Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Vunja jungu huyuhuyu nilivyokuwa mdogo tulikuwa tunatishana ukimuua vunja jungu na vyombo vya udongo vya kwetu vyote vinavunjika..

Nitarudi kusoma comments zaidi
Kheri yako wewe kama ulikuwa na courage hata ya kumuua...mimi huyu mdudu tangu udogo wangu mpk hivi mtumzima namuogopa. Nikijikaza kumuua basi nimpulizie dawa ya kuua wadudu labda. Halafu mshari huyu mdudu kama umempeleza, ukipita karibu yake utaona anageuza kichwa kukuangalia, mara utamuona anainua makono yake kama anataka kupigana boxer 😆
 
Hao watakuwa na Imani ya nguvu ya mwezi na jua, nguvu zilizotumika zamani kupata nguvu katika vita na mafanikio.
 
Aisee, kuhusu bahati naweza kukubali maana nilimuona kama wiki mbili zilizopita.

Sasa nimepata upepo wa pesa hata sikuutarajia.
 
Wewe bila shaka ummekulia mjini. Sisi tuliokulia shamba hawa tunaishi nao kila siku hasa wakati wa mvua ni wengi.
 
Duh
 
Mwingine huyu. Mtoto wa mjini. Sisi tuliokulia shamba hawa wako kila mahali, hasa wakati wa mvua. Wanaingia ndani na chakula chao ni wadudu wadogo. Ukiwasha taa usiku inavutia wadudu wengi hivyo na yeye anaingia ndani kuwinda wadudu. Wakati mwingine anakumbuka na wale mijusi wa ndani wanamgeuza kitoweo. Mwinda kawa mwindwa!
 
Ile movie nishaiona. Walipiganisha ili kujifundisha style za kupiga karate. Unajua hiyo miguu yake ya mbele wanapopigana huwa wanatumia kama mikono ya binadamu anapopigana zile style za kina Bruce Lee.
 
Ni kwa vile Imani zipo za namna nyingi ila hii inaweza kukukutanisha na roho nyingine za uharibifu pasipo kujua. Unapohusisha Imani katika muunganiko na kiumbe kama chanzo cha nguvu ni sawa na kunuiza na kutegemea nguvu kutoka katika chanzo kisicho rasmi sana ndiyo maana unaona mtu anayefanya hivi inakuwa ni siri yake
 
Afrika bado tuna safari ndefu sana . !!! Hivi na wewe unajiita great thinker kweli? Wazo la kijinga kama hili linaweza vipi kukaa kwenye ubongo wa mwanadamu anae fikiri sawa sawa?
Maisha yamekushinda sasa unataka kufanikiwa kupitia vunja chungu!!! Na wewe una PHD kabisaaa au umejipa jina tu?
 
Kweli wadada ni wadada tu [emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…