Leo nimejisikia vibaya sana wakuu!

Leo nimejisikia vibaya sana wakuu!

Huyu nimejiridhisha mkuu na dawa amendikiwa ila hakuwa na hela,mimi nimewahi kuwa tapeli na Jambazi,hivyo naelewa mtu akiwa tapeli,huyu mama alikuwa na uhitaji maana karibia pesa yote aliyokuwa nayo imeishia kwenye matibabu ya mwanaye!,Halafu mwanaye ni alichubuka usawa wa jicho hivyo alikuwa na Jeraha!

Kuna muda alitaka nisipompa hela nimsaidie kumnunulia mwanaye dawa alizoandikiwa,Aiseee kuna matapeli lakini yule Sister anapitia magumu mno!.


Yaani sielewi hata kesho na kuendelea atakula nini,kibaya zaidi sikuchukua namba yake!

Pesa niliyokuwa nimepanga nifanyie mambo yangu nimeona nimpatie yeye,kwani hata hivyo mkuu huwa tunapoteza kiasi gani kwenye mambo ya ajabu?,Huwezi amini baada ya kumsaidia nina amani kuliko kawaida!
Pesa umepigwa io pole yako.
 
Huwezi kuweka hitimisho kwa kupewa story ya upande mmoja.

Wanawake wakiamua kuharibu/kumtibua mwanaume hutokwa maneno magumu wana vinywa vichafu hatari haifai kuhadithia.

Pia hao hao ni good pretender pale mambo yanapowafika shingoni! Hivyo huwezi jua kilichotokea siku anatemana na huyo mzazi mwenzie.
Pengine alitoa kauli za kishupavu kiasi cha kumchefua kamanda.

Trust me, hakuna mwanaume anaependa kutelekeza mwanae. Ila ukichafukwa ghadhabu yetu ni mbaya sana unafuta kila kitu.

Mkuu usiombe yakutokee. Wanawake wanatia maudhi na mwanaume jasiri anaamua liwalo na liwe potelea pote nakata mawasiliano period.
Umenena vyema kabisa na huu ndio ukweli wenyewe.
 
Sisemi vibaya ila Wanawake sio watu wa kawaida kbs, umesikia upande mmoja ila ungesikia upande wa pili huenda ungetoa laki umpe huyo mwanaume. Hawa viumbe Mungu ndio anajua alipowakosea ktk uumbaji wake ndio maana alisema tuishi nao kwa akili Mungu sio fara.
Na kwa vile walikuwa hawaishi wote kama wanandoa waweza kuta huyo mtoto ana kadi 2 au 3 za kriniki na mwanaume akagundua hilo.
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Siku ya leo kwangu imekuwa siku mbaya sana kwasababu mimi huwa nina huruma sana na huwa naguswa na matatizo ya watu wengine wanayopitia!.

Leo nilikuwa nimeenda Hospitali moja pale Sinza,nilimpelekea Dada mmoja hivyo ikabidi nipaki nje kumsubiri!, Sasa wakati nikiwa pale nje kuna dada mmoja alitoka ndani ya hospitali mwanaye akiwa analia kweli!

Alipofika kwangu akawa ameniomba nimsaidie nauli ya kumfikisha kwake,ikabidi nimuulize maswali kadhaa,baada ya kujiridhisha kutokana na majibu yake kiukweli niliumia sana!.

Yeye " Kaka mambo"

Mimi " Poa,Kwema"

Yeye "Samahani kaka,naomba unisaidie!"

Mimi " Nikusaidie nini Sister?"

Yeye " Kaka pesa yote niliyokuwa nayo nimefanya vipimo vya mwanangu na nyingine nimechukulia dawa!"

Aliendelea " Naomba tu unisaidie nauli ya kunifikisha nyumbani kaka"

Mimi "Pole sana,Unaishi wapi?"

Yeye " Nakaa Banana"

Mimi "Umemtaarifu Mumeo kwamba umeishiwa nauli?"

Yeye "Wee acha tu kaka,ni kama huyu mtoto hana Baba"

Mimi "Kwanini?,Baba yake yuko wapi?:

Yeye " Baba yake alimkataa mwanaye!"

Mimi "Usione kama nakuuliza maswali dada,nisamehe kama nitakuudhi lakini nataka kujiridhisha maana matapeli huu mji ni wengi mno!"

Yeye "Mimi si tapeli kaka naomba unisaidie tu nauli"

Mimi "Hapana sister,sijasema wewe ni tapeli,nilikuwa nakuelewesha tu!:

Yeye "Basi ngoja nkutolee kadi la kriniki uone"

Kweli,alinitolea kadi la kriniki pamoja na dawa ambazo aliandikiwa akanunue kwa ajili ya mwanaye!

Sikutaka kumchimba sana maana pengine niliona isingekuwa vema kumpeleleza,mimi niliamua tu kujiongeza!

Sasa ni kwamba, kwa maelezo yake ni kuwa jamaa aliyempa mimba alimkimbia akiwa mjamzito na jamaa anafanya kazi Tanesco Mkoa wa Kitanseco wa Ilala!.

Kiukweli mwanamke ni mzuri na amezaa mtoto wa kike mzuri sana kama mama yake!. Nilijaribu kumuuliza sababu za yeye kuachana na huyo mshikaji akadai ni wivu wa kimapenzi!.

Leo nimenikuta natoa Tsh 50,000/= namsaidia yule dada, Kiukweli sijawahi kutoa kiasi hicho cha pesa kusaidia kutokana na nature ya kazi yangu (Hayo mambo niliyafanya zamani nilipokuwa Don kabla sijarudi kuanza moja).

Kiukweli baada ya kumpa hiyo hela huyo Dada nimejihisi amani sana na nimekuwa na furaha ya moyo ingawa nimehuzunika sana!

USHAURI:

Wanaume wenzangu, hata kama utakuwa umekosana na mwanamke ambaye amekubebea mimba yako kiasi gani, tafadhali usimtelekeze,kiukweli huwa wanapitia mateso makubwa mnooo!, nawaomba sana msije mkafanya hivyo!.

Hata kama huyo mwanamke awe ameekuudhi kiasi gani, tafadhali jifanye mjinga tu ili umnusuru mtoto kwasababu dogo anakuwa hana tatizo, tatizo linakuwa kwenu, hivyo mtoto mpeni haki yake ya matunzo na malezi!.

Mwanamke hata akiwa amekosea kiasi gani lakini machozi na maumivu yake ni laaana tosha!, huwezi kutoboa kamwe kama akiwa anamuangalia mwanaye anateseka na wakati Baba yake yupo kazi kulewa tu na kubadili wanawake, hakika huto toboa!.

Hebu wanaume wenzangu tubadilike ndugu zangu,kiukweli inaumiza sana kukutana na mwanamke anaomba nauli wakati Baba yake yupo!

Chanzo cha watoto wetu kuaribika tatizo huanzia pia kwa Wanaume wanaowatelekeza wanawake wao! Tusiishie kuwalaumu Marekani na Nchi zilizoendelea kwa kutuleta Ushoga bila kubadilika sisi wenyewe na kutatua matatizo yetu!.

Wewe unamuacha mwanao wa kiume analelewa na mama yake, unategemea nini?!.

Hebu naomba tubadilike! Tuache Upuuzi!
Nipe namba ya huyo dada na mimi nimsaidie
 
Bila shaka baba wa huyo mtoto atakua THE CHARISMATIC FELLA, ENTERTAINER AND GAME CHANGER, zao la SAUT.
 
Back
Top Bottom