Leo tukumbushane vipindi vya RFA na watangazaji wote miaka hiyo kuanzia 2005 pamoja na watangazaji wa vipindi

Leo tukumbushane vipindi vya RFA na watangazaji wote miaka hiyo kuanzia 2005 pamoja na watangazaji wa vipindi

Bolibgo time Msabaha zubeir akishika mic ilikuwa hatari na nusu unakula bia Villa park ukimbip anakurusha kwa hewa.....
Those days
 
Prince Baina Kamukulu.. Alikua anasimulia Movies za kihindi Kila Jumapii kuanzia saa nne kamili usiku.
Muda huo nanyoosha na kuandaa nguo na viatu vya shule kesho yake.
Kale ka feeling na hisia mpaka leo huwa nakumbuka na huwa na wakumbuka watu niliokua nao kipindi hicho.
 
Mpaka sasa RFA Ina vipindi vizuri sana wanajitahidi sana japo vingine wamevitoa kama kipindi cha nyimbo za kihindi ikibidi wakirudishe bana.
 
Leo nimekumbuka nyuma hapo 2005/2006 nakuendelea VIPINDI VYA RFA hakika vilikuwa ni VIPINDI vizuri sana.

Nakumbuka kulikuwa na kipindi kinaendeshwa na mwanadada ajulikanae kama Grory Robson mtoto wa mama sabuni, kulikuwa na sindano tatu za moto na Fredwaa.

Kipindi Cha search Line simkumbuki mtangazaji wake ila alikuwa dada mmoja hivi, jioni unakutana na kipindi Cha mambo mambo eee hatari Sana.

Sitasahau na Sky Woker, hakika tulipata burudani nzuri sana ya vipindi RFA hakika tutamiss sana Vibe la WATANGAZAJI wa RFA. Karibuni tuflashback wakuu.

RFA si ya juzi tu hapa? Hapo ni suala la kukumbushana au kusimuliana tu. Hiyo radio iliyoanza huku Taji Liundi ameshafanya kazi Radio One na kufukuzwa, nayo ni kukumbushana mambo?

Ova
 
Daah umekumbusha mbali aise. Nikikosa hicho kipind lazim niulize mwendelezo kwa wafuatiliaji wenzangu. Hamna kitu kilikuwa kinakera kama redio kukatika. Sijui ilikuwa inasababishwa na nini?
Tangazo lake alifanya skywalker lilikuwa linasema utaenda wapi zaidi ya hapa walipokuzoea, wewe ni wa hapa hapa.
 
Kuna beat Moja la Tkzee, Shibobo. Lilikuwa linapigwa kwenye kipindi Cha michezo saa mbili Asubuhi, ilikua balaa
 
Nakumbuka 2005 tukiwa Rocken Hill secondary KAHAMA siku ya jumapili tunafua nguo bweni zima huku tumeizunguka radio tunasikiliza kipindi cha sintosahau aiseee ilikua poa sana
 
Mpaka leo hii radio yangu namba 1 ni RFA siwezi kujiskia vizuri ipite siku sijamsikia Rebeka Mulesi aiseeee ntaugua homa kali ya mafua.
 
Back
Top Bottom