Mimi nakumbuka nilivyookoka tu nilikuwa na nguvu sana (upako) wa kusoma Biblia tangu kitabu cha Mwanzo mpaka ufunuo na kukimaliza ndani ya miezi kadhaa! Kwa mwaka Biblia nilikuwa naisoma yote mara mbili. Hiyo ni miaka zaidi ya 20 iliyopita! Sasa baada ya changamoto nyingi za maisha na kutafuta msaada wa upenyo kwa kumtegemea Mungu nilianza kuiona Biblia kitofauti. Hayo maneno ya Biblia sio maneno ya kawaida! Kiasi kwamba "ukisoma mstari mmoja tu na ukapata ufunuo" huwezi kumaliza sura nzima kwa wiki moja kama unataka mafunuo kwa kila mstari! Yaani kila mstari unamafunuo yaliyoambata na Roho ya nguvu za hilo neno "hatari kabisa! wee acha tu". Ndo maana usipokuwa na hekima na ulinzi kifikra na kiakiri unaweza kuchanganyikiwa na kuishia kuanzisha dini "dhehebu" lako.
Sasa basi, mleta mada hiyo sura ya "waebrania 1:1-14", inataka kumtofautisha Yesu na viumbe wengine wote kimamlaka. Maana kabla ya kuumba wanadamu aliumba malaika. Malaika ni viumbe vya kiroho wana nguvu, utashi, akili karibia na Mungu (kwa ummoja wao na sio mmoja mmoja). Isipokuwa, Mungu alivyoamua kuumba mwanadamu kwa sura ya kimwili kama Mungu hasiyekuwa na mwili ikabidi ajifunue katika nafsi tatu: Baba, mwana, roho mtakatifu. Sasa nafsi ya mwana kimwonekano akawa anafanana na malaika hivyo pakawepo hali ya dharau kwa malaika kutaka kujilinganisha na Yesu. Sasa hii sura ya "Ebrania 1:1-14" ni mafunuo yetu wanadamu kutaka tujue tofauti ya Yesu na malaika.
Life Management