Leo tuwachane madaktari na manesi kujiona wadogo zake Mungu

Kama hata huwezi kuelewa mfano rahisi huo, itoshe tu kusema heshimu kazi za watu…. eti daktari aanze kusikiliza ushauri wa mgonjwa na ndugu.!
Huna lolote wewe. Huyo Mangi anawezaje kunihudumia bila kunisikiliza. Na kama nikiona hanihudumii ipasavyo inakuwaje? Kama chuoni kwenu mnafundishwa huo ujinga niletee mimi nikufundishe kazi.
Nimekupa mifano halisi kwenye uzi bado unakaza fuvu?
 
Kuna daktari mmoja muhaya pale JKCI anajiona mjuaji sana.
Nilimwambia anisikilize Mimi mgonjwa kwani nimeugua Ugonjwa wangu kwa miaka thelathini yeye amekuwa daktari chini ya miaka mitano hivyo Nina uzoefu kuliko yeye kwenye suala langu hakuta kunisikiza
 
Akishasema mzungu wao hawapingi wala kushughulisha akili tena
 
Ncha Kali soma hapa wewe nesi uchwara
 
Point namba mbili nakubishia. Daktari au mfanya kazi yeyote wa afya haruhusiwi kuoa taarifa ya mgonjwa. Labda mgonjwa mwenyewe akuambie wewe anaumwa nini ila siyo daktari, sheria inawafunga.
 
Kwahiyo unajivunia uzoefu wa kuugua kwa miaka 30!

Eti 'ugonjwa wangu', pathetic.!!
 
Alifeli sana ila na wewe ulifeli pia unayo haki ya kumkataa daktari ila sasa kwenye haka kakijiji ketu unajua ratio ya wagonjwa wangapi kwa daktari mmoja ?
 
Madaktari na manesi wanafanya kazi kubwa sana,badala ya kuwasakama nadhani ungezidi kuwaombea kwa mungu baba mwenyezi.
 
Mkuu OKW BOBAN SUNZU
Unajua ratio ya wagonjwa kwa daktari mmoja ?

Rafiki unajua jinsi ilivyo ngumu kumtibu mtu anayejihisi kujua anaumwa nini kwa miongozo ya Google?

Ndugu unajua ni jinsi gani madaktari na manesi huukataa uhuru wa fikira na saikolojia ili kukuhudumia ?

By the way ni kweli daktari wa hivyo wapo japo sio wote ila wengi wako hivyo je wajua ni kwanini ?

Ujinga wa serikali yenu , madaktari na manesi ni wachache unafanya kazi mpaka kichwa kinauma , je mishahara inaendana na wanachokifanya ? Haiendani .

Bado hujapigiwa simu na wapuuzi wakuitwa RMO na DMO kuhusu mapato ya zahanati, Kituo cha Afya na hospitali pasipo kujua ni vipi wanatatua adha unazopitia kituoni .

Je wajua hata leo nikubebe nikusomeshe ili uwe daktari unaweza usiweze na ukakimbiaa sababu ile ni wito bila wito huwezi kufanya .

Stop kulalamika waelimishe taratibu ila anza na serikali ikubali makosa ndiyi uje huku .

Pole kwa huduma mbovu ya huyo daktari .

Ila nikukumbushe kuwa siku hizi hata nesi , lab technician , pharmacist , na Clinical officer wote wanajiita madaktari hivyo angali usije kuwa unawalaumu watu tajwa hapa kwa jina la daktari maana kutokana na uhaba wa madaktari basi hata hao kuna roles wanasaidia vituoni .

Usisahau kuwa hali ni mbaya mpaka wale Data clerks wa CTC nao vijijini na mijini nao wanajiita madaktari na pia wanatoa misaada kwa wagonjwa na kutoa description ya magonjwa kisa wako karibu na madaktari.

Pole kwa huduma mbaya uliyopata ila chunguza pia is he a real doctor or preffession attacker .?
 
Ugonjwa huonekana kwa dalili na vipimo, sio uzoefu na maelezo pekee….. unataka usikilizwe utibiwe kwa mazoea au majibu ya vipimo?
Wewe mbishi au ni nesi umejishtukia kiasi kwamba hata huelewi hoja. Sasa asiponisikiliza atajuaje kwa kina hizo dalili? Atajuaje dawa zenye madhara kwa mgonjwa? Mf. Mtu ana vidonda vya tumbo kaenda kutibiwa maumivu ya kiuno daktari anampa Diclofenac. Unadhani akimsikiliza mgonjwa angempa hiyo dawa?
 
Asante mkuu kwa maoni yako. Wewe umeeleza mzizi wa tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…