1. Nitapunguza masaa ya kazi kutoka masaa 11 hadi masaa sita yaani kuanzia muda wowote unaoingia kazini iwe saa moja jioni, saa saba mchana, saa kumi na mbili asubuhi, then hesabia kuanzia muda huo then mbele yako ni masaa sita unakuwa umemaliza muda wa kazi na utapisha mtu mwingine aingie shifti yako.
Hii itapunguza kwanza masaa ya kazi na kuwapa wafanyakazi nafasi ya kushiriki shughuli zingine za kijamii kama malezi ya familia, ndoa na biashara.
Lakini pia itapunguza ubwanyenye na umangi meza ambapo mtu anaweza hodhi ofisi na mamlaka na kuyatumia vibaya akijua ofisi yupo pekee yake na hatimae kuleta urasimu na ukiritimba kwenye ofisi za serikali na kuharibu ufanisi.
2. Nitafuta malipo ya mshahara kwa mwezi na kupendekeza taaisisi moja baada ya nyingine kuingizwa katika malipo ya masaa. Yaani masaa sita utalipwa kwa kila lisaa chini ya uangalizi na ukaguzi wa kufa mtu. Hii itapunguza mzigo wa serikali kulipa wafanyakazi hewa, na kulipa watu wasiofanya kazi. Mtu anaingia ofisini na kutoka masaa manne hayupo eneo la kazi ila mwisho wa siku analipwa, kwann analipwa?
3. Watu wataweza kuajiriwa na kuwa na mikataba zaidi ya mitatu. Yaani mfano mtu anaajiriwa CRDB, NMB na Exim, na kote huko anafanya kazi kwa masaa kulingana na uwezo wake. Au anaweza fanya kazi NMB, shirika la posta, na Hotelini kama Serena. Na kazi zote analipwa kwa masaa yake ya utendaji.
4. Nitabadilisha mfumo wa malipo badala ya mwezi waajiriwa watalipwa stahiki zao kwa wiki ili kupunguza msongamano wa malipo mwisho wa mwezi na pia kuwaondolea kadhia raia ya kupata malipo baada ya siku 30.
5. Nitashawishi mitaala ya vyuo vikuu kubadili masomo yasiwe notisi nyingi na mitihani mingi bali yawe ni lecture wastani, presentation za group na individual za kuongea ziongezwe, na seminars sessions,ziwe za kutosha ili kuwapa wanavyuo uwezo wa kitaaluma wa kuchanganua mambo, lakini pia nitashawishi serikali wanavyuo kutumia semester ya kwanza ya kila mwaka wa masomo kufanya field practice kwenye taaisisi mbali mbali popote walipo. Sio tu hadi kusubiri mwaka wa tatu.
Performance zao zikuwa nzuri zitawaruhusu kupata post za internships za kujitolea kwenye makampuni lengwa kulingana na taaluma zao, ili kuwasaidia kupata ujuzi na uzoefu wa kitaasisi na kuweza kutambua uhalisia na changamoto halisi na sio story za vijiweni au hadithi za matutorial na lecturers.
Pia vijana hawa nitashawishi serikali kutenga fungu maalumu waweze kupata vitu basic kama vifurishi vya simu kwaajiri ya mawasiliano, pesa ya chakula na nauli, na posho ya kujikimu kimaisha ili kuweza kuwasaidia kujihudumia kipindi wakiwa wanasubiria kupata mikataba kamili yenye stahiki zote. Watalipwa pia kwa masaa ila kwa 60% ya kiwango anacholipwa mfanyakazi wa kawaida kama basic salary.
6. Nitahakikisha kila taaisisi ya serikali ndani ya departments zake inakuwa na kitengo cha internships na kunakuwa na maofisa wake ambao wata act kama supervisors wa kurepoti kwenye taasisi yenyewe, vyuo, na wizarani kutoa ripoti za kimwenendo za hawa wahusika wataopewa nafasi aidha za trainings au internships.
Nitaongeza points nyingine baadae.