Leo sayari zile 7 zitaonekana angani kwa mara ya mwisho na hutaziona tena hadi mwaka 2040

Leo sayari zile 7 zitaonekana angani kwa mara ya mwisho na hutaziona tena hadi mwaka 2040

𝗟𝗘𝗢 𝗦𝗔𝗬𝗔𝗥𝗜 𝗭𝗜𝗟𝗘 𝗦𝗔𝗕𝗔 𝗭𝗜𝗧𝗔𝗢𝗡𝗘𝗞𝗔𝗡𝗔 𝗔𝗡𝗚𝗔𝗡𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗪𝗜𝗦𝗛𝗢 𝗨𝗧𝗔𝗭𝗜𝗢𝗡𝗔 𝗧𝗘𝗡𝗔 𝗛𝗔𝗗𝗜 𝟮𝟬𝟰𝟬

View attachment 3251250

😉 Kama ulikua na hamu ya kuziona Sayari zile saba zikijipanga kwenye mstari mmoja mnyoofu basi Leo ndo itakua siku ya Mwisho kuziona kama bado hujaziona.

View attachment 3251252

💡 Leo jioni tukio la Nadra la Sayari kuonekana live litaweza kutokea wiki hii ya mwisho wa Mwezi Februari usipojaaliwa kuiona Leo basi mpaka 2040 ndo zitaweza kuonekana tena kwenye macho ya watu Sayari zote saba.

🔆 Utaweza kuziona kuanzia Mars,Jupiter, Uranus, Venus(Zuhura), Neptune, Mercury na Saturn (Zohari) 🪐 huku muda Bora wa kutizama ni wakati wa jua linapozama mida ya jioni.

View attachment 3251253

🚀 Kumbuka Sayari ambazo utaziona kwa uzuri kupitia macho yako ni Venus, Jupiter, Mars zitaonekana wazi Huku Sayari zingine utaziona lakini kwa Udhaifu hivyo itakupa umakini wa kutulia Angani ili kuziona.
Kwanini sayari ya Jupiter ina kitu kama ringi/pete kuizunguka tofauti na sayari zingine?

Ina maana hiyo pete haviachani na sayari tangu kuumbwa kwake?
 
Acha ufala kwani yeye ni Mungu badala umshukuru Mungu kwa uhai na anga unamshukuru mwanadamu u siuchawa sasa ni ujinga
Daaaa! Mkuu, mbona hivyo? Haujaelewa maana ya huu ujumbe wake? Jamaa "anawakejeri" wale waimba MAPAMBIO, ambao kila kitu, ni 'MAMA, MAMA, NANI KAMA MAMA'!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Angani usiku kuna vitu vitu vinachanganya sana kwa mionekano yake ya kuwakawaka na kutoa mwanga na miale. Kuna nyota, sayari, vimondo, satelaiti na ndege ongeza na wadudu na vibwengo. Vile ambavyo vimetulia havisogei kwa haraka ndio huchanganya haijulikani zipi ni nyota na zipi ni sayari zote zinafanana. Ndege zisizo na kitaa chekundu kinachowakawaka nazo huwa ni ngumu kuzitofautisha na satelaiti. Kuna wale wadudu wawakao usiku nao ni vigumu kuwatofautisha na vibwengo. Vimondo vyenyewe vina kasi kasi kubwa na hupotea haraka angani. Ishu ni kutofautisha nyota na sayari wakati wa usiku zote hufanana
 
Kuna dalili ya kuwa na mawingu siku ya Leo!!!
Hali ya hewa ya dar huwa haitabiriki mkuu, kwa mtu aliyeamka kuanzia mida ya saa mbili asubuhi angeweza kukuona muongo, kwa jua linalowaka muda huu utadhani hakukuwa na mawingu mazito wala dalili ya mvua masaa machache yaliyopita
 
Tutatambuaje kama hizi ndizo sayari maana ni ngumu kuzitofautisha na nyota zingine kwa kuwa ukubwa wa nyota na sayari ni kama unalingana tu na hizo heavenly bodies ni kama nyingi sana so inakuwia vigumu kutambua kipi ni kipi
Just try to spot anything in a straight line mkuu, umeshaambiwa zitakuwa kwenye mstari mmoja mnyoofu, hizo nyota and other heavenly bodies mara nyingi huwa ziko scattered au hutengeneza random shapes
 
Kwanini sayari ya Jupiter ina kitu kama ringi/pete kuizunguka tofauti na sayari zingine?

Ina maana hiyo pete haviachani na sayari tangu kuumbwa kwake?
Mkuu mbona siyo jupiter pekee yenye rings, hata saturn, uranus, na neptune nazo zina rings, tena saturn ndio maarufu kwa kuwa na rings maana zake ni kubwa, na huonekana zaidi kuliko rings za hizo sayari nyingine, ambazo ni ndogo na huonekana kwa tabu
 
Mwezi huu niliona Kama nyota 21 zimepangana zikifuatana angani.Nilishangaa sikujua ni kitu gani.
 
Back
Top Bottom