#COVID19 Leo ni siku ya 23 tangu nipone au kupata nafuu na ugonjwa wa Covid-19

#COVID19 Leo ni siku ya 23 tangu nipone au kupata nafuu na ugonjwa wa Covid-19

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Jamani mimi leo naandika ni siku ya 23 tangia nipone au kupata nafuu na ugonjwa wa korona, pia nikamwambukiza mke wangu na mamaangu mzazi alikuwa amekuja kututembelea pia ikampiga na binti wa kazi pia aikumbakiza na shemeji alikuwa amkuja salimia naye akubaki salama, yaani nyumba nzima tulichapwa na Korona kasoro watoto wangu wadogo mmoja darasa la nne na mwingine lasaba.

Nilipo anza kuumwa nilikwenda hospitalini na kupimwa UTI, Maleria na Tayfodi majibu yote yakaja negativu na kijana mmoja ambaye ni docta katika ile hospitali akaniambia utakuwa unauchovu tu kapumzike. (sijui alikuwa na maana ya mapumziko yapi)

Jamani mziki wa korona ni noma, maumivu yake ni balaa ndiyo maana wazungu hawaombi maji. Naomba niwape uzoefu hili tusaidiane kupona na kuacha kujinyonga.

Mimi nina rafiki zangu wawili tofauti ambao wapigwa na Korona ambao walinipa uzoefu. Nilianza kuumwa sana kama siku 4 za kwanza lakini nilikuwa nikitupia diclopa, sasa ilikuwa hivi, diclopa mtu mzima ni 1 x 2 lakini kama nimemeza asubui saa 1 ikifika saa 7 nguvu ya diclopa inakwisha. Hivyo kwa matumizi ya kitabibu ya 1x2 mimi nikawa najipa 1 x 3.

Homa ni kali, kichwa kinauma sana na kugonga, misuli inakaza hasa kiunoni, yaani hiyo misuri ndiyo inakuvizia kukukarisha chini na mwili unakuwa kama kuna polisi au wakola wamekubana mwili mzima, nika wanataka kuku Geoge Floid hivi, hapo tayari nilikuwa siwezi kumgusa shemeji yenu au kuamsha dude kokote. Dalili nyingine hii ilikuwa inatokea zaidi jioni pua zinauma ukivuta punzi nikama zizina washa hivi.

Sasa nakumbuka siku ya 6 usiku nikaanza kuota ndoto nawaona Ansesta yaani kama wananipungia hivi mikona wengine kama wananiita wakiniuliza unakuja? ndotoni nilikataa nikachomoa maana nikawaambia mbona mke wangu anamimba.

Nilivyostukatu akili ndiyo ikanijia kuwa hii ni UVIKO na kugundua kuwa nipo kwenye noma. Ilikuwa saa 9:25 usiku nilishindwa kulala. nikakumbuka rafiki angu ambaye aliumwa Korona na kupona aliwai kunipa dalili nyingine ya kupoteza kunusa.

Nikamwamsha mke wangu nikamwambia mimi naumwa akanijibu ndiyo najua unaumwa nikamjibu naumwa korona, akastuka kidogo nikamwambia nipe pafyumu yako akaileta nilipo pulizia mkononi na kunusa sikusikia kitu chochote wala harufu yoyote ndiyo nikajua yenyewe mwanangu.

Niliamua kupiga simu usiku ule ule kwa rafiki yangu nashukuru alipokea na kumweleza hari harisi hili anipe uzoefu akanitajia dawa zote alizotumia mpaka akapona.

Dawa ya kwanza ni Aziwok au Azuma au Azikyua.
Dawa ya pili ni Asprin Junia
Dawa ya tatu Zinki
Dawa ya nne ni kujifukiza.

Wandugu nilianza dozi asubui maduka yalipo funguliwa na majani yakujifukisa yalikuwa tayari. Kesho yake mama akaanza kulalamika kuwa anaumwa siku ya 3 akaanza kuzidiwa tukaungana katika dozi, wakati mama anaingia katika dozi mkewangu akaanza kuvuta kamasi na vikoozi vya kupip naye akaanza kujisikia ovyo akaanza dozi. Baadaye shemeji na msichana nao wakaja na dalili hizo hozo.

Kuhusu nyungu nilicho jifunza ni kuwa mimi nilikuwa tayari hasa wakati wa usiku hata mchana ukitulia nasikia sauti au mkolomo wa mapafu tumboni hasa pafu la kushoto, hapa nashindwa kuelezea vizuri ila pafu ni kama linatetemeka au linavuma hivi. Nakumbuka baada tu kujifukiza tu niliona hewa nyepesii.

Nyungu kwa uzoefu wangu nilioupata haya ni majani ya miti au mimea ambayo inanukia au inatoa harufu nzuri au afrufu ya matunda yake. Majani haya ni pamoja na majani ya miembe, mpera, mzambarau, mstaferi, mchaichai, mlimao na mingine ila mimi nikawa nakatia katia na tangawizi na vitunguu swaumu pia.

Kuhusu chanjo mimi siziamini kwa maana moja tu kuwa waletaji wote wa chanjo wamesema chanjo akiingizwa mtu mwilini inaenda kumsaidia kinga za asili za mwili, sasa mimi Korona imenipiga tayari na kinga za mwili kusaidiana na dawa zimeishinda Korona sasa kunahaja gani mimi kuchanjwa.

Kwa upande wangu mimi kama mtoto wa mchugaji nimesikitishwa sana na kustshwa na wazazi wangu wa kiroho kama Askofu Kakobe, Askofu Gamanywa na wengine kwa kukataa nguvu za Mungu ambazo walitufundisha tangia wadogo kuwa ikishindikana kwa mwanadamu kwa Mungu inawezekana. Lakini leo wamebadilika wanaamini chanjo ya mwanadamu kwanza sielewi.

