Mkuu wala sintofanya hivyo isipokuwa kwa maandishi nayoyasoma hapa. Siwezi kukuingiza kundini wakati mimi na wewe tupo pamoja ktk hili isipokuwa tofauti zetu ni ktk kuafikiana nani mbaya wa Wazanzibar.Huyu jamaa hapa anafanya haya uliyoshauri hapa. Wala huyu siye Nonda.
.... vurugu hizo siyo za kidini kama wanavyodhani watu wengi bali ni njia iliyotumika kufikisha ujumbe wa walalamikaji.
.... Si suala la kidini, ni hoja za kujishikiza tu, kuna masuala ya msingi yanayovishwa hoja za kidini."
Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...alitarajia-kurudi-zanzibar-4.html#post4006894
Mengine mengi ambayo umeyagusia katika mchango wako yana wenyewe.Unajaribu kuniingiza kundini. Ni jamaa zako.
Tafakari hayo maneno aliyosema huyo jamaa yetu.
Unajua kina Mwanakijiji ni watu wanaosoma maansiko vile vile wanatazama maandamano kama haya yanayobeba bendera zenye aya za kuran na Utaifa wa Zanzibar wakati wanashindwa kuelewa kwamba aliyewauza Wazanzibar ni hao hao wanaoongoza Zanzibar lakini lawama zote zinamfuata Nyerere kwa sababu ni mkristu kama alivyosema Nguruvi3. Na hakika hata wewe akishambuliwa JK kwa sababu ya Uislaam wake wakitumia parapanda sidhani kama utakaa kimya maana vita sasa imegeuka kuwa ya UDINI..
Siku zote napinga Udini na sioni nafasi ya Uislaam ktk unafiki huu maana ukweli unabakia kwamba sisi tumeunda UNION wala sii COMUNITY kwa mfano wa EAC na wala sii FEDERATION kwa maana ya kutambua sovereignty ya nchi husika chini ya Umoja wa kitaifa ambao unaua Identity ya nchi nje kama zilivyo States za Marekani. Tumeunda kitu kinaitwa UNION na uzito wake ni sawa na yamin ya Undugu kama kitu kimoja na hivyo kutengenishwa kwetu sii swala la mzaha hata kidogo. Hao waasisi wa muungano huu wameivunja Tanganyika na kuiacha Zanzibar ktk mfumo wa kipekee kiutawala ambao pengine umefuata WATU na MAZINGIRA yetu ambayo sii sawa na ya Uingereza wala marekani, au umejengwa kulindana au vyovyote vile, hivyo kama kuna matatizo basi haya yaorodheshwe na kutazamwa kwa undani wake maana hakua kati yetu anayejua kwa uhakika sababu na malengo ya muungano ule zaidi ya maandalizi ya Uhuru wa nchi za kiafrika.
Lakini hizi habari za kuilalamikia Bara na hasa Wakristu ilihali sisi hatuwezi kuondokana na historia ya nchi na dini zetu ambazo zote zimekuja kwa watu wasioabudu na zikaweza kushamiriu na kufuatwa leo kweli sisi Waislaam tunaacha Sunna kubwa ya mtume ktk kuitangaza dini kwa amani tunaanza kutafuta kujitenga?.. Ebu nambie kama Mtume aliweza kumwingia mtu kama Sayyidina Omar (RA) na akaweza kumshawiushi kuingia uislaam wewe leo unashindwa nini kuutangza Uislaam isipokuwa kutafuta vita ya kujitenga na hawa wakristu wakati ushenzi wote unafanyika Zanzibar ya leo.
Ni haya ndio yanayopelekea mimi hata kupinga Mahakama ya kadhi ambayo inataka tu sheria ktk mambo madogo lakini yale yanayowaondoa watu ktk Uislaam kama Ushoga, Zinaa, Kamari, riba ktk Mabenki, madawa ya kulevya, Ufisadi ktk mikopo na mengine mengi machafu yanakubalika tena mbele ya macho yao na hakuna hata Sheikh mmoja kasimama na kusema lazima tuiboreshe sheria kwanza kufuata Uislaam kabla ya kuwahukumu watu. Na hawa wenyewe ndiio wahsiriki wakubwa wa mabaya haya wakijificha nyuma ya pasia la dini kama kinga..Kama haiwezekani kuziweka sheria za kiislaam ipaswapo basi tumwachie Mungu maaana siku ya hukumu kila mmoja wetu atawajibika yeye kwa makosa yake na sii kuchagua ibada ambazo zina tu suite kwa sababu tunatafuta ULAJI..
Mwisho mkuu wangu ebu rudi tazama hiyo picha hapo juu!...Maskini hawa watu hawafahamu wanachotetea isipokuwa Uislaam wakati laani ipo ndani ya viongozi wao wenyewe. Nimesema sana na nitarudia mara 100 kidogo, kama kweli Baraza la Mapinduzi hawautaki Muungano wao wachukue dhamana ya wananchi kusimama kidete na kutaka kujitoa ktk Muungano huu wasizungumzie pembeni maanake hata Maalim Seif Hamad siku ya kuapishwa kwake alisema wazi kuunga mkono umoja wa Kitaifa na huwezi kuitenganisha CCM na bara.
Kifupi, kwa mtazamo wangu Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ni sawa kabisa na muafaka baina ya CUF na CCM kwa maana kwamba umoja huu umeundwa kwa malengo ya kiutawala zaidi kuliko maswali yanayohusiana na kuwepo kwa muungano huu - The end justify the means!