Leo nimefurahi sana kumsikia Tundu Lissu akisema yale ambayo nimekuwa nikiyasema kwa miaka mingi!

I just call balls and strikes. Never blinded by fanaticism.

Hakuna aliye juu ya kukosolewa na hakuna aliye chini ya kupongezwa.

Ukitenda sawa, ukifanya vyema, nitakupongeza.

Ukiharibu, nitakuchana tu. Sitokufumbia macho wala kukuzibia masikio.

Alichokiongea Tundu Lissu leo ndicho nimekuwa nikikihubiri miaka nenda rudi, hapa JF na kwingineko.

Na hicho ni hakuna kushiriki chaguzi za maigizo mpaka pawepo na mabadiliko ya kweli ya namna ambavyo chaguzi zetu zinavyoendeshwa.

View: https://youtu.be/ZxRytUvLb6A?si=3KluAQKBpWx0ccSd

Nimeandika mara nyingi sana kuhusu hili jambo, tokea 2006 [ na kabla ya hapo kwingineko kwenye mitandao ya mijadala].

2020 baada ya uchaguzi mkuu, nilianzisha hii mada;

Mapema mwaka jana, 2024, nilileta hii mada hapa pia;

Hizi mada mbili zina-dovetail vizuri sana na maudhui ya kile alichokiongea Lissu leo.

Nimefurahi sana kumsikia Lissu akiongea jinsi alivyokuwa akiongea. Ni mwanzo mzuri sana.

Sasa kilichobaki ni kupanga mikakati na kufanya utekelezaji wake mpaka yapatikane matokeo tunayoyatamani na kuyataka.

Way to go Mr. Lissu. You got my full support on this one!

Chaguzi za maigizo za kuchoma pesa za wananchi huku unaiwaibia process ya uchaguzi sasa mwisho!
 
2025 kuna jambo ni suala la muda tu.
 
I just call balls and strikes. Never blinded by fanaticism.

Hakuna aliye juu ya kukosolewa na hakuna aliye chini ya kupongezwa.

Ukitenda sawa, ukifanya vyema, nitakupongeza.

Ukiharibu, nitakuchana tu. Sitokufumbia macho wala kukuzibia masikio.

Alichokiongea Tundu Lissu leo ndicho nimekuwa nikikihubiri miaka nenda rudi, hapa JF na kwingineko.

Na hicho ni hakuna kushiriki chaguzi za maigizo mpaka pawepo na mabadiliko ya kweli ya namna ambavyo chaguzi zetu zinavyoendeshwa.

View: https://youtu.be/ZxRytUvLb6A?si=3KluAQKBpWx0ccSd

Nimeandika mara nyingi sana kuhusu hili jambo, tokea 2006 [ na kabla ya hapo kwingineko kwenye mitandao ya mijadala].

2020 baada ya uchaguzi mkuu, nilianzisha hii mada;

Mapema mwaka jana, 2024, nilileta hii mada hapa pia;

Hizi mada mbili zina-dovetail vizuri sana na maudhui ya kile alichokiongea Lissu leo.

Nimefurahi sana kumsikia Lissu akiongea jinsi alivyokuwa akiongea. Ni mwanzo mzuri sana.

Sasa kilichobaki ni kupanga mikakati na kufanya utekelezaji wake mpaka yapatikane matokeo tunayoyatamani na kuyataka.

Way to go Mr. Lissu. You got my full support on this one!

Dah bonge la hotuba.

Huwa napenda kusikiliza madini kutoka kwenye brains za namna hii, si akina Bibi Titi wachambaji
 
Kwa mtazamo wangu, Mbowe hakuwa consistent.

Kuna nyakati alikuwa anayumba. Leo anasema hakuna uchaguzi bila mabadiliko, baadaye anasikika akisema CHADEMA ijiandae na uchaguzi mkuu.
Always keep your powder dry. And also keep your adversary guessing. Ndicho alichokuwa anakifanya.

