo Mwenge unazimwa Chato.

Tunamuenzi Mwalimu na kumsifu sio kwa sababu ya maendeleo bali aliweka maslahi ya Taifa mbele.
Alikaa madarakani miaka 23 lakini akastaafu akiwa na maisha ya kawaida. Hakujiuzia Mali za Umma . Hakujimilikisha ardhi kubwa na majumba wala mahoteli kama hao wengine wote akiwemo huyo aliyetukuzwa kuliko.

Leo Viongozi wa Nchi maskini ya Kijamaa ni Mabepari wa kutupwa.
Awamu ya Tano watu walikua wanapata ukuu wa Mkoa au wilaya kwa miaka mitatu mtu ni Bilionea na haulizwi na mtu kwa sababu tu anavunja Katiba na kujifanya mzalendo wa kutengeneza maadui feki.

Mwalimu alijitahidi kuishi maisha yanayoendana na hali ya uchumi wa watanzania.
Leo sio mbunge sio Mkurugenzi sio diwani wote wanawaza kujinufaisha kupitia mgongo wa CCM na serikali yake.

Waliomshauri Mama nadhani Mzimu wa Mwalimu utawaandama mana wameudnganya umma kuwa wanamuenzi KUMBE Wanamuenzi yule aliyewapa vyeo na ubunge na nafasi za ukaji kwa kuwahujumu wapinzani. Kuna wabunge na madiwani wasingepata nafasi kama sio uporaji ule na uchafuzi wa mwaka 2020. Hao wanasherehekea dhulma ya kitaifa ya mwaka 2020.



Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Mtateseka sana, heshima ya JPM ni kubwa!
Baada ya Nyerere ni JPM Tanzania!
Hawa akina Kikwete hata wakifa leo, kumbukumbu yake ilishafutika
 
nilichokigundua hapa, haters wa magufuli hua mnatamani viongozi wa serikali wawaunge mkono kwa kila kitu

mngetamani kuona magufuli hakumbukwi kwa chechote

mngetamani kuona anatukanwa hadharani na viongozi aliowaacha

nikuulize, tukio la mwenge kuzimwa lina uhusiano gani na kumbukumbu ya baba wa taifa?

huoni ingekua ni upotevu wa pesa za umma, viongozi kua sehemu mbili tofauti? yaani wengine wawe kwenye mwenge chato na wengine waende butiama!

mbona sioni tatizo!

najua kilichowachukiza ni samia kwenda kwenye kaburi la mtangulizi wake.
 
Unafahamu kwa nn mwenge iliamuliwa uzimwe Oct 14 kila Mwaka? Kama hujui unachoongea kaa kimya!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…