Leo nimejaribu kusoma Biblia japo kidogo tu ila nahisi kuchanganyikiwa

Leo nimejaribu kusoma Biblia japo kidogo tu ila nahisi kuchanganyikiwa

Ni kitabu cha mazezeta ambayo maoga ya maisha yanatia huruma machoni mwa Mungu ambae anaonekana ni katili kwa watu wake
 
🤣🤣 hiki ni kichaka cha kukwepa mkanganyiko uliopo na kujichanganya kwenye mambo mengi.
sio kichaka, ushawah kujiuliza kwanini Bibilia ni kitabu kigumu kusoma? shida ni nini?
 
Ni kitabu cha mazezeta ambayo maoga ya maisha yanatia huruma machoni mwa Mungu ambae anaonekana ni katili kwa watu wake
Hizi ni kashfa sasa, kwani ukisoma Bibilia unapata hela? hata hicho kitabu inachofikiria kuwa ni cha matajiri utasoma ujifungie ndani? kutafuta maisha ni hitaji la msingi la mwanadamu lakini maarifa ni hitaji muhimu zaidi haijalishi ni ya kiroho au kimwili
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Anza mwanzo na kama hutaelewa Rudia pale pale ukianzia katikati utachabganyikiwa zaid
 
Usio

Usiogope,soma tu utaelewa,usikubali kushikiwa masikio,soma kwa unyenyekevu,tafakari peke yako utaona Nuru
Biblia ni labyrinthine kinoma sio kwamba in contradiction,haina contradiction hata kidogo.
Katika Biblia Kuna Mungu aliyekuwa kwa MUNGU.
Yh 1:14

kwenye Waebrania Kuna Mungu anatiwa Mafuta na Mungu wake.
yaan Kuna Mungu ila Huyo Mungu ana Mungu wake..sasa Kuna wakati watu wanawachanganya hawa wawili.

ukienda kichwa kichwa kwenye bibilia na ukikutana na Sheikh mtaani ni lazima Uslimishwe faster.
na ukisha-slim tu mungu anakutumia ujumbe wa ..
Hosea 4:6

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Unakurupuka tuu unafungua huko mbali? Ebu anza mwanzo ukifika huko utakuwa umeelewa.
 
Pole...Kuna utaratibu mzuri wa kuisoma biblia na kuielewa. Je naomba kujua kama hii ndio mara yako ya kwanza kuisoma biblia seriously?

Kwamfano, kuna namna ya jinsi gani uanze kusoma Agano la kale na ufuate mtiririko upi?
Pia jinsi gani usome agano jipya na ufuate utaratibu upi!.
Kwa sasa nikama hakuna mkristo anaye ielewa biblia...injili yote na maandiko yamepotoshwa makanisani ...ni mimi peke yangu ndiyo naielewa kwa sababu ya akili niliyo jaliwa
 
ugumu ndio uko hapo sasa umeshindwa kutranslate na kuapply katika maisha ya kawaida
Hakuna kitu kigumu zaidi ya hadithi ambazo hata kabla yakuletwa Africa watu walikua wanaishi tu
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14...

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliye elewa naomba Ufafanuzi wa kina..
Mimi nakumbuka nilivyookoka tu nilikuwa na nguvu sana (upako) wa kusoma Biblia tangu kitabu cha Mwanzo mpaka ufunuo na kukimaliza ndani ya miezi kadhaa! Kwa mwaka Biblia nilikuwa naisoma yote mara mbili. Hiyo ni miaka zaidi ya 20 iliyopita! Sasa baada ya changamoto nyingi za maisha na kutafuta msaada wa upenyo kwa kumtegemea Mungu nilianza kuiona Biblia kitofauti. Hayo maneno ya Biblia sio maneno ya kawaida! Kiasi kwamba "ukisoma mstari mmoja tu na ukapata ufunuo" huwezi kumaliza sura nzima kwa wiki moja kama unataka mafunuo kwa kila mstari! Yaani kila mstari unamafunuo yaliyoambata na Roho ya nguvu za hilo neno "hatari kabisa! wee acha tu". Ndo maana usipokuwa na hekima na ulinzi kifikra na kiakiri unaweza kuchanganyikiwa na kuishia kuanzisha dini "dhehebu" lako.

Sasa basi, mleta mada hiyo sura ya "waebrania 1:1-14", inataka kumtofautisha Yesu na viumbe wengine wote kimamlaka. Maana kabla ya kuumba wanadamu aliumba malaika. Malaika ni viumbe vya kiroho wana nguvu, utashi, akili karibia na Mungu (kwa ummoja wao na sio mmoja mmoja). Isipokuwa, Mungu alivyoamua kuumba mwanadamu kwa sura ya kimwili kama Mungu hasiyekuwa na mwili ikabidi ajifunue katika nafsi tatu: Baba, mwana, roho mtakatifu. Sasa nafsi ya mwana kimwonekano akawa anafanana na malaika hivyo pakawepo hali ya dharau kwa malaika kutaka kujilinganisha na Yesu. Sasa hii sura ya "Ebrania 1:1-14" ni mafunuo yetu wanadamu kutaka tujue tofauti ya Yesu na malaika. Life Management
 
Biblia hii ya kiswahili imeandikwa kitapeli sana...