Amandla...
 
Hivi kuna nchi ambayo ilileta mabadiliko kwa kuzuia chaguzi kufanyika? Tatizo kubwa sio kuwa taratibu ni mbaya. Tatizo kubwa ni kuwa hata hizo taratibu mbaya zilizokuwepo hazifuatwi. Mfano hai ni wa wakina Halima. Pamoja na kuwa Katiba kusema kuwa mbunge ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa, wakina Halima wanamaliza miaka yao mitano pamojq na kuwa waliishafukuzwa kutoka kwenye Chama chao na chama hicho kusema hakiwatambui. Hii ni pamoja na precedent za Spika kuwanyang'anya ubunge wale waliotumuliwa na vyama vingine. Tamko la kuwafukuza lilipotoka, nafasi zao zikatangazwa kuwa wazi. Kwa mantik hii sitashangaa kuona wagombea wa Chadema wakipitishwa kugombea bila ridhaa ya Chama chao. Hapo bado vyama vingine ambavyo vitaona kuwa ni fursa ya kuchukua nafasi ya CDM.

Na kutegemea mataifa ya nje kuweka presha ni kujidanganya hasa katika enzi hizi za Trump na nchi za Ulaya kuongozwa na far right parties. Hawa watu hawana mpango na Tanzania na watakuwa comfortable kutambua utawala wowote utakaokuja.
Njia inayoweza kufanikiwa ni ya mass mobilization. Mimi ningewashauri wasahau uchaguzi wa 2025 walenge zile za 2029 na 2030. Hakuna Rais ambae atakubali kuwa wa kwanza wa mukula mmoja. Hakuna.

Kwa sasa waweke nguvu katika kuhamasisha watu na ku identify wagombea. wanaokubalika na wenye moyo wa kupambania haki zao. Watu kama Aisha wa Dodoma, yule dada wa Chato, mbunge wa Nkasi, yule dada wa Njombe, Susan Kiwanga, Catherine Ruge n.k.

Wa identify maeneo ambayo wana uhakika wa ushindi na wawekeze katika kuhakikisha kuwa hujuma hazifanyiki katika maeneo hayo. Hao wabunge wachache watakaopatikana watawapa nafasi ya kupiga kelele bungeni na kura watakazopata zitawapa ruzuku ambayo wataitumia kujitayarisha kwa ajili ya 2029 na 2030.

Hakuna nchi iliyopata mabadiliko bila Jasho la damu. Njia waliyochagua CHADEMA ni sahihi sana tena ilipaswa kuchukuliwa takribani miaka 20 iliyopita.

Nchi hii bila kuwaonesha CCM kuwa wananchi sio wajinga kila siku tutakuwa kama mazuzu.
 
Huo ubabe wa kishamba chawa acheni kuwavimbisha kichwa ccm ili mnufaike, Dunia imebadilika mkileta ubabe misaada yote toka nje itafutwa na pia vikwazo vya uchumi vitakuja
Ahahahahaha! Eti misaada toka nje! Ahahahahaha!!!
 
Hapo changamoto itakua kushawishi vyama vingine vigomee pia ndio itakua na IMPACT kubwa..... yaani Fisiemu waende kwenye uchaguzi peke yao

Lakini ikigomea CDM pekee CCM inaweza kuwapa ACT na vyama vingine ubunge wa viti kadhaa na madiwani ikaleta picha ya CDM wamegomea kwa hofu yao tu na kiburi

Hapa ndo pana kazi ngumu sana, maana vyama mamluki ni vingi sana.
 
45X45=2025 ❣️
1739381589024.png

X*X = XX (NOT XY) --- LADY'S YEAR!
 
Hakuna nchi iliyopata mabadiliko bila Jasho la damu. Njia waliyochagua CHADEMA ni sahihi sana tena ilipaswa kuchukuliwa takribani miaka 20 iliyopita.

