Mkuu pole kwa majanga umenikumbusha mbali kidogo.
Mimi sikuwahi kupata corona Ila familia yangu yote ilipata corona ile ya pili. Mke, watoto 3, mama mkwe, Binti wa kazi yaan wote.
Mke wangu ni mtumishi pale Aghakan hospital, yeye ndiye aliye ambukiza familia maana ndiye alinza dalili kwa madai yake..
Wakati wanaugua mm nilikuwa safarin akanipigia cm na kuniambia familia mzima iko karantini. Mkuu bahat mbaya mm nilijua wenye corona wanakufa wote hivyo nilijua familia mzima nitazika.
Babaaa, ukisikia mtu kuomba Mungu jaman niliomba, nilitubu dhambi zote , nikarudi dar na kukuta nyumba nzma, nikukooa, kubanwa kifua, nilikuwa natembea nalia njian, mke wangu alinitaka nikalale guest nisije nyumban kabisa kwa lengo tusife wote. maana nyumba nzma Ina virus.
Kiufupi walipona wote. Nilijifunza Sana kwamba Mungu anajibu maombi watu wakiomba. Pole mkuu. Corona ipo tuchukue taadhar Wana JF