Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, hawakufanya hayo, japo kuna mauaji na utekaji chini ya utawala wao.
Wakati wa Mwalimu, hata waliotaka kumpindua walishtakiwa. Hawakutekwa wala kuuawa.
Wakati wa Mkapa, polisi waliua Wazanzibari, hata yeye Mkapa amelisema kwenye kitabu chake, na alijutia, na wala hakuamrisha wala kubariki. Ndivyo ilivyokuwa kwa Kikwete juu ya Ulimboka na mauaji ya kule Arusha na Morogoro. Kikwete hakuamrisha wala hakubariki. Kuna hatua alichukua za ndani, japo umma haukuambiwa. Na polisi walipoonekana kuendelea kufanya uovu, aliamua kuunda tume, na polisi walishtakiwa (ref. uharamia wa polisi dhidi ya wafanyabiashara wa madini).
Marehemu, waliokuwa wanafanya unyama huo, aliwapandisha vyeo. Ni Bashite pekee aliamua kumwacha baada ya kuona US wamejua uhalifu wake wote.