Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Nondo,
Nilikuwa sijapitia mada nyinginezo kumbe kuna mpango wa kura za maoni? sasa walikuwa wapi siku zote ilihali linawezekana pasipo ruksa kutoka bara?..Ebu msome Maalim Seif Bofya na amesema wazi kuhusu serikali ya Zanzibar na viongozi wake ktk uwakilishi wao..Hivyo ipo serikali kamili na ndio maana kawahakikishia.
Huyu Huyu Maalim aliwahi kuwa waziri kiongozi kisha waziri wa Elimu toka enzi zileee hakufanya lolote kuboresha maisha ya Wazanzibar leo anawaambia wasitie wasiwasi ilihali swala analojadili ni la katiba ya Muungano mkatoe maoni yenu na sio swala la referendum kuhusu Zanzibar kuendelea kuwa ktk muungano. Bado unataka kipi upate kuamini kuwa mdudu yuko ndani ya kokwa?
 
Mkuu Mkandara,
Ndugu yetu Nonda anajifanya haelewi au amegoma kuelewa.
Kwanza hajibu hoja na anatuletea vijarida vilivyoandikwa pengine na wananchama wa UAMSHO. Nonda, inakubidi uelewe kuwa kusoma kitu peke yake hakutoshi, kunatakiwa nawe uwe na mtazamo na fikra, upime na uchambue.
Hivi unategemea usome kijarida cha Ahmed Rajab au Ally Salehe unufaike na nini kama si ulaghai, uongo, fitna na chuki

Tumemuuliza, Rais, Mkamu wawili, SMZ, Baraza la mapinduzi, BLW, Wabunge wa Zanzibar wote hao wanakazi gani?
Hivi baraza la mapinduzi linajukumu la kuandaa baraza la Idd tu ?

Amekiri kuwa kuvunja muungano kunahitaji bunge la muungano! kwa maneno mengine anatambua kuwa katiba ya JMT ni juu ya katiba zote. Anapojichanganya ni pale anaposhindwa kuelewa kuwa BLW lina nguvu kubwa kuliko Bunge la JMT.
Nguvu hizo ni za kisheria na ubabe. Ni BLW limepitisha mambo mengi sana yanayoigusa katiba ya JMT bila kuguswa. Hata vifungu vingine katika katiba ya JMT ni useless lutokana na ubabe wa BLW

Nonda, amegoma kutambua kuwa Zanzibar ina Rais, makamu wawili ambao kazi yao ni kuendesha SMZ.
SMZ haiwezi kuamua kuhusu muungano lakini inaweza kuamua kuhusu kura ya maoni ya GNU, ni kituko kama si kichekesho.

Labda amesahau kuwa Zanzibar ina wimbo wa taifa, bendera n.k walivyovidai kama silaha ya kuweza kufanya maamuzi.
Kama hawawezi kuitisha kura ya maoni tofauti ya kisiwa cha ukerewe, mafia na Zanzibar ni nini?

Nonda anakiri kuwa viongozi wa Zanzibar ni 'mamluki' lakini hasemi ni makafir hata kama wanatumikia makafir.
Kwa mantiki hiyo tatizo lao ni umoja wa kudai nchi yao, kwa bahati mbaya wamekabidhi hoja kwa UAMSHO na wenzetu hawa wanachojua ni kiberiti na mafuta. Ningewaelewa UAMSHO kama wangewabana viongozi kwa haya

1. Wamlazimishe makamu wa Rais wa JMT ajiuzulu na wasikubali Mzanzibar mwingine kuchukua nafasi hiyo
2. Wawakataze wabunge( wameshafika Dodoma) kutokwenda katika bunge
3. Wshinikize baraza la mapinduzi lifanye kazi iliyokusudiwa ya mapinduzi ya mzanzibar
4. Washinikize BLW liite kikao cha dharura kuhusu muungano na muafaka ufikiwe hapo hapo

Njia zote hizo hazitahusu FFU kwasbabu hakuna sababu ya FFU kushambulia vyombo halali vinavyokaa kwa masilahi ya Zanzibar. Kuchoma makanisa ni akili ya chini sana na hakika mtu ajisikie aibu kutetea au kuwa mwana UAMSHO!

