Mimi hoja yangu siyo wewe kujua kuwa Asprin imemponyesha au la.
Hoja yangu ni kwamba hupaswi kufikia muafaka kuwa amepona kutokana na dawa alizotumia kama ulivyodai hapa kwa sababu hakuna controlled experiment ambayo umefanya ukajua ni dawa alizotumia ndizo zimemponyesha na wala siyo vigezo vingine vyovyote vile.
Halafu suala kwamba kwa sababu mimi nimedai kuwa Asprin inaponyesha basi atakuwa amepona kutokana na kutumia Asprin siyo sahihi kwa sababu mimi siyo mamlaka za dawa zinazoaminika.Kwani mimi ni WHO hadi nilichoongea kiwe kipo sahihi?Kwani mimi ni FDA?Kwani mimi ni NIMRI?
Halafu sikusema kuwa Asprin ni dawa ya kutibu Corona bali nimesema kuwa ina uwezo mdogo sana kustimulate kinga ya mwili dhidi ya Corona na ndiyo maana hata mamlaka za dawa za kuaminika kama vile FDA walikataa dawa kama hiyo.
Sasa dawa ambayo haina kibali chochote kile cha kutibu Corona kutoka mamlaka ya kuaminika yoyote ile ya madawa nije kuipitisha mimi?Mimi ni nani hadi niipitishe dawa hiyo kuwa inatibu Corona?Unanisikiliza mimi au unasikiliza mamlaka za madawa za kuaminika?