Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Nyerere au Magufuli?

Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Nyerere au Magufuli?

Ni upumbavu wa Hali ya Juu, yaani leo hii Magufuli ndio achukue nafasi ya Mwalimu?

Hivi mama hawezi kufikiri kwamba timu ya Mwendazake inamuendesha inavyotaka?

Yaani kapigwa na kuaminishwa propaganda kwamba wasukuma ndio wanaamua Rais? Miaka yote kabla ya Uhuru walikuwa wanaamua Rais?

Magu alipata 58% za kubumba dhidi ya Lowassa kwa nini wasukuma hawakumpa aailimia zote? Huu ni upuuzi na dhihaka kwa Marehemu mwalimu Nyerere.
wacha ujinga wewe.
 
Wanasema leo ni kumbukumbu ya Kifo cha Nyerere lakini viongozi wote wakubwa wameenda kutembelea na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Magufuli. Kwahiyo siku ya kumbulumbu ya kifo cha Magufuli watakwenda Butiama kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Nyerere? Au walitaka kutuonesha kuwa wamelijengea nyumba kaburi la Magufuli? Sijaelewa!
View attachment 1973955View attachment 1973956View attachment 1973957
Ikifika March 17 tunaelekea Butiama. We always loose focus hatuna Habare!!!
 
Unashangazwaje kwa ufafanuzi ambao umekwisha kutolewa?!!!

Wameamua kuuzima mwenge Chato kwa ajili ya pia kumkumbuka hayati JPM....

HASTA LA VICTORIA EL COMANDANTE JKN🙏
... kumbukumbu zina utaratibu na cycle zake. Huwezi kujiamulia tu from nowhere kufanya kumbukumbu. Kwa mfano, leo Jpm anakumbukwa siku ya kifo chake? Ya kuzaliwa kwake? Au?
 
Yee mwenyewe kapigwa bumbuazi kwa hz akili za viongozi wetu[emoji848]
20211014_143500.jpg
 
Duuuh, hii haikuwa sawa hata Kidogo.

Yule mtu alijijenga sana kwenye kila idara kupitia watu wa nyumbani.

Hili liwe fundisho kwa taifa ,Katiba tuliyo nayo inajenga viongozi madikteta. Wanaamua wanachotaka bila kuzuiwa wala kumsikiliza mtu.
Yule mtu aliyeondoka awamu ya tano alifanya mambo mengi mazuri lakini angefanikiwa kukalia kiti na meza kwa miaka kumi nchi hii ingekua na ukabila mbaya sana.

Tunahitaji Katiba Mpya inayoweza kumpata kiongozi na sio mtawala .
Hata akitoka kabila kubwa asiwe na fursa ya kujijenga kikabila au kidini au kijinsia.
Katiba hii inatoa mwanya kwa Mkuu wa jamii Kujijenga ama Kikabila au Kijinsia au Kirafiki au Kidini bila kuzuiwa na mtu au chombo chochote.

Kwa Katiba hii ipo siku nchi hii itapata inachokitafuta yaani Dikteta kamili. Na dikteta huyo ataumia ama Ukabila,au udini au jinsia.


Miaka yote Mwenge unazimwa Butiama Leo Mwenge unazimwa Chato.

Tunamuenzi Mwalimu na kumsifu sio kwa sababu ya maendeleo bali aliweka maslahi ya Taifa mbele.
Alikaa madarakani miaka 23 lakini akastaafu akiwa na maisha ya kawaida. Hakujiuzia Mali za Umma . Hakujimilikisha ardhi kubwa na majumba wala mahoteli kama hao wengine wote akiwemo huyo aliyetukuzwa kuliko.

Leo Viongozi wa Nchi maskini ya Kijamaa ni Mabepari wa kutupwa.
Awamu ya Tano watu walikua wanapata ukuu wa Mkoa au wilaya kwa miaka mitatu mtu ni Bilionea na haulizwi na mtu kwa sababu tu anavunja Katiba na kujifanya mzalendo wa kutengeneza maadui feki.

Mwalimu alijitahidi kuishi maisha yanayoendana na hali ya uchumi wa watanzania.
Leo sio mbunge sio Mkurugenzi sio diwani wote wanawaza kujinufaisha kupitia mgongo wa CCM na serikali yake.

Waliomshauri Mama nadhani Mzimu wa Mwalimu utawaandama mana wameudnganya umma kuwa wanamuenzi KUMBE Wanamuenzi yule aliyewapa vyeo na ubunge na nafasi za ukaji kwa kuwahujumu wapinzani. Kuna wabunge na madiwani wasingepata nafasi kama sio uporaji ule na uchafuzi wa mwaka 2020. Hao wanasherehekea dhulma ya kitaifa ya mwaka 2020.



Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Mtateseka sana, heshima ya JPM ni kubwa!
Baada ya Nyerere ni JPM Tanzania!
Hawa akina Kikwete hata wakifa leo, kumbukumbu yake ilishafutika
 
Mkuu,
1. Usi-panic,
2. Kwani kulikuwa na ulazima gani wazimie Mwenge Chato na si Butiama ambako ndo uhalisia wa tarehe ya kumbukizi ya tukio?
3. Au asingeenda leo lbd Mwendazake angefufuka na kuona Mh Rais aliyempokea kijiti hajamtembelea akiwa mfu?
4. March 17 watafanya nini cha tofauti na walichokifanya leo kwenye tarehe ambayo haireflect uhalisia wa kumbukizi ya tukio?, huoni hayo yatakuwa matumizi mabaya ya fedha za wanyonge mnaowakamua tozo kila kukicha?
5. Unadhani Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa soku ya leo amependezwa na hili hata kama hajatamka wazi?

Mjirekebishe.... Planne wenu ni hopeless kwa makusudi au kwa njaa zake za kutengeza activity za per diem na usikute mmejilipa sitting allowance...Bure kbs nyie!!
nilichokigundua hapa, haters wa magufuli hua mnatamani viongozi wa serikali wawaunge mkono kwa kila kitu

mngetamani kuona magufuli hakumbukwi kwa chechote

mngetamani kuona anatukanwa hadharani na viongozi aliowaacha

nikuulize, tukio la mwenge kuzimwa lina uhusiano gani na kumbukumbu ya baba wa taifa?

huoni ingekua ni upotevu wa pesa za umma, viongozi kua sehemu mbili tofauti? yaani wengine wawe kwenye mwenge chato na wengine waende butiama!

mbona sioni tatizo!

najua kilichowachukiza ni samia kwenda kwenye kaburi la mtangulizi wake.
 
nilichokigundua hapa, haters wa magufuli hua mnatamani viongozi wa serikali wawaunge mkono kwa kila kitu

mngetamani kuona magufuli hakumbukwi kwa chechote

mngetamani kuona anatukanwa hadharani na viongozi aliowaacha

nikuulize, tukio la mwenge kuzimwa lina uhusiano gani na kumbukumbu ya baba wa taifa?

huoni ingekua ni upotevu wa pesa za umma, viongozi kua sehemu mbili tofauti? yaani wengine wawe kwenye mwenge chato na wengine waende butiama!

mbona sioni tatizo!

najua kilichowachukiza ni samia kwenda kwenye kaburi la mtangulizi wake.
Unafahamu kwa nn mwenge iliamuliwa uzimwe Oct 14 kila Mwaka? Kama hujui unachoongea kaa kimya!!!!
 
Back
Top Bottom