Mkandara, wanachotaka ni bunge la muungano lijadili kwasababu hapo kutakuwa na muafaka wa mambo 2 wanayotaka
1. Serikali 3
2. Mkataba

Kwa hili Nonda hatutakubali hata kwa bahati mbaya. Sisi tumeridhia Zanzibar ijifanyie mambo yake kama inavyojifanyia sasa. Kama watasubiri bunge la muungano basi wakae kimya kwasababu hawana sababu za maana zaidi ya kelele.
Huwezi kulikashifu na kukiuka katiba ya JMT halafu leo useme unataka katiba hiyo hiypo ikutendee haki!

Mkandara, somo lako la USA, Quebec ni mwanana lakini lazima msomaji aipe akili nafasi ya kuelewa.
Mtu akigoma kuelewa hatakuelewa.
Quebec ni mfano mzuri sana wa mazingira tunayokabiliana nayo.
 
Nondo,
Nilikuwa sijapitia mada nyinginezo kumbe kuna mpango wa kura za maoni? sasa walikuwa wapi siku zote ilihali linawezekana pasipo ruksa kutoka bara?..Ebu msome Maalim Seif Bofya na amesema wazi kuhusu serikali ya Zanzibar na viongozi wake ktk uwakilishi wao..Hivyo ipo serikali kamili na ndio maana kawahakikishia.
Huyu Huyu Maalim aliwahi kuwa waziri kiongozi kisha waziri wa Elimu toka enzi zileee hakufanya lolote kuboresha maisha ya Wazanzibar leo anawaambia wasitie wasiwasi ilihali swala analojadili ni la katiba ya Muungano mkatoe maoni yenu na sio swala la referendum kuhusu Zanzibar kuendelea kuwa ktk muungano. Bado unataka kipi upate kuamini kuwa mdudu yuko ndani ya kokwa?
Mkuu Mkandara, nimeisoma hotuba ya maalim Seif. Amejaribu sana kuwatahadharisha Wazanzibar kuwa muungano bado wanautaka na muhimu.

Amejaribu pia kuonyesha kuwa Watanganyika hawataki serikali 3.
Akaingiza hoja ya kuwa kuwepo serikali mbili, ya Tanganyika na ya Zanzibar halafu uwepo mkataba.
Hiki ndicho tunachopinga kila siku, mkataba utamnufaisha Mtanganyika kwa jambo gani?
Anajua bajeti ya Ulinzi na Elimu tu zinatosha kuwa mzigo, anajua uwekezaji na soko la ajira, anajua ardhi na soko la bidhaa ni kikwazo kwao. Hakuna hata kimoja kitakachomnufaisha Mtanganyika.

Katika kujenga hoja ya mkataba, Maalim akanyunyuzia kuwa tunaweza kuwa na muungano kama wa EU au EAC. Hiki ni kichekesho sana kwa kiongozi wa ngazi ya Seif kwasababu kama kila mmoja takuwa na mamlaka yake kamili kwanini tusikutane huko EAC tukajenga umoja wenye nguvu. Ni kwanini tuwe na ka'EAC' ka vinchi viwili halafu tukaenda EAC kubwa?

Lakini pia maalimu seifu katusaidia kuweka wazi kuwa Zanzibar ina serikali yenye mamlaka na viongozi kindaki ndaki. Watalinda masilahi ya Zanzibar kwa gharama zozote. Ni hapa ndipo tunasema kwanini wasiwasikilize wana UAMSHO na kulinda masilahi kwa kuvunja muungano?

Hii ni kutapa tapa kwa kujua kuwa kuvunja muungano ndio mwisho wa uhusiano na itakula Zanzibar vibaya sana.
Watanganyika, nawasihi ndugu zangu, hawa watu wanachuki za dhati kutoka mioyoni mwao dhidi yetu. Hatutaki kusikia tena kuna mtu kachomwa moto kwasababu hulka ya mwanadamu hujinasibu ikipata fursa.