Vile vile nimesikitishwa na hawa viongozi wa dini kwa ujumla kwani wakati wa awamu ya 5 waliungana kufunga na kuomba lakini nimeshangaa awamu hii ya 6 wameacha kabisa kumtaja Mungu mbele badalayake chanjo ndiyo wameweka mbele kama tai. Kibaya zaidi mashehe na wachungaji wengine wamekaa kimya ambapo Yesu hawa aliwaita mafalisayo wanafiki.

Jamani Korona ipo ila unapona.
Mtoto wa mchungaji nimejaribu kushea uzoefu tu.
 
Pole Sana mkuu na hongera sana. Hapo kwenye pua kupoteza uwezo was kunusa mwenyewe mwezi ulopita nlipatwa na Hali hyo na ckuwa na mafuta Wala kikohozi msaada wangu ulikuwa ni kunywa mchanganyiko was tangawizi,asali na ki2nguu saumu ndipo nkawa fresh iia mwenyewe naamini ulikuwa covid. 2endlee kumwamini mungu. Amina.
 
Umesoma headings ya habari? Huo ni USIA wa Marehemu aliejinyonga.
 
Ok, huamini chanjo lakini unaziamini dawa za mzungu, yote kheri bora umepona.

Hapo kwenye kuitwa na ancestors mtoto wa mchungaji unaamini mizimu, zitafakari njia zako, hiyo sio dalili nzuri kama ungeondoka usingefikia kwenye mikono salama.
 
Katika variants za Delta na Lambda Asprin pamoja na nyungu haziwezi kufua dafu.Kimbilia chanjo haraka sana halafu utarudi hapa bila shuruti kunishukuru.

Mimi nilishawahi chanjo mapema sana na sasa hivi nafanya mpango wa kupata booster.Binadamu ambae haamini katika Sayansi ni binadamu mjinga sana na binadamu mfu.

Wakati gonjwa la ndui lilipoingia duniani lilitishia kuua binadamu wote duniani lakini chanjo iliokoa jahazi.Kama siyo chanjo gonjwa la ndui lilikuwa liue binadamu wote duniani.

Pona yako ni uamini katika sayansi kwa sababu hata kama utapona sasa hivi jua kuwa siku za mbele wanakuja variants nyingine wa Corona ambao itakuwa siyo rahisi kupona kwa kutumia Asprin.
 
Ujumbe ni mzuri, lakini kichwa cha habari kinanitatiza. Sielewi aliye andika haya ni reporter kuhusu kijana aliyepata uviko ama ni mgonjwa mwenyewe anaongea? Na je kama yeye na familia yake wote walipona , huko kujinyonga kumekujaje?
 
Hivi Kama mtu kaisha ugua corona na akapona, Kuna haja gani ya yeye kuchoma chanjo?!!!

Hili ndo nimeliona kwenye mada yako, mengine naomba unisamehe.
 
Katika variants za Delta na Lambda Asprin pamoja na nyungu haziwezi kufua dafu.Kimbilia chanjo haraka sana halafu utarudi hapa bila shuruti kunishukuru.

Mimi nilishawahi chanjo mapema sana na sasa hivi nafanya mpango wa kupata booster.Binadamu ambae haamini katika Sayansi ni binadamu mjinga sana na binadamu mfu.

Wakati gonjwa la ndui lilipoingia duniani lilitishia kuua binadamu wote duniani lakini chanjo iliokoa jahazi.Kama siyo chanjo gonjwa la ndui lilikuwa liue binadamu wote duniani.

Pona yako ni uamini katika sayansi kwa sababu hata kama utapona sasa hivi jua kuwa siku za mbele wanakuja variants nyingine wa Corona ambao itakuwa siyo rahisi kupona kwa kutumia Asprin.
Kwani Asprin ndio iliyopambana na virusi vya corona au ni kinga zake za mwili?
 
Ok, huamini chanjo lakini unaziamini dawa za mzungu, yote kheri bora umepona.

Hapo kwenye kuitwa na ancestors mtoto wa mchungaji unaamini mizimu, zitafakari njia zako, hiyo sio dalili nzuri kama ungeondoka usingefikia kwenye mikono salama.
Mi kwa sasa sina jibu la kukupa ila kumbuka kuwa babu zetu walikuwa wanasali na kumwomba Mungu kabla ya kuja kwa wazungu na ukristo na Biblia na matukio mengi makubwa yalifanyika ikiwemo kuishi maisha marefu miaka zaidi ya 150, waliomba mvua ikanyesha, nzige walikufa kwa maombi na si famigesheni.

Kuhusu kutokuamini chanjo nimesemakatika mada yangu, ila kiimani nilikuwa na mimi sielewi kwani huku nyuma walitufundisha kuwa Yesu anaweza na yanayoshindikana kwa mwanadamu Yesu hashindwi na jambo, sasa hata mimi sielewi viongozi wa dini wamegeuza na kuanzia katika chanjo au walikuwa wanatudanganya, au uwezo wa Yesu haupo au uliacha kufanya kazi sijui.
Nakumbuka watumishi wengi akiwemo Kakobe aliagiza walete vyeti vya magonjwa wa ukimwi waone uponyaji wa Yesu.
 
Yani kwanini umetumia hizo dawa kama asprin katika kujitibu na corona badala ya kumtegemea tu Mungu kama ambavyo unataka watu waache kutegemea chanjo na kumtegemea Mungu?
 
delta huwa inaanza iliposhia ya kwanza, so jitahidi kuwa makini usipate tena hutachomoa
 
Back
Top Bottom