Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Mantis is so useful,
Alivyo ni mdudu imara,kichwa chake kinazunguka kwa nyuzi 360, ana uimara wa kumuona adui kwa HARAKA sana,na kukabiliana nae,wenzetu huko ngambo humuhusisha mdudu huyu na maombi Fulani siyaweki hapa,lakini baada ya kuko mbine,huwa na nguvu kubwa sana ya kushinda uadui wowote ule,maneno mabaya visasi,nguvu za kiza,pia hukupa ushindi kwa kila ukifanyacho,maombi hayo huambatana na imani za fikra zaidi.(yoga)+(meditation)
 
Kwani Hadi saa Tisa kasoro hii haujala tatizo ni Nini haswa?au unaleta Yale mambo yetu ya kula Kwa picha ya samaki?

Huu mji unaweza ukakufanya ukawa bize mpaka ukasahau Kula.
Huku JF Joannah ananipa Stress
Huku mtaani bills kama zote na siku zinakimbia kama upepo.
 
Huu mji unaweza ukakufanya ukawa bize mpaka ukasahau Kula.
Huku JF Joannah ananipa Stress
Huku mtaani bills kama zote na siku zinakimbia kama upepo.
🤣🤣🤣🤣🤣Naomba nikuache mtibeli wa watu usije pata vidonda vya tumbo ukanisingiza bure
 
Ndugu wana nzengo amani iwe kwenu.

Leo kuna jambo naomba tushirikishane uzoefu limeniumiza kichwa muda mrefu sana.

Katika maisha yangu nimebahatika kuishi na wazungu kwa ukaribu sana kiasi kwamba nilipaswa kujuwa ukweli wa ninachokiuliza lakini wazungu ni wagumu kufunguwa codes, ukiwauliza wanakwambia just for fun.

Nimeishi kwa mabeberu, nimefanyakazi nao Africa kwenye tourist industry lakini kuna vitu nakosa majibu.

Nimefanyakazi kwenye hunting company, mpaka leo bado sijaelewa vizuri ukiacha trophy za meno ya tembo hawa wanyama wengine wana thamani ya trophy kwa zile pesa wanazospend kuja Africa?

Maswali ni mengi kuliko majibu, sasa tuache yote leo nataka kujuwa kuhusu wazungu wanaofuga Mantis (Vunja jungu) je ni kweli hawa Vunja jungu wana super natural? je ni za namna gani? Zinamsaidia vipi huyu anayewatunza Vunja jungu? Kuhusu Swala la kujifurahisha tu hilo nimelikataa ndani ya ubongo wangu.

Yani huwezi kuamini mzungu yupo ulaya au America maisha yake yote na uchumi wake wote unatokana na hawa Vunja jungu, je kuna siri gani? Kuna elimu gani ambayo wazungu wanaojuwa na hawatoi codes?

Yani Africa mtu unajitutumuwa kufuga Kuku, Ng'ombe, mbuzi na hutoboi, inakuwaje hawa jamaa wanatobowa kwa Vunja jungu? tena wanawachukuwa kwetu na kuwasafirisha kwa magendo?

Cc: Mshana Jr Rakims Pascal Mayalla

Huyu Mdudu ni nouma nlishawahi kuona clip anamuua nyoka, nilishangaa sana

Mantis ni jamii ya Insect, ni Insect pekee mwenye kuweza kuzungusha kichwa pande zote ili kuona chochote hasa wadudu wadogo wadogo ambao yeye huwala..kwa style hiyo wazungu wanasema wanasali/swali

wazungu pia wanawafuga hawa kwenye Gardens zao kwaajili ya kupunguza au kuondoa Mbu, Inzi na wadudu wengine

Huyu hana tofauti sana na Owl...yaani Bundi...ambao nao huzungusha kichwa pande zote na hula panya na mijusi ni vile Bundi ni master wa usiku

Sidhani km kuna kingine
 
Kwa hiyo vunja jungu alimpiga roba nyoka?au kinyoka kilikuwa kidogo?Namuogopa sana huyo mdudu Mimi tangu utotoni mpaka leo
Nyoka mkubwa wa kummeza hata panyabuku.

Nyoka alikuwa anamnyatia vunja chungu ili amtafune. Vunja jungu akamuona na kumuwahi kwa roba iliyopelekea nyoka kuwa chakula cha mchana cha vunja jungu siku hiyo 😂😂😂. Nimekutumia picha uone jinsi nyoka alivyokuwa anahanga kujinyonga nyonga ili kujitoa katika roba ya vunja jungu bila mafanikio.
 
Attachments

  • Screenshot_20230803-140813.png
    Screenshot_20230803-140813.png
    185.8 KB · Views: 9
Nataka tujikite na tuzame kwa undani, kuna kitu wazungu wanakijuwa lakini nadhani wamekula kiapo kabisa asijue mtu yeyote nje ya jamii yao.

Sasa si vibaya tukifanya vireseach vyetu wenyewe.

Ona kama Bongo zozo anazunguka dunia ukimuuliza source of income yake atakwambia ni forex trading, uwongo mtupu.
Mirror effects, fungua hiyo code mwenyewe, au moon effects.
 
Mirror effects, fungua hiyo code mwenyewe, au moon effects.
Kwa Imani yetu ya kimila Sisi kwetu Vunjajungu siku zote analeta msg, na kwetu huwa tunapata faraja Sana tunapomkuta ndani, tulishawahi kupotea kaburi la Bibi yetu yaani tulishahangaika mpaka tukataka kukata tamaa from no where akaja yeye taratibu akaenda mpaka kwenye kaburi husika kisha akatulia. Tulilia kweli kweli. Tukaja kuambiwa ni kweli Hilo ndo kaburi sahihi la Bibi yetu. Hivyo kila mtu na anavyomchukulia huyu Vunja jungu.
 
Wazungu sometimes hupenda kuyafanya mambo ambayo sisi tunayaona madogo, wao huyafanya makubwa. Mambo ambayo sisi tunayaona hayana maana wao huyafanya ya maana.

Unakuta mtu anatengeneza mechi ya mapigano kati ya vunja chungu na mende, nyoka au wadudu wengine hatari afu anaweka kiingilio cha pambano ambapo watu wanaingia kuangalia, au wengine wanafuatilia pambano hilo kupitia YouTube nk. Na kupitia pambano hilo unakuta mtu anavuna madolar ya kutosha. Afu mara nyingi vunja jungu ndo hushinda mapambano hayo 😂😂😂
Kuna pambano nimeshahudia vunja jungu akiuwa nyoka. Aisee vunja jungu yupo vizuri kwa kung fuu, na akikupiga roba moja tu kwisha habari yako. Maana ni mfano wa roba yenye mbao ya misumari.
Tangu siku niloona clip vunjajungu anaua nyoka nimezidi kumuogopa
 
Back
Top Bottom