Leo nimejaribu kusoma Biblia japo kidogo tu ila nahisi kuchanganyikiwa

Leo nimejaribu kusoma Biblia japo kidogo tu ila nahisi kuchanganyikiwa

Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Nini kimekufanya uanzie kitabu cha waebrania? Yaani ni sawa na mtu ambaye hujui hata ‘what is physics’ then ushike kitabu cha Abbot kwa mara ya kwanza ufunue ukurasa wa 45 uanzie hapo, kweli?!
 
Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Na aliyeelewa huu mstari atuambie!

Isaya 34:6​

"Upanga wa BWANA umeshiba damu, umejazwa mafuta, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo dume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu".

Nb 1): Agano la kale lilijikita zaidi kwa wayahudi, humo walipewa misingi yote ya utamaduni wao huku dini ya kiyahudi ikiwa kama dini kuu.(Stori nyingi ni za maeneo ya mashariki ya kati)

Nb 2): Agano jipya lilijikita zaidi katika kueneza utamaduni wa watu wa magharibi na ukristo ikiwa ndiyo kama dini yao, hapa dola ya kirumi ikishika hatamu zote.(Stori nyingi ni za maeneo ya Ulaya)

Ni mtazamo tu.
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Mimi nimeisoma mara 3 mwanzo mwisho, sijachanganyikiwa. Ni ama hujaisoma kabisa au ulisoma kutafuta makosa.
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Mistari hii inasisitiza ukuu wa Yesu Kristo juu ya malaika, akionekana kama Mwana wa Mungu na Mkombozi, aliye na mamlaka yote na anayeketi kwenye mkono wa kuume wa Mungu. Inatukumbusha kuwa Yesu ndiye Mungu na mpatanishi mkuu wa wokovu wetu.
 
Mimi nakumbuka nilivyookoka tu nilikuwa na nguvu sana (upako) wa kusoma Biblia tangu kitabu cha Mwanzo mpaka ufunuo na kukimaliza ndani ya miezi kadhaa! Kwa mwaka Biblia nilikuwa naisoma yote mara mbili. Hiyo ni miaka zaidi ya 20 iliyopita! Sasa baada ya changamoto nyingi za maisha na kutafuta msaada wa upenyo kwa kumtegemea Mungu nilianza kuiona Biblia kitofauti. Hayo maneno ya Biblia sio maneno ya kawaida! Kiasi kwamba "ukisoma mstari mmoja tu na ukapata ufunuo" huwezi kumaliza sura nzima kwa wiki moja kama unataka mafunuo kwa kila mstari! Yaani kila mstari unamafunuo yaliyoambata na Roho ya nguvu za hilo neno "hatari kabisa! wee acha tu". Ndo maana usipokuwa na hekima na ulinzi kifikra na kiakiri unaweza kuchanganyikiwa na kuishia kuanzisha dini "dhehebu" lako.

Sasa basi, mleta mada hiyo sura ya "waebrania 1:1-14", inataka kumtofautisha Yesu na viumbe wengine wote kimamlaka. Maana kabla ya kuumba wanadamu aliumba malaika. Malaika ni viumbe vya kiroho wana nguvu, utashi, akili karibia na Mungu (kwa ummoja wao na sio mmoja mmoja). Isipokuwa, Mungu alivyoamua kuumba mwanadamu kwa sura ya kimwili kama Mungu hasiyekuwa na mwili ikabidi ajifunue katika nafsi tatu: Baba, mwana, roho mtakatifu. Sasa nafsi ya mwana kimwonekano akawa anafanana na malaika hivyo pakawepo hali ya dharau kwa malaika kutaka kujilinganisha na Yesu. Sasa hii sura ya "Ebrania 1:1-14" ni mafunuo yetu wanadamu kutaka tujue tofauti ya Yesu na malaika. Life Management
Mistari mirefu huna lolote fix tU.
 
Mistari hii inasisitiza ukuu wa Yesu Kristo juu ya malaika, akionekana kama Mwana wa Mungu na Mkombozi, aliye na mamlaka yote na anayeketi kwenye mkono wa kuume wa Mungu. Inatukumbusha kuwa Yesu ndiye Mungu na mpatanishi mkuu wa wokovu wetu.
Yaani wewe maelezo yako yenyewe yamejichanganya ndo Bible iko hivyo ili uelewe inabidi ujitoe Akili.
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Nenda mlimani au mahali pafaragha funga siku tatu kwa ajili ya hilo mwambie Mungu maana Bibilia ni mambo ya rohoni utapata majibu yako
 
Biblia siyo kama gazeti,inahitaji uwe na ROHO MTAKATIFU akuongoze kuyatafakari na kuyaelewa usomayo
UBARIKIWE NA BWANA
 
sio kichaka, ushawah kujiuliza kwanini Bibilia ni kitabu kigumu kusoma? shida ni nini?
Bibia sio hekaya na haditdhi za Abwunwasi,

1730118335723.png
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Biblia si kitabu cha kuelewa, ni kitabu cha kuamini.

Ukitaka kuelewa utaona hizi zote hadithi za kutungwa na watu tu, utakitupa chini.
 
Kuna nguvu ya roho wachafu walioko ndani yako wanakuzuia kutolielewa neno la Mungu. Unahitaji usaidizi kwenye hili.
 
Nimeanza na kitabu cha waebrania sura ya Kwanza mstari wa kwanza hadi wa 14.

Kusema kweli sijaelewa Jinsi Mungu na Mwanae walivyojipambanua.

Aliyeelewa naomba Ufafanuzi wa kina.
Ungeanza na kitabu Cha mwanzo
Mbona unarukaruka🤒
 
Kwa sasa nikama hakuna mkristo anaye ielewa biblia...injili yote na maandiko yamepotoshwa makanisani ...ni mimi peke yangu ndiyo naielewa kwa sababu ya akili niliyo jaliwa
Sawa mkuu, nafikiri nimekuelewa ulichosema na ninakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa. Injili ya sasa imeghoshiwa mnoooo no wonder watu hawaoni thaman yake no more na ndio maana wengi wanaipinga
 
Ni Mungu huyo huyo, Agano la kale alijipambanua namna nyingine na katika Agano jipya kajimbanua vingine,

Katika Agano jipya Yesu amefanyika sadaka ili kutengeneza mahusiano yetu na Mungu, ukisoma Ebrania sura ya tisa utaona Yesu amekuwa mpatanishi au kiunganishi au mrejeshaji wa mahusiano baina yetu(wanadamu) na Mungu.

Katika Agano la kale hutamuona Yesu akitajwa na Mungu alijifunua kupitia mtu mmoja mmoja, mfano ni Ibrahim, Yakobo, Isaka, Musa na wengine ambao Mungu alijifunua kwao
"Amefanyika sadaka" au laana?

Au mmesahau biblia inaposema "... kila atundikwae kwenye mti?

Kondoo semeni kweli, msidanganyane kikondoo hapa, tupo tunaoijuwa biblia.
 
"Amefanyika sadaka" au laana?

Au mmesahau biblia inaposema "... kila atundikwae kwenye mti?

Kondoo semeni kweli, msidanganyane kikondoo hapa, tupo tunaoijuwa biblia.
ungeijua ungemfafanulia mtoa mada, mtoa mada anahitaji ufafanuzi wa Ebrania 1:1-14, mpe ufafanuzi wewe unayeijua
 
Back
Top Bottom