Kama kuna kosa Tanganyika itafanya ni kuwa na ushirikiano na Zanzibar kwa namna yoyote ile.
Tutaendelea kulea donda kwa miongo mingine kwa ujira wa moto, matusi na Kejeli.
Ni wakati sasa hawa watu tuachane nao, kwasababu amani na chuki havikai mahali pamoja.

LET ZANZIBAR GO! PACK AND GO ASAP
 
Nguruvi3 said:
Katika kujenga hoja ya mkataba, Maalim akanyunyuzia kuwa tunaweza kuwa na muungano kama wa EU au EAC. Hiki ni kichekesho sana kwa kiongozi wa ngazi ya Seif kwasababu kama kila mmoja takuwa na mamlaka yake kamili kwanini tusikutane huko EAC tukajenga umoja wenye nguvu. Ni kwanini tuwe na ka'EAC' ka vinchi viwili halafu tukaenda EAC kubwa?

Nguruvi3,

..asante sana X 2 kwa mchango wako.

..hata mimi hii habari ya "muungano wa ki-mkataba" inaniacha na maswali mengi sana.

..wa-Zanzibari wanajua nini wanachokitaka, sasa kuna kitu gani kwenye huo "mkataba" mpya wanaoupendekeza??

..kama ulivyoeleza wewe, kuna ulazima gani wa kuwa na mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar? Kwanini tusiende moja kwa moja kwenye EAC ???

NB:

..napendekeza hii hoja ya "muungano wa ki-mkataba" iundiwe thread yake maalum. kwa maoni yangu hiyo ni HILA ya kutaka kuendelea kuinyonya Tanganyika.
 
Muungano wa kila siku ni manung'uniko kutoka kwa Wazanzibar ni kero kubwa hata kwa Watanganyika. Wazanzibari wamefikia kiwango ambacho kinafanana na yaliyompata Najib Balala ambaye alikuwa Waziri wa Utalii Kenya kutoka ODM. Balala aliendekeza tabia ya kuomba talaka kwa Waziri Mkuu Raila Odinga mara kwa mara kwa kuendekeza kumchokoza bosi wake mpaka alipomfukuza kwenye baraza la Mawaziri.
 
Nguruvi3,

..asante sana X 2 kwa mchango wako.

..hata mimi hii habari ya "muungano wa ki-mkataba" inaniacha na maswali mengi sana.

..wa-Zanzibari wanajua nini wanachokitaka, sasa kuna kitu gani kwenye huo "mkataba" mpya wanaoupendekeza??

..kama ulivyoeleza wewe, kuna ulazima gani wa kuwa na mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar? Kwanini tusiende moja kwa moja kwenye EAC ???

NB:..napendekeza hii hoja ya "muungano wa ki-mkataba" iundiwe thread yake maalum. kwa maoni yangu hiyo ni HILA ya kutaka kuendelea kuinyonya Tanganyika.
Unajua Mkuu Jokakuu, ile hoja ya serikali 3 imekufa baada ya swali la je, itaendeshwa kwa gharama zipi, nani atalipa na asipolipa iweje. Wazanzibar wakawa hawana jibu la maana kwakujua kuwa serikali 3 ni utegemezi na mzigo kwa mtanganyika.

Ukiangalia katika mambo 11 ya muungano na hata yalipoongezwa hadi 22, asilimia 97 yanaisaidia Zanzibar.
Suala kama elimu ya juu halipo katika 11 lakini wanafaidi kwa gharma.

Leo kuna waziri wao kasema wanasaka watu wenye vitambulisho haramu vya ukaazi Zanzibar.
Eti wanachukua ajira za wazanzibar. Ukichunguza hapa anayetafutwa ni Mtanganyika, siyo Mhindi, Mwarabu Mkenya au Mwitaliano.

