Mkuu Mkandara
pitia hii pia
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/272807-video-sultani-wa-zanzibar-alivyofurahia-mauaji-ya-karume%3B-alitarajia-kurudi-zanzibar-4.html#post4006558 halafu uunganishe dots na hiyo picha/ video.
Ni siku nyingi Zanzibar inataka Muungano ukarabatiwe;
kero za Muungano zitatuliwe. Kila anayejaribu anaishia pabaya.
Mara hii baada ya Wazanzibari kukosa Sauti ya "mtetea" haki zao. CUF ndiyo ilishika bango la kukosoa na kudadisi muungano. CCM ya Zanzibar ni trela la CCM Chimwaga, ni bendera kufata upepo. Wakiambiwa Muungano ni mfumo wa Serikali mbili, wanaitikia, ndiyooo..wakiambiwa serikali mbili kuelekea moja, wanasema "ndioo".
Baada ya sauti za vinara wa CUF kupotea na ulipojitokeza "uchokozi" kuwa Muungano usijadiliwe uwepo wake au kutokuwepo kwake bali mjadala uwe juu ya kuboreshwa tu, Wazanzibar walioana sasa" janja" hii itawamaliza/ itawameza. Kama Tanganyika ilivyomezwa na Muungano.
Imeibuka sauti mpya huko, UAMSHO ambayo imejibebesha jukumu la kuwa msemaji au mpigania haki za Zanzibar. Ushahidi wa picha uliosema niutizame ni wazi kuwa UAMSHO wanakubalika huko. Lakini UAMSHO si chama cha siasa kama JF au Mwanakijiji kuwa si chama cha siasa lakini vikundi hivi vimekuwa chachu ya mjadala mpana/ wa kina juu Muungano.
Nilichotahadharisha mimi ni kuwa Mijadala iliyoibuka sasa hivi hapa JF imeanza/ imeanzishwa kwa kukurupuka ikibeba dhana kuwa UAMSHO ( waislamu wa Zanzibar) wamechoma makanisa.(Mtego wa magamba)
Hili naona ni kosa na linaondoa ladha ya mijadala yenyewe..pitia threads uone hilo. Ningependa sana tuwaunge mkono UAMSHO na wazanzibari katika kupigania haki na maslahi yao. Siku wakiridhika / wakijua kuwa haki katika Muungano inatendeka basi tutakuwa na Muungano wa Nchi, watu na jamii ambayo inafurahia matunda/ faida ya/za Muungano.
Leo watu wa Tanganyika wanaona Muungano hauna faida kwao na watu wa Zanzibar kama unavyowaona wanasema wananyonywa/ wanabinywa na kwa hiyo Muungano hauna faida kwao.
Nikukumbushie maneno ya Lissu.
Anaongeza kuwa
vurugu hizo siyo za kidini kama wanavyodhani watu wengi bali ni njia iliyotumika kufikisha ujumbe wa walalamikaji.
"Ukristo wa bara ulitokea Zanzibar. Makanisa ya kwanza Afrika Mashariki na kati yalijengwa Zanzibar karibu na soko la watumwa. Baada ya Zanzibar ndiyo yakaja, Bagamoyo na Rabai na sehemu nyingine. Si suala la kidini, ni hoja za kujishikiza tu, kuna masuala ya msingi yanayovishwa hoja za kidini."anasema Lissu.
link
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...alitarajia-kurudi-zanzibar-4.html#post4006894
Nafikiri ni vyema mijadala ya Muungano iwe mipana na ya uwazi na siyo kama hii inayoongozwa na hamasa au kuona upande mmoja ndio wenye dhima ya kuuvunja. Majadiliano ya wazi na ya kina yafikie uamuzi huo au vyenginevyo.
Sio vibaya kuwashawishi watawala kufungua mjadala rasmi wa wazi na mpana juu ya Muungano, hatima ya Muungano, Muundo wa Muungano au kugawana fito bila ya kutoboana macho au kutiana ulemavu. Hii iwe ndio chachu/ changamoto yetu. Au yafunguliwe majadiliano Rasmi katika ya pande mbili za Muungano kuujadili Muungano.(majadiliano na sio kuhojiwa staili ya Kolimba).
Ichaguliwe timu ya Tanganyika na timu ya Zanzibar zikae mkao wa kula, majadiliano ya wazi ili wananchi waelewe nini kinajadiliwa isiwe kama walivyofanya Nyerere na Karume
Lugha za kutishana, ubabe, ufedhuli au kujifanya "Sheik Yahya" /utabiri wa nini kitatokea baada ya kuvunjika Muungano hazitaendesha mjadala wa Muungano na kufikia hitimisho la nini tunakutaka juu ya muungano huu wa Kero.
Bado Muungano wa Tangayika na Zanzibar umegubikwa na usiri mkubwa(mazinagombwe/kiini macho). Tufungue Pandora box ya Muungano!