Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Leo tupeane uzoefu wako, unajua nini kuhusu huyu kiumbe vunja jungu? (Mantis) je ni kweli ana super natural kama wazungu wanavyoamini?

Swala la kujifurahisha tu
hili ndo jibu Dr Matola PhD

kuna watu wanavutiwa sana na wanyama, wazungu wanakua sana na hulka hii labda kwasababu hawakai karibu na mazingira asili

ukipita mitandaoni utaona wazungu wanafuga wanyama mbalimbali kuanzia wadudu kama panzi mpaka ndege kama kunguru, bundi... na kuna wazungu wanaona ni bora kua na mbwa kuliko kulea mtoto.... hawa wanayama wa kufugwa hivi wanawaita 'pets'
 
Nataka tujikite na tuzame kwa undani, kuna kitu wazungu wanakijuwa lakini nadhani wamekula kiapo kabisa asijue mtu yeyote nje ya jamii yao.

Sasa si vibaya tukifanya vireseach vyetu wenyewe.

Ona kama Bongo zozo anazunguka dunia ukimuuliza source of income yake atakwambia ni forex trading, uwongo mtupu.
Wapo kiajent kutoka mashirika ya Ujasusi
 
Ndugu wana nzengo amani iwe kwenu.

Leo kuna jambo naomba tushirikishane uzoefu limeniumiza kichwa muda mrefu sana.

Katika maisha yangu nimebahatika kuishi na wazungu kwa ukaribu sana kiasi kwamba nilipaswa kujuwa ukweli wa ninachokiuliza lakini wazungu ni wagumu kufunguwa codes, ukiwauliza wanakwambia just for fun.

Nimeishi kwa mabeberu, nimefanyakazi nao Africa kwenye tourist industry lakini kuna vitu nakosa majibu.

Nimefanyakazi kwenye hunting company, mpaka leo bado sijaelewa vizuri ukiacha trophy za meno ya tembo hawa wanyama wengine wana thamani ya trophy kwa zile pesa wanazospend kuja Africa?

Maswali ni mengi kuliko majibu, sasa tuache yote leo nataka kujuwa kuhusu wazungu wanaofuga Mantis (Vunja jungu) je ni kweli hawa Vunja jungu wana super natural? je ni za namna gani? Zinamsaidia vipi huyu anayewatunza Vunja jungu? Kuhusu Swala la kujifurahisha tu hilo nimelikataa ndani ya ubongo wangu.

Yani huwezi kuamini mzungu yupo ulaya au America maisha yake yote na uchumi wake wote unatokana na hawa Vunja jungu, je kuna siri gani? Kuna elimu gani ambayo wazungu wanaojuwa na hawatoi codes?

Yani Africa mtu unajitutumuwa kufuga Kuku, Ng'ombe, mbuzi na hutoboi, inakuwaje hawa jamaa wanatobowa kwa Vunja jungu? tena wanawachukuwa kwetu na kuwasafirisha kwa magendo?

Cc: Mshana Jr Rakims Pascal Mayalla

me cjui

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Wazungu sometimes hupenda kuyafanya mambo ambayo sisi tunayaona madogo, wao huyafanya makubwa. Mambo ambayo sisi tunayaona hayana maana wao huyafanya ya maana.

Unakuta mtu anatengeneza mechi ya mapigano kati ya vunja chungu na mende, nyoka au wadudu wengine hatari afu anaweka kiingilio cha pambano ambapo watu wanaingia kuangalia, au wengine wanafuatilia pambano hilo kupitia YouTube nk. Na kupitia pambano hilo unakuta mtu anavuna madolar ya kutosha. Afu mara nyingi vunja jungu ndo hushinda mapambano hayo 😂😂😂
Kuna pambano nimeshahudia vunja jungu akiuwa nyoka. Aisee vunja jungu yupo vizuri kwa kung fuu, na akikupiga roba moja tu kwisha habari yako. Maana ni mfano wa roba yenye mbao ya misumari.
Dah, roba ya mbao tena
 
Nataka tujikite na tuzame kwa undani, kuna kitu wazungu wanakijuwa lakini nadhani wamekula kiapo kabisa asijue mtu yeyote nje ya jamii yao.

Sasa si vibaya tukifanya vireseach vyetu wenyewe.

Ona kama Bongo zozo anazunguka dunia ukimuuliza source of income yake atakwambia ni forex trading, uwongo mtupu.
Bongo zozo kumbe ni forex trader?
 
Waba akili sana wale watu,kuna vitu vingi wanavijua na sisi hatuvijui na hatutakuja kuvijua

Binafsi, nakataa kwamba ni suala la Akili, kwamba wametuzidi sana Akili.

Mtoto wa Kizungu anafuga nyoka chumbani kwake kwenye box la kioo, ukiuliza utaambiwa “that’s Brian’s pet snake” ila mtoto wa Tandale kwa Tumbo akikutwa na nyoka chumbani tena kwenye box la kioo utaambiwa “ule ni mzimu wa family yao, ndio unawapa hela!”


Wametuzidi matumizi ya Akili.
 
Huwa namuogopa sana huyu mdudu, hivi karibuni nilimkuta chumbani kwangu tena maliwatoni,
alikuwa na rangi ya kijani, nikampulizia dawa ya kuulia wadudu akafa.
 
Maisha yana siri.....

Ukitaka ujue ni siri hebu jiulize.....

Ni wapi ulikuta wenye nidhamu ya kuchunga maneno wakaelezea yote walioyaona JANDONI ama UNYAGONI ?!!!

Uliona wapi wazalishaji bidhaa kama "Coca Cola" wakaweka wazi jinsi ya kutengeneza bidhaa hiyo ?!!!