Wao wamesahau kuwa wapo bara na hakuna anayeuliza ajira zao. Ukigusa tu ajira watalalmika kuwa ni suala la muungano.

Maana yake ni kuwa wanataka chao kiwe chao, chetu kiwe chao! Hili suala la mkataba hakuna anayeeleza mkataba huo uwe ni wa nini, si Maalim Seif na UAMSHO, si Ahmed Rajab, Si Ally Salehe au mwingine awaye.None!

Nadhani wazo lako la kuchunguza nini maana ya makataba na nini kiwepo ndani ya mkataba ni muhimu sana.
Hawa wanataka muungano lakini muungano wa kuwasaidia wao na si Tanzania.

Sasa wamekuja na uhusiano wa EAC,kama ni hivyo kwanini tusiwe kama Burundi, Rwanda na Kenya katika EAC?
Kwanini tuwe na kauhusiano pembeni na halafu twende EAC vipande vipande.

Swali ni kuwa huu uhusiano na mkataba ni wa kuhusu mambo gani?
 
Unajua Mkuu Jokakuu, ile hoja ya serikali 3 imekufa baada ya swali la je, itaendeshwa kwa gharama zipi, nani atalipa na asipolipa iweje. Wazanzibar wakawa hawana jibu la maana kwakujua kuwa serikali 3 ni utegemezi na mzigo kwa mtanganyika.

Ukiangalia katika mambo 11 ya muungano na hata yalipoongezwa hadi 22, asilimia 97 yanaisaidia Zanzibar.
Suala kama elimu ya juu halipo katika 11 lakini wanafaidi kwa gharma.

Leo kuna waziri wao kasema wanasaka watu wenye vitambulisho haramu vya ukaazi Zanzibar.
Eti wanachukua ajira za wazanzibar. Ukichunguza hapa anayetafutwa ni Mtanganyika, siyo Mhindi, Mwarabu Mkenya au Mwitaliano.

Wao wamesahau kuwa wapo bara na hakuna anayeuliza ajira zao. Ukigusa tu ajira watalalmika kuwa ni suala la muungano.

Maana yake ni kuwa wanataka chao kiwe chao, chetu kiwE chao! Hili suala la mkataba hakuna anayeeleza mkataba huo uwe ni wa nini, si Maalim Seif na UAMSHO, si Ahmed Rajab wa Raia mwema, Si Ally Salehe wa BBC au vuvuzela mwingine awaye.None!

Nadhani wazo lako la kuchunguza nini maana ya makataba na nini kiwepo ndani ya mkataba ni muhimu sana.
Hawa wanataka muungano lakini muungano wa kuwasaidia wao na si Tanzania.

Sasa wamekuja na uhusiano wa EAC,kama ni hivyo kwanini tusiwe kama Burundi, Rwanda na Kenya katika EAC?
Kwanini tuwe na kauhusiano pembeni na halafu twende EAC vipande vipande.

Swali ni kuwa huu uhusiano na mkataba ni wa kuhusu mambo gani?
Nguruvi3, chokochoko za muungano zilikuwa na nguvu ya wakubwa wengi. Na tangu mwanzo sikuamini kama wanataka kujitenga, ila walitaka kurasimisha Tanganyika iwe 'cash cow'. Na kama umefuatilia baada ya Tanganyika kuanza kusema go go go kelele zinapunguwa (walau kwa wakubwa).

Mtu wa kawaida kwenye mitaa ya Zanzibar anaweza asilitambue hili la wakubwa kushikwa na butwaa maana wako kwenye catch 22! Kauli ya Maalim Seif kwamba 'hatutawaangusha' is rather telling. Anaanza kuona ngoma sio rahisi kama alivyokuwa anahubiri, na kuna kipindi alikuwa anasema lazima Zanzibar iwe na sarafu yake!

Bunge la Muungano ndio limeenza, lets wait and see kama kuna watu wamepewa maagizo!
 