Mfano ukisoma bible ya kiswahili na ukisoma Ile ya kingereza utashangaa maana tofauti kabisa
 
Biblia hii ya kiswahili imeandikwa kitapeli sana...

Mfano ukisoma bible ya kiswahili na ukisoma Ile ya kingereza utashangaa maana tofauti kabisa
Kwa wageni wa Biblia inabidi muwe waangalifu sana! Mitaani kuna Biblia feki kama zoote! Kutokana na technologia ya simu kuna Biblia za kudownload app kwenye simu. Sasa sikia! Biblia ni hile hile haitakiwi kuongeza au kupunguza "ufunuo 22:18-19". Sasa sikia, ukidownload Biblia kwenye mtandao utaletewa ujumbe wa kutaka "update to new version au new releases", sasa ebu jaribu kukubali hiyo new release version, utakuja kuona maneno yamebadilishwa maana, mengine yameondolewa, mengine yameongezwa, nafsi ya Mungu ambayo ni ya kiume (God the father) imebadilishwa! Lakini sisi wazoefu huwa tunapenda kusoma Biblia za kwenye kitabu "Hardcopy" na tunajua hipi kweli na hipi ya uongo. Nyakati za mwisho ambazo ndo tulipo sasa Biblia halisi itapotea kabisa! Hiki kitabu kitakuja kutoweka kabisa na kama tutaendelea kuwepo duniani kabla Yesu kuja (maana wengi wetu hata mimi sitaki (Hatutaki) Yesu arudi mapema, wale wazembe wasiotaka kupambana kimalaka na shetani, wale walegevu wanaomba mwisho wa dunia utokee sasa, 😂😂😂). Yesu sio dhahifu, hawezi kumkimbia shetani kirahisi, kimamlaka anatumia wanadamu waliomtii na kutumia nguvu ya neno la Mungu na kumdunda shetani mpaka anaomba 'pooo', chezea wee! Ni kwa vile nyie hamjuhi nguvu za neno la Mungu hili hili lililoko kwenye Biblia Wakipekee
 
Mimi nakumbuka nilivyookoka tu nilikuwa na nguvu sana (upako) wa kusoma Biblia tangu kitabu cha Mwanzo mpaka ufunuo na kukimaliza ndani ya miezi kadhaa! Kwa mwaka Biblia nilikuwa naisoma yote mara mbili. Hiyo ni miaka zaidi ya 20 iliyopita! Sasa baada ya changamoto nyingi za maisha na kutafuta msaada wa upenyo kwa kumtegemea Mungu nilianza kuiona Biblia kitofauti. Hayo maneno ya Biblia sio maneno ya kawaida! Kiasi kwamba "ukisoma mstari mmoja tu na ukapata ufunuo" huwezi kumaliza sura nzima kwa wiki moja kama unataka mafunuo kwa kila mstari! Yaani kila mstari unamafunuo yaliyoambata na Roho ya nguvu za hilo neno "hatari kabisa! wee acha tu". Ndo maana usipokuwa na hekima na ulinzi kifikra na kiakiri unaweza kuchanganyikiwa na kuishia kuanzisha dini "dhehebu" lako.

Sasa basi, mleta mada hiyo sura ya "waebrania 1:1-14", inataka kumtofautisha Yesu na viumbe wengine wote kimamlaka. Maana kabla ya kuumba wanadamu aliumba malaika. Malaika ni viumbe vya kiroho wana nguvu, utashi, akili karibia na Mungu (kwa ummoja wao na sio mmoja mmoja). Isipokuwa, Mungu alivyoamua kuumba mwanadamu kwa sura ya kimwili kama Mungu hasiyekuwa na mwili ikabidi ajifunue katika nafsi tatu: Baba, mwana, roho mtakatifu. Sasa nafsi ya mwana kimwonekano akawa anafanana na malaika hivyo pakawepo hali ya dharau kwa malaika kutaka kujilinganisha na Yesu. Sasa hii sura ya "Ebrania 1:1-14" ni mafunuo yetu wanadamu kutaka tujue tofauti ya Yesu na malaika. Life Management
Aisee
 
Ili ukielewe hicho kitabu inabidi na wewe usiwe na akili hata hao waumini wenyewe huwa hawakisomi hadi jumapil padri awaambie fungua mathayo 5:8
Una hoja kubwa sana boss inabidi usikilizwe kwakweli wallah
 
sio kweli, kama haujakisoma usijumuishe wote, wapo tuliosoma na tunaenjoy kusoma maana tunapata maarifa
Ungekua unakisoma usingekula nguruwe maana imekatazwa
 
Back
Top Bottom