Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Wazungu hawatuzid akili mkuu. Ila ni watu walioweka bidii kujifunza kila kitu coz wanaamin kwenye Kufanya research na kurisk. Na wana kanuni usimuamshe aliyelala. Nikija kwenye swali lako. Huyu Mungu tunaefundishwa kumuabudu tunamjua kwa asilimia 0.002 tu. Na hii dunia tunayoishi tunaifahamu kwa kiasi kidogo sana. Ndio maana kila cku watu wanavumbua vitu. Katikati kuna Malaika kabisaa wanaishi na Mashetan vile vile.
 
Natoa code Kidogo Vunja jungu anaishara kubwa sana ya mafanikio. Ukitaka kuamini siku ukimuona, ama akiwa amakurukia mwilini alafu katulia, subili baada ya siku chache ama siku hiyohiyo utapata kitu kizuri sana sana hela, ama dili la hela ndefu kabisa. Na kama Kuna mtu alikuwa anazuia ujue kafeli
 
Sio wazungu tu hata waafrika tena wa bongo wana imani na huyu mdudu. Akija kwako na kuonesha rangi nyekundu umekwisha, kuna balaa na mkosi utakutokea. Akionesha rangi ya kijani una kheri na bahati. Ana rangi nyingi na kila rangi ina ujumbe wake. Wengine humuua mdudu huyu haraka sana wakimuona kwenye makazi yao asije akawaonyeshea rangi hatari
 
Suala la kujua vitu vingi ni sawa,hata sisi tunavijua vitu vingi pia ambavyo wao hawavijui. Mimi nimemuelewa sana mleta mada,nipo hapa kujifunza nisiyoyajua.
Vitu vingi vya kwetu wanavijua maana wametutawala na ni wadadisi sana,mfano wajerumani wanatufahamu sana kupitia naandishi yaliyoachwa na watawala enzi za mkoloni
 
Hizo rangi anazioneshaje Mkuu?
 
Maelezo yako yanajicontradict,nara useme wazungu hawana akili kutuzidi,mara useme wanafanya sana reseach!!hizo ndio akili zenyewe sasa
 
Hizo rangi anazioneshaje Mkuu?
ana mabawa huwa anayafunua na kuwa kama ya kipepeo ila yake ni marefu. Hayo mabawa yana michirizi yenye rangi saba kama za upinde wa mvua. Rangi itakozidi kuonekana ndiyo salamu yako upate habari ni ishara gani, ya bahati au balaa au onyo au taarifa zingine zitakazokutokea.
 
Kumbeee mi nimemuona hv karibuni na kuna safar ya nje ya nchi naifuatilia na ilikua inanifikirisha sana hyo safari
 
Kwa hiyo vunja jungu alimpiga roba nyoka?au kinyoka kilikuwa kidogo?Namuogopa sana huyo mdudu Mimi tangu utotoni mpaka leo
 
Sio vunja jungu Tu, wadudu wengi wanna codes, tulivyo Kua wadogo tulikua tunahusianisha vunja jungu ama Bruce Lee Na vitu vungi Tu, basi hadi Leo nikimuona napata hisia flani hv
 
Ndio nasikia leo licha ya kumwona sana utotoni na tulikuwa tunamwita papa.
 
Hata mimi naijua hii, kuna nyumba nilishi mwaka juzi nikawa nawaona mara kwa mara wakubwa wenye afya,, ndo faza house alivyopata hela hicho kipindi loh, mi nikiwaona tu ujue kuna mchongo umetiki km sio kwangu basi nyumba husika nitakayokuwepo, japo namuogopa anasisimua sana jinsi anavyojongea
 
Mbona hizi ni sifa za kinyonga? Vunja jungu naye ana sifa hizo?
maeneo anapoishi kinyonga na huyu mdudu huishi ndio maana humchanganya kinyonga aone ni majani ya mti tu. Wapo mpaka vyura wanaojibadilisha rangi kwendana na mazingira, mpaka nyoka na wadudu wengine wanaojibadilisha rangi ili wajifiche. Shangaa kuna ndege hutaga mayai ardhini yanayofanana na udongo na mawemawe au mchanga ili kuchanganya adui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…