Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Nyerere au Magufuli?

Hawataisha kama Tanzania day inafanyika Kenya wajinga wataishaje.
sawasawa bwana mataha...

ila lazima mjue, nyerere hakua kwa ajiri ya watu wa butiama tu

ni wa taifa zima, so kumbukumbu ya maisha yake itafanyika sehemu yeyote ndani ya tz.
 
Upo Ukweli watu wanaolipwa humu kutetea UOZO wewe ni mmoja wapo. Hii mada inatia simanzi sana jinsi Mwalimu Nyerere alivyokosewa adabu leo. Siku ya Magufuli ni March 17. Inakuwaje CCM wamkosee adabu Mwalimu?

Tuonyeshe Wosia/Usia wa Hayati Mwalimu Nyerere uliosema “maadhimisho ya kuzima Mwenge ni marufuku kufanyika popote nje ya maeneo ya Kaburi langu (isomeke lake) !...??
 
kama wewe ni mtanzania na una akili timamu, naomba unitajie raisi ambae hakufanya ulichoandika hapa.
Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, hawakufanya hayo, japo kuna mauaji na utekaji chini ya utawala wao.

Wakati wa Mwalimu, hata waliotaka kumpindua walishtakiwa. Hawakutekwa wala kuuawa.

Wakati wa Mkapa, polisi waliua Wazanzibari, hata yeye Mkapa amelisema kwenye kitabu chake, na alijutia, na wala hakuamrisha wala kubariki. Ndivyo ilivyokuwa kwa Kikwete juu ya Ulimboka na mauaji ya kule Arusha na Morogoro. Kikwete hakuamrisha wala hakubariki. Kuna hatua alichukua za ndani, japo umma haukuambiwa. Na polisi walipoonekana kuendelea kufanya uovu, aliamua kuunda tume, na polisi walishtakiwa (ref. uharamia wa polisi dhidi ya wafanyabiashara wa madini).

Marehemu, waliokuwa wanafanya unyama huo, aliwapandisha vyeo. Ni Bashite pekee aliamua kumwacha baada ya kuona US wamejua uhalifu wake wote.
 

Chief, unaongea kama umekunywa mataputapu!!

Are you sure you’re doing well?
 
MACCM yaana laana kamwe hawajawahi kumuheshimu Nyerere si wangetenga hela wamjengee jengo la Mwalimi Nyerere Foundation yenyewe yanajijengea mijumba ufukoni na kupeana magari huku yakitumia jina lake nenda Butiama ukaone kulivyochakaa wameshindwa kutenga hata milioni 10 kwa mwezi kupafanya pawe green majambazi makubwa uone siku yake kwenda kumlinganisha na mwendazake wa chato
 

Huyu Nyerere uliyemzungumzia hapa ni wazi ni wa kwa fantasy zako! Has nothing to do with reality!!!

Nyerere wa Mzee Kambona??
Nyerere wa Mzee Hanga??
Nyerere wa Mama Bibititi??
Nyerere wa Mzee Karume??

Dah!!

Allah awajaalie mapumziko mema wale wote waliotangulia mbele za haki...Ameen!
 
Kama mwenge siyo lazima uzimwe Butiama, basi ungezimwa Chato ,lakini viongozi kuanzia Rais wangekuwa Butiama kuweka mashada, Kama ishara ya kuheshimu Nyerere day. Wamemwacha mama Maria peke yake mashada wanaweka kwa Magufuli! Mwalimu amekosewa adabu.

Una hakika Mama Maria Nyerere yuko Butiama?
 
Ha ha bora aliondoka dunia kwa laana ya kuuwa watu na kufunga na kufirisi watu
 
Nilikuwa na mgeni kutoka magharibi huko ugaibuni aliniuliza pia kama Magufuli na Nyerere ni mtu mmoja.

Aaa ikabidi namie nipige siasa kumuweka sawa.

Leo ni kweli kumbukizi ya kifo chake,lakini huitumia kitaifa kufanya shughuli za uzimwaji wa mwenge wa uhuru.

Hivyo popote unapotokea unazimiwa hapo,basi hiyo ndiyo theme mengineyo huwa ni matukio tu, kama hili la leo.

Shughuli ni kuzimwa mwenge,kwa vile linafanyikia chato basi kiutanzania kwa vile kuna mwamba wetu amepumzika pale huwa mila na desturi kuzuru kaburi na kumuombea marehemu.

Ni upendo,umoja na mshikamano tu wa kitaifa.
 
ok sawa ngoja nifanye kukuelewa

aliyemteka na kumtesa ulimboka yuko jela gani hapa tz? maana hakutumwa na kikwete

aliyetoa amri ya kuuwawa wazanzibari si mkapa sio?(kwa mujibu wako, maana umeandika hakubariki), emu tuambie aliyetoa amri hiyo ni nani nayuko jela gani hapa tz?

unayafahamu mauaji ya mwembe yanga?
 
Tuonyeshe Wosia/Usia wa Hayati Mwalimu Nyerere uliosema “maadhimisho ya kuzima Mwenge ni marufuku kufanyika popote nje ya maeneo ya Kaburi langu (isomeke lake) !...??
Kwahiyo imeandikwa Nyerere day akumbukwe Magufuli.
 
Baba wa Taifa leo amefanyiwa "daylight robbery"

Yaani CCM watu wa hovyo sana, kumbukizi ya siku ya Baba wa Taifa lakini ajenda yote anajadiliwa baba wa kambo
Nyerere na magufuli ni dugu moyaa
The legacy
 
Daaah hatari aisee hii chuki imepita kiwango

Hii ndio yenyewe!! Nzuri mno kwa viwango vya Binaadam!

Inafaa sana maana itakupandisha juu ya kilele chake kiasi kwamba ukianguka kutoka hapo ni unapasuka tu!!

Tuwaache wajiachie, hakuna mbeleko ya kuwabeba!!
 
Katika watu ambao hawakuwa na falsafa yo yote ni Magufuli! Alikuwa hatabiriki, mtu mwenye chuki, mbinafsi na mwenye visasi!

Magufuli hastahili hata chembe kulinganishwa na Nyerere!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…