Sijawahi kuona mitandaoni watu wakiwa wanafahamu kutengeneza soda mathalani "Coca Cola"[emoji1787][emoji1787]

Kwanini viko vitu vingi ambavyo watoto wanatumia pesa nyingi za baba zao kusomeshwa shuleni kwa miaka mingi ilihali viko wazi tu mitandaoni?!!!....

Jibu ni kuwa hivi havina MADHARA makubwa kwa "wanaomiliki" njia kuu za uchumi....ni tofauti na hao mathalani "Coca Cola"....

Je Coca Cola wanachangia fedha kiasi gani kwa taasisi kubwa za "kibepari" duniani?!!!

Chenye thamani na faida maradufu huwa hakiwezi kupatikana KIRAHISI....kinagubikwa na USIRI MKUBWA....

Ukitaka ujue katika ulindaji SIRI pia hutumika UPOTOSHAJI kwa walio wengi(miluzi mingi kumpoteza mbwa) wewe angalia jinsi wakati wa COVID-19 SHIRIKA LA AFYA DUNIANI lilipotuambia kuwa AFRIKA tutakufa kwa kuanguka barabarani kama nzi ilihali wataalamu wetu "locally" wakasema TUISHI NAYO TU NA ITAPITA kwani MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA VIRUSI hayana TIBA.....miili itazoea tu ..na kweli afrika "hatukutandikwa" sana kama zilivyokuwa "projection" za "WHO"....je ni kweli kabisa "walioverlook" ama ni SIRI ndani ya SIRI ?!!! [emoji1787][emoji1787]

Waturuki wana msemo wao kuwa usiwe "MUWAZI".....[emoji1787]

Back to the topic......

Wanyama ,wadudu ,miti ,mimea inategemeana.....

Kila mmea ,kila mnyama ,kila mti una faida zinazoonekana na zisizoonekana kwa urahisi....

Una faida zinazojulikana na wachunguzi ,na wanasayansi na zile zinazoweza kujulikana na wenye HEKIMA NA BUSARA TU....hapa hekima na busara inaweza ikawa kupitia njia za KIDINI....njia za KIPAGANI....njia zinazoitwa "UCHAWI".....

Like it goes " NEVER GIVE WISDOM TO UNWORTHY AS IT IS UNJUST TO THE KNOWLEDGEABLE [emoji1787][emoji1787]

Oooh Mwenyezi Mungu tuongezee BUSARA NA HEKIMA juu ya elimu tunazopata ,amen [emoji120]

#Do Not Do Harm[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Afrika bado tuna safari ndefu sana . !!! Hivi na wewe unajiita great thinker kweli? Wazo la kijinga kama hili linaweza vipi kukaa kwenye ubongo wa mwanadamu anae fikiri sawa sawa?
Maisha yamekushinda sasa unataka kufanikiwa kupitia vunja chungu!!! Na wewe una PHD kabisaaa au umejipa jina tu?
Tamaduni zetu ndio msingi wa maisha yetu
 
Afrika bado tuna safari ndefu sana . !!! Hivi na wewe unajiita great thinker kweli? Wazo la kijinga kama hili linaweza vipi kukaa kwenye ubongo wa mwanadamu anae fikiri sawa sawa?
Maisha yamekushinda sasa unataka kufanikiwa kupitia vunja chungu!!! Na wewe una PHD kabisaaa au umejipa jina tu?
Nimechaguwa kukupuuza tu mjinga kabisa.

Who is profesa? Profesa is someone who knows too much about little thing.

Katafute basha Tiktok.
 
Nimechaguwa kukupuuza tu mjinga kabisa.

Who is profesa? Profesa is someone who knows too much about little thing.

Katafute basha Tiktok.

Kumbe I was right eeh wewe ni zero brain . Zero brain wote huwa wana respond challenge kwa matusi ya nguoni.

Uzi wako ni wa kipuuzi sana aisee sijawahi ona mtu mwenye akili timamu anawaza kama wewe.

Eti kivunja chungu daaah
 
Kumbe I was right eeh wewe ni zero brain . Zero brain wote huwa wana respond challenge kwa matusi ya nguoni.

Uzi wako ni wa kipuuzi sana aisee sijawahi ona mtu mwenye akili timamu anawaza kama wewe.

Eti kivunja chungu daaah
Huwa sirespond mashoga, nimekupa bonus tu Kenge wahed.
 
Nimefika kwa kuchelewa .
Nitarejea kwa mengi zaidi

Jua Anayeomba katika Ndoto anaashiria jinsi ulivyo mtulivu, mvumilivu, mbunifu na dhabiti kama mtu. Pia inamaanisha kuwa unakosa baadhi ya fursa katika maisha yako.

Maana ya Baadhi ya Ndoto za Vunjajungu

Vunjajungu wawili wanaoomba - kupata amani maishani

Kuomba Vunjajungu kuruka - kunyakua nafasi yako
Vunjajunguya kuomba dhahabu - fuata matamanio bila woga

Kuomba vunjajungu kama tattoo - uamuzi mzuri maishani Hakimiliki

[emoji2398] The PleasantDream, Haki zote zimehifadhiwa.



Kukamata vunjajungu - pata utambuzi unaostahili
Vunjajungu Kuua - tengeneza njia yako (Hatima) mwenyewe

Kupigana na vunjajungu kuomba - kutengana na rafiki wa kike

Vunjajungu kuomba kijani kibichi - hatari inakuja kwako

Kuona vunjajungu kwenye gari - kuwa mwangalifu maishani

Kuomba vunjajungu kwenye mkono wako kurejesha ujasiri wako

Praying-mantis-dream-61-61-1024x1024.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom