Leo tuwaenzi na kuwakumbuka wazazi wetu waliotangulia mbele za haki

Leo tuwaenzi na kuwakumbuka wazazi wetu waliotangulia mbele za haki

Kama umelelewa na ndugu, watu baki, au na mama pekee au baba pekee kutokana na kufiwa na mama, au baba ama wazazi wote. Tuwakumbuke na kuwaombea waendelee kulala mahali pema peponi. Nasi tutafuata japo hatujui kama tutakutana njia moja. Tuendelee kumwomba Mungu atupe mwisho mwema.

Nimejikuta siko sawa kwa muda baada ya kumkumbuka marehemu baba aliyekufa nikiwa na miaka mitatu. Kumbukumbu niliyobaki nayo ni kuambiwa na mama kwamba baba alikuwa ananipenda sana😭😭😭.

Mliojaaliwa kulelewa na wazazi wote wawili hongereni na msiache kuwapenda wazazi wenu, wahudumieni msichoke. Hivyo unavyobania kuwapa wazazi katu hutozikwa navyo, watachezea na kutapanya wengine.

Mungu ambariki mama yangu, aendelee kujaaliwa afya njema, amepambana sana mpaka nimefikia hapa.

Poleni sana wahanga, duniani tunapita wote pambaneni na maisha mpaka tone la mwisho la jasho na damu👊.

Andika R.I.P kwa mzazi aliyekwisha tangulia mbele za haki, kuna member atakupa pole kwa kureply comment yako, utajisikia vyema.🙏🙏🙏

Mungu awabariki sana 🙏
Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi baba angu.
Nakukumbuka, natamani ningetumia muda mwingi zaid kua nawe, Lakini Mungu aliamua kukuchukua mapema.
Kinachoniuma zaidi ni kuona wote walosababisha kifo chako wako uraiani.
Endelea kupumzika kwa amani.
 
Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi baba angu.
Nakukumbuka, natamani ningetumia muda mwingi zaid kua nawe, Lakini Mungu aliamua kukuchukua mapema.
Kinachoniuma zaidi ni kuona wote walosababisha kifo chako wako uraiani.
Endelea kupumzika kwa amani.
😭😭Mnhuu,walimuua? Pole mpenz...aisee
 
Daah miezi 4 sasaa[emoji24][emoji24][emoji24]Sijui kama kuna mtu duniani anaweza chukua nafasi ya mama japo robo tuu[emoji27][emoji27]
Acha tu Mimi miwili nawaza ikifika birthday yake 12.12 naacha pombe kama kumuenzi
 
Sana mkuu,Kuna watu wametupa na kuwasahau kabisa wazazi
Hao ni suala la muda tu huwa wanakuja kutambua kuwa wazazi hawana mbadala dakika za mwisho

Kwenye misiba ya wazazi ukiacha kulia kwa uchungu wa kuwapoteza wazazi wengine ni kilio cha uchungu pamoja na majuto kwa jinsi hawakuwatendea wazazi wao kwa upendo walipokuwa hai
 
Hao ni suala la muda tu huwa wanakuja kutambua kuwa wazazi hawana mbadala dakika za mwisho

Kwenye misiba ya wazazi ukiacha kulia kwa uchungu wa kuwapoteza wazazi wengine ni kilio cha uchungu pamoja na majuto kwa jinsi hawakuwatendea wazazi kwa upendo walipokuwa hai
kweli mkuu, nimewahi kumuona mmoja.... wanajuta sana
 
Back
Top Bottom