Last edited by a moderator:
Jana nimesikia BLW wakisema wanataka mgao wa 4.5 uongozwe hadi 11%. Wanasema sasa hivi wanapata mgao wa 7% kutoka hazina Dar ambayo ni Hazina ya Muungano a.k.a Tanganyika.
Hawajasema wao wanachangia nini katika hilo pato la taifa ili wadai zaidi au hata kupata tu!

BLW wanadai wapewe fungu la elimu ya juu kutoka hazina ya muungano. Hapa ndipo nasema Wazanzibar ni wanafiki sana. Siku zote wanasema Tanganyika imeongeza MAMBO 11 ya muungano hadi kufikia 22. Wanasahau kuwa elimu ya juu haikuwa suala la muungano, lakini wanapotaka pesa za elimu ya juu wanasema ni haki yao!

Hakuna hata mmoja aliyesimama na kusema hataki muungano, sasa hapa ndipo nachanganyikiwa wale wazanzibar 'wengi' wanawakilishwa na nani? UAMSHO au BLW , na je BLW ni vibaraka na wasaliti kama viongozi wa muungano kutoka Zanzibar?
 
Jana nimesikia BLW wakisema wanataka mgao wa 4.5 uongozwe hadi 11%. Wanasema sasa hivi wanapata mgao wa 7% kutoka hazina Dar ambayo ni Hazina ya Muungano a.k.a Tanganyika.
Hawajasema wao wanachangia nini katika hilo pato la taifa ili wadai zaidi au hata kupata tu!

BLW wanadai wapewe fungu la elimu ya juu kutoka hazina ya muungano. Hapa ndipo nasema Wazanzibar ni wanafiki sana. Siku zote wanasema Tanganyika imeongeza MAMBO 11 ya muungano hadi kufikia 22. Wanasahau kuwa elimu ya juu haikuwa suala la muungano, lakini wanapotaka pesa za elimu ya juu wanasema ni haki yao!

Hakuna hata mmoja aliyesimama na kusema hataki muungano, sasa hapa ndipo nachangyika wale wazanzibar 'wengi' wanawakilishwa na nani? UAMSHO au BLW , na je BLW ni vibaraka na wasaliti kama viongozi wa muungano kutoka Zanzibar?

Siyo tu Elimu, baadhi ya wajumbe wa BLM wanataka kila kitu/idara iliyo chini ya muungano iwe pasu-pasu in terms of nafasi za kazi. As usual hawajasema wanachangia kiasi gani kuendesha hizo wizara/idara mfano wizara ya ulinzi, au wizara ya mambo ya ndani! For 48 years Tanganyika imekuwa inabeba mzigo wa kuhudumia wizara zote za muungano.
 
Nguruvi3, chokochoko za muungano zilikuwa na nguvu ya wakubwa wengi. Na tangu mwanzo sikuamini kama wanataka kujitenga, ila walitaka kurasimisha Tanganyika iwe 'cash cow'. Na kama umefuatilia baada ya Tanganyika kuanza kusema go go go kelele zinapunguwa (walau kwa wakubwa).

Mtu wa kawaida kwenye mitaa ya Zanzibar anaweza asilitambue hili la wakubwa kushikwa na butwaa maana wako kwenye catch 22! Kauli ya Maalim Seif kwamba 'hatutawaangusha' is rather telling. Anaanza kuona ngoma sio rahisi kama alivyokuwa anahubiri, na kuna kipindi alikuwa anasema lazima Zanzibar iwe na sarafu yake!

Bunge la Muungano ndio limeenza, lets wait and see kama kuna watu wamepewa maagizo!

Ha ha ha...naona chibuku inafanya kazi yake kichwani. Endeleeni kujifurahisha na ndoto za mchana. Zanzibar, ilikuwapo kabla ya Muungano na itaendelea baada ya Muungano. Msijipe U-MASTER wakati nyinyi wenyewe hamna mbele wala nyuma. I LIKE THAT " LET ZANZIBAR GO " , I HOPE THAT IT IS TRULY FROM YOUR HEART.
 
