Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Vunja jungu huyuhuyu nilivyokuwa mdogo tulikuwa tunatishana ukimuua vunja jungu na vyombo vya udongo vya kwetu vyote vinavunjika..

Nitarudi kusoma comments zaidi
Kheri yako wewe kama ulikuwa na courage hata ya kumuua...mimi huyu mdudu tangu udogo wangu mpk hivi mtumzima namuogopa. Nikijikaza kumuua basi nimpulizie dawa ya kuua wadudu labda. Halafu mshari huyu mdudu kama umempeleza, ukipita karibu yake utaona anageuza kichwa kukuangalia, mara utamuona anainua makono yake kama anataka kupigana boxer 😆
 
Ndugu wana nzengo amani iwe kwenu.

Leo kuna jambo naomba tushirikishane uzoefu limeniumiza kichwa muda mrefu sana.

Katika maisha yangu nimebahatika kuishi na wazungu kwa ukaribu sana kiasi kwamba nilipaswa kujuwa ukweli wa ninachokiuliza lakini wazungu ni wagumu kufunguwa codes, ukiwauliza wanakwambia just for fun.

Nimeishi kwa mabeberu, nimefanyakazi nao Africa kwenye tourist industry lakini kuna vitu nakosa majibu.

Nimefanyakazi kwenye hunting company, mpaka leo bado sijaelewa vizuri ukiacha trophy za meno ya tembo hawa wanyama wengine wana thamani ya trophy kwa zile pesa wanazospend kuja Africa?

Maswali ni mengi kuliko majibu, sasa tuache yote leo nataka kujuwa kuhusu wazungu wanaofuga Mantis (Vunja jungu) je ni kweli hawa Vunja jungu wana super natural? je ni za namna gani? Zinamsaidia vipi huyu anayewatunza Vunja jungu? Kuhusu Swala la kujifurahisha tu hilo nimelikataa ndani ya ubongo wangu.

Yani huwezi kuamini mzungu yupo ulaya au America maisha yake yote na uchumi wake wote unatokana na hawa Vunja jungu, je kuna siri gani? Kuna elimu gani ambayo wazungu wanaojuwa na hawatoi codes?

Yani Africa mtu unajitutumuwa kufuga Kuku, Ng'ombe, mbuzi na hutoboi, inakuwaje hawa jamaa wanatobowa kwa Vunja jungu? tena wanawachukuwa kwetu na kuwasafirisha kwa magendo?

Cc: Mshana Jr Rakims Pascal Mayalla

Hao watakuwa na Imani ya nguvu ya mwezi na jua, nguvu zilizotumika zamani kupata nguvu katika vita na mafanikio.
 
Aisee, kuhusu bahati naweza kukubali maana nilimuona kama wiki mbili zilizopita.

Sasa nimepata upepo wa pesa hata sikuutarajia.
 
Sio wazungu tu hata waafrika tena wa bongo wana imani na huyu mdudu. Akija kwako na kuonesha rangi nyekundu umekwisha, kuna balaa na mkosi utakutokea. Akionesha rangi ya kijani una kheri na bahati. Ana rangi nyingi na kila rangi ina ujumbe wake. Wengine humuua mdudu huyu haraka sana wakimuona kwenye makazi yao asije akawaonyeshea rangi hatari
Wewe bila shaka ummekulia mjini. Sisi tuliokulia shamba hawa tunaishi nao kila siku hasa wakati wa mvua ni wengi.
 
ana mabawa huwa anayafunua na kuwa kama ya kipepeo ila yake ni marefu. Hayo mabawa yana michirizi yenye rangi saba kama za upinde wa mvua. Rangi itakozidi kuonekana ndiyo salamu yako upate habari ni ishara gani, ya bahati au balaa au onyo au taarifa zingine zitakazokutokea.
Duh
 
Kheri yako wewe kama ulikuwa na courage hata ya kumuua...mimi huyu mdudu tangu udogo wangu mpk hivi mtumzima namuogopa. Nikijikaza kumuua basi nimpulizie dawa ya kuua wadudu labda. Halafu mshari huyu mdudu kama umempeleza, ukipita karibu yake utaona anageuza kichwa kukuangalia, mara utamuona anainua makono yake kama anataka kupigana boxer 😆
Mwingine huyu. Mtoto wa mjini. Sisi tuliokulia shamba hawa wako kila mahali, hasa wakati wa mvua. Wanaingia ndani na chakula chao ni wadudu wadogo. Ukiwasha taa usiku inavutia wadudu wengi hivyo na yeye anaingia ndani kuwinda wadudu. Wakati mwingine anakumbuka na wale mijusi wa ndani wanamgeuza kitoweo. Mwinda kawa mwindwa!
 
Angalia movie ya Bruce inter the Dragon, wakati wapo kwenye mashua kutoka Hong Kong kwenda kwenye kisiwa cha Dragon kwenye ile mashuwa walikuwemo Bruce Lee, Jim Kelly, Jim Brown na wengine siwakumbuki, kuna Mantis walitumika pale walipiganishwa.

Hii movie Bruce inter the Dragon kama sikosei ilichezwa mwaka 1976, Vunja jungu alikuwemo kama hiden code.
Ile movie nishaiona. Walipiganisha ili kujifundisha style za kupiga karate. Unajua hiyo miguu yake ya mbele wanapopigana huwa wanatumia kama mikono ya binadamu anapopigana zile style za kina Bruce Lee.
 
Mantis is so useful,
Alivyo ni mdudu imara,kichwa chake kinazunguka kwa nyuzi 360, ana uimara wa kumuona adui kwa HARAKA sana,na kukabiliana nae,wenzetu huko ngambo humuhusisha mdudu huyu na maombi Fulani siyaweki hapa,lakini baada ya kuko mbine,huwa na nguvu kubwa sana ya kushinda uadui wowote ule,maneno mabaya visasi,nguvu za kiza,pia hukupa ushindi kwa kila ukifanyacho,maombi hayo huambatana na imani za fikra zaidi.(yoga)+(meditation)
Ni kwa vile Imani zipo za namna nyingi ila hii inaweza kukukutanisha na roho nyingine za uharibifu pasipo kujua. Unapohusisha Imani katika muunganiko na kiumbe kama chanzo cha nguvu ni sawa na kunuiza na kutegemea nguvu kutoka katika chanzo kisicho rasmi sana ndiyo maana unaona mtu anayefanya hivi inakuwa ni siri yake
 
Afrika bado tuna safari ndefu sana . !!! Hivi na wewe unajiita great thinker kweli? Wazo la kijinga kama hili linaweza vipi kukaa kwenye ubongo wa mwanadamu anae fikiri sawa sawa?
Maisha yamekushinda sasa unataka kufanikiwa kupitia vunja chungu!!! Na wewe una PHD kabisaaa au umejipa jina tu?
 
Kheri yako wewe kama ulikuwa na courage hata ya kumuua...mimi huyu mdudu tangu udogo wangu mpk hivi mtumzima namuogopa. Nikijikaza kumuua basi nimpulizie dawa ya kuua wadudu labda. Halafu mshari huyu mdudu kama umempeleza, ukipita karibu yake utaona anageuza kichwa kukuangalia, mara utamuona anainua makono yake kama anataka kupigana boxer [emoji38]
Kweli wadada ni wadada tu [emoji16]
 
Back
Top Bottom