Nchi hii bila kuwaonesha CCM kuwa wananchi sio wajinga kila siku tutakuwa kama mazuzu.
Swali lilikuwa kama kuna nchi ilipata mabadiliko kwq kugomea uchaguzi. Hamna mahali Lissu amesema kuwa jasho la damu litatumika kuleta mabadiliko. Alichosema ni kuwa wanatumia njia hii kuepuka hilo jasho la damu.

Amandla...
 
Hapo changamoto itakua kushawishi vyama vingine vigomee pia ndio itakua na IMPACT kubwa..... yaani Fisiemu waende kwenye uchaguzi peke yao

Lakini ikigomea CDM pekee CCM inaweza kuwapa ACT na vyama vingine ubunge wa viti kadhaa na madiwani ikaleta picha ya CDM wamegomea kwa hofu yao tu na kiburi
Muhimu hapo ni kusifanyike uchaguzi.
 
Wa identify maeneo ambayo wana uhakika wa ushindi na wawekeze katika kuhakikisha kuwa hujuma hazifanyiki katika maeneo hayo. Hao wabunge wachache watakaopatikana watawapa nafasi ya kupiga kelele bungeni na kura watakazopata zitawapa ruzuku ambayo wataitumia kujitayarisha kwa ajili ya 2029 na 2030.

Amandla...
Mkuu hiki unachopendekeza ndio kinafanyika toka uchaguzi wa vyama vingi uanze upya na matokeo yanazidi kuwa mabaya zaidi kila chaguzi

Nilishiriki kikamilifu kwenye harakati za uchaguzi mkuu 2020 na ilifanyika MIKAKATI THABITI kabisa lakini Upinzani uliishia “kupewa” mbunge mmoja tu.
Nikiri tu kwamba hakuna namna yoyote unaweza kupata hata 10% ya uchaguzi huru na haki Fisiemu wakiamua kufanya yao chini ya Katiba hii na tume hii na sheria hizi za uchaguzi

Kuna namna nyingi ya kufanya shinikizo ikiwemo kugomea chaguzi..... halafu baada ya hapo hatua zingine zitafuatia
 
Hapajawahi kuwa na usimamizi wa dhati wa kuhakikisha haki inatendeka. Mara nyingi ni viongozi wachache ndio wanaachiwa kupambana wenyewe. Wananchi wanabaki kulalamika.
Hilo la kugomea uchaguzi halitafanikiwa maana bado watu wengi tu watapiga kura ( wafanyakazi wa serikali, vyombo vya dola, wapenzi wa chama tawala n.k.). Aidha ACT-WAZALENDO itakataa kugomea kwa sababu wana hakika ya kupata wabunge kutoka Pemba na Unguja. Mgomo utashindwa kabla ya kuanza.

Amandla....
 
Mkuu usimamizi wa dhati ndio upi labda?

Hivi kiuhalisia mpinzani akipata kura 50,000 na CCM akipata kura 10,000 halafu msimamizi akitangaza CCM imepata 50,000 na CDM 10,000 na mawakala wa CDM wakagoma kusaini fomu itabadilisha nini?

Masanduku ya kura wanatunza wao mahakama za kwao hata ukienda huko hamna kitu

Mkuu hizi suggestions zenu ni kwasababu hampo field kujionea umafya unaofanywa na ccm

Hapo sijazingumzia wagombea kenguliwa, kununuliwa, kutekwa, kuporwa fomu, fomu kuongezwa makosa na tume nk nk

Just imagine Mtu wa upinzani kakaa jela miezi 6 kafutiwa kesi na kuachiwa huru bila hakimu usiku wa saa 2 Singida na kesho yake Asubuhi yupo Bungeni anaapishwa ubunge wa Viti maalumu wa upinzani 😳
Yaani wapinzani wenyewe wanajishangaa😂
 
Back
Top Bottom