Nakupenda TANGANYIKA nakusubiri kwa hamu sana. tunaweza kudelay lakini si kuzuia
 
Ha ha ha...naona chibuku inafanya kazi yake kichwani. Endeleeni kujifurahisha na ndoto za mchana. Zanzibar, ilikuwapo kabla ya Muungano na itaendelea baada ya Muungano. Msijipe U-MASTER wakati nyinyi wenyewe hamna mbele wala nyuma. I LIKE THAT " LET ZANZIBAR GO " , I HOPE THAT IT IS TRULY FROM YOUR HEART.

takashi, kwanini hawapeleki muswada wa kuvunja. Kulalamika ni kupoteza nguvu. Muswada uweke mambo yaishe, hakuna cha u-master wala mjakazi.
 
jana nimesikia blw wakisema wanataka mgao wa 4.5 uongozwe hadi 11%. Wanasema sasa hivi wanapata mgao wa 7% kutoka hazina dar ambayo ni hazina ya muungano a.k.a tanganyika.
Hawajasema wao wanachangia nini katika hilo pato la taifa ili wadai zaidi au hata kupata tu!

Blw wanadai wapewe fungu la elimu ya juu kutoka hazina ya muungano. Hapa ndipo nasema wazanzibar ni wanafiki sana. Siku zote wanasema tanganyika imeongeza mambo 11 ya muungano hadi kufikia 22. Wanasahau kuwa elimu ya juu haikuwa suala la muungano, lakini wanapotaka pesa za elimu ya juu wanasema ni haki yao!

Hakuna hata mmoja aliyesimama na kusema hataki muungano, sasa hapa ndipo nachangyika wale wazanzibar 'wengi' wanawakilishwa na nani? Uamsho au blw , na je blw ni vibaraka na wasaliti kama viongozi wa muungano kutoka zanzibar?

hivi hawa jamaa wao wanajiona wana haki ya kulishwa bure, kupewa umeme bureeee, ubwabwa bureee , kwani wao nani lakini, halafu wanakesha wakitupigia makelele na kutuchomea makanisa. Hebu huu muungano uvunjike wabaki na urojo na karafuu zao ambazo ndio rasilimali kubwa waliyonayo,
 
Jamani mnajua kuwa kuna wazanzibar wa Oman na Bara (waluguru, wasambaa, wabondei, wazaramo nk) sasa mnaposema muwape kisiwa ni chao? au cha nani Mikataba ya Carl Peter na Mangungu ipo wapi
Huyu mwarabu anataka na kilometa 20 kuja bara toka Pwani. Mm nakubali wote waarabu warudi Arabuni na hicho kisiwa tuwape wazawa km wapo (wakwezi na wakulima waliokuweoo kabla ya mwarabu na Mjerumani
 
Siyo tu Elimu, baadhi ya wajumbe wa BLM wanataka kila kitu/idara iliyo chini ya muungano iwe pasu-pasu in terms of nafasi za kazi. As usual hawajasema wanachangia kiasi gani kuendesha hizo wizara/idara mfano wizara ya ulinzi, au wizara ya mambo ya ndani! For 48 years Tanganyika imekuwa inabeba mzigo wa kuhudumia wizara zote za muungano.
Ukweli ni kwamba wanachangia 0 lakini wanadai asiliamia za mgao wapato la taifa !!!
Hawajui bajeti ya ulinzi, mambo ya ndani wala elimu.
Kinachoshangaza si wana wizara ya elimu, baraza la mitihani na chuo kikuu zote zikiwa chini ya SMZ.
Hili la elimu ya juu si sehemu ya muungano kama ilivyo mafuta, sasa wanataka pesa za nini hawa jamaa zetu?

Kwa wale msioelewa maana ya serikali 3, mkataba au mahusiano maalumu hii ndiyo maana yake. Kwamba, penye ugumu kuna muungano mafuta aah a! hayo si muungano. Unafiki, uchoyo, ubinafsi ni vitu vibaya sana kwa mwanadamu.

Sisi Tanganyika tunasