Leo ni mwaka mmoja kamili toka kifo cha Shangazi wetu kilipotokea kwa kutumbuliwa utumishi Serikalini. Inasikitisha

Leo ni mwaka mmoja kamili toka kifo cha Shangazi wetu kilipotokea kwa kutumbuliwa utumishi Serikalini. Inasikitisha

Huyu Mama alikuwa Afisa Muuguzi Mkunga, mwenye elimu ya stashahada toka KCMC COLLEGE na shahada Muhimbili university.
Alifariki akiwa na miaka 58 (miaka 2 kabla ya umri wa kustaafu), kwa shinikizo la damu na heart stroke.

Kabla ya kupata maradhi haya alitumbuliwa UTUMISHI wake na serikali kutokana na "INCONSISTENCY" kwenye cheti chake cha form four

Kutumbuliwa kwake kukaenda sambamba na kukosa mafao yake kwa utumishi wa miaka 33 ndani ya serikali.

FUNZO:
Sio kila hukumu kwa mujibu wa sheria ni hukumu kwa mujibu wa haki.

RIP - SHANGAZI

Usijali muda si mrefu atakutana na Msababisha Kutumbuliwa Kwake huko aliko Mawinguni na akiweza akionana nae tu amuulize Kipo wapi sasa? Mbona hata Yeye Israeli Mtoa Roho nae Kamtumbua asiwepo nasi hapa duniani tena Kiulaini tu?
 
Huu utaratibu wa Kila mtu kujiona anapaswa kufikiriwa ndiyo ulokua unalalamikiwa miaka nenda rudi,unajisikiaje mtu anafanya kazi kwa Vyeti vya ujanja janja then wewe mwenye Vyeti visivyo na shaka unahangaika upo uraiani.

Hili fagio bado lilipaswa kuendelea tu na hakuna huruma iwe umefanya kazi hata miaka100,lazma uwajibishwe.

We huoni kiasi gani manesi feki wanavyokatiza maisha ya wagonjwa wangapi mahospitali?

Nimeshuhudia watu wakitengeneza Vyeti feki na hata Mimi nishaombwa cheti changu kieditiwe mtu aingizwe kwenye system na Mkubwa mmoja bwana wake mdada aliyekua rafiki yangu.

Haya Mambo ukiangalia kijujuu na kihuruma huruma nchi haitoenda na utaishiwa kulaumiwa tu Kama utawala wa J.k
Kwa hapa hata mi namsapoti, huna cheti unakula salary, posho then unakuja kututambia sisi wenye vyeti original[emoji848]

Kwa hili Magu nampa[emoji122][emoji122][emoji122]

Na ndio maana jamaa pia ana mazuri yake mengi tu
 
Tukufe si neno la Kiswahili.

Kufa ni sehemu ya the second law of thermodynamics.
Nilijua utalizungumzia hilo neno, na ndio lengo la kuweka kwa herufi kubwa, siko serious masaa yoote, nilitia masihara ndani yake..

Bado hujanijibu chief, nisaidie mie niliyekimbia fizikia.
 
Poleni sana RIP Shangazi. Baba wa udhalimu kaumiza Watanzania wengi sana. Mtu amefanya kazi miaka 33 bila matatizo yoyote ile kufukuzwa kazi kwa cheti cha form four ambacho hakihusu kitu na kazi yake ya miaka 33. Mwenyezi Mungu Mkubwa 🙏🏾
Huyu Mama alikuwa Afisa Muuguzi Mkunga, mwenye elimu ya stashahada toka KCMC COLLEGE na shahada Muhimbili university.
Alifariki akiwa na miaka 58 (miaka 2 kabla ya umri wa kustaafu), kwa shinikizo la damu na heart stroke.

Kabla ya kupata maradhi haya alitumbuliwa UTUMISHI wake na serikali kutokana na "INCONSISTENCY" kwenye cheti chake cha form four

Kutumbuliwa kwake kukaenda sambamba na kukosa mafao yake kwa utumishi wa miaka 33 ndani ya serikali.

FUNZO:
Sio kila hukumu kwa mujibu wa sheria ni hukumu kwa mujibu wa haki.

RIP - SHANGAZI
 
Usema kweli, hili lilikuwaga tatizo sana na liliyumbusha sana familia za watu. Kwa hili uongozi ulichemka haukutumia hekima
Kabisa. Hata kama walikos sifa za kuwa na cheti cha kidato cha nne, hekima ingetakiwa, kwa kuwastaafisha kwa manufaa ya umma, wangepewa kiinua mgongo chao na kupotelea mtaani. Otherwise waliotumbuliwa kwa kukosa cheti cha CSEE ni wengi waliathirika kwa namna moja ama nyingine
 
Huu ni moja shuhuda kww yule mumwitae shujaa wa Africa(kwanza sidhani Kama anastahili hio title) alikuwa husika na vifo vingi Sana vya watu .

So tuache unafiki

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Pole Sana Mkuu, nami nina Dada yangu ambae yeye ilikuwa imebaki miaka 8 astaafu. Yeye alitumia cheti kisicho chake kujiunga na Chuo cha Ualimu, pamoja na kwamba hii Kozi ya Ualimu alisoma yeye mwenyewe. Huyu ajafariki lakini maisha anayoishi yanatia Simanzi.
Inapendeza hongera Magu
 
Mkuu fasiliteta Wahanga wengine walitumia tu cheti cha kidato cha nne, kujiunga na chuo, hivyo ametumikia Kozi husika kwa Kipindi chote cha Kozi na kuhitimu. Huyu utamwita ni "FEKI"??!!
Anyway kwa Wahanga wa aina hii Serikali ingekuwa na jicho la Huruma kuwalipa japo Viinua Mgongo vyao.
Swali
Kufanya hivyo ilikuwa legal au illegal??
 
Nchi ngumu hii........maamuzi yoyote lazima yawaathiri wengine na wengine wanufaike
 
Polen,ila mtesi wenu nae kaondoka,kunywen bia.

Ambajo jiwe hakujua,ni kuwa aliwatumbua watu ambao wamesoma vyuo na wakafaulu,tatzo lilkuwa cheti cha form 4,kwahyo ujuzi waliusomea na wakafaulu
Je system inataka hivyo maana kila mtu anaweza pita njia hii je wote tupite tutapata ajira??

tusisapoti dhambi hata kama ujuzi aliosomea miaka 200 we under the system.
 
Pole Sana Mkuu, nami nina Dada yangu ambae yeye ilikuwa imebaki miaka 8 astaafu. Yeye alitumia cheti kisicho chake kujiunga na Chuo cha Ualimu, pamoja na kwamba hii Kozi ya Ualimu alisoma yeye mwenyewe. Huyu ajafariki lakini maisha anayoishi yanatia Simanzi.
"Alitumia cheti kisicho chake kujiunga na chuo cha Ualimu " hiyo sentensi imenishtua
 
Kwa hapa hata mi namsapoti, huna cheti unakula salary, posho then unakuja kututambia sisi wenye vyeti original[emoji848]

Kwa hili Magu nampa[emoji122][emoji122][emoji122]

Na ndio maana jamaa pia ana mazuri yake mengi tu
Wanaambukizana ujinga humu
 
Nilijua utalizungumzia hilo neno, na ndio lengo la kuweka kwa herufi kubwa, siko serious masaa yoote, nilitia masihara ndani yake..

Bado hujanijibu chief, nisaidie mie niliyekimbia fizikia.
Under ceteris paribus, given time and without compensating maintenance, the entropy of any closed system will tend to increase and not decrease. Such is the intricate and inherent nature of the defining feature of the arrow of time.
 
Back
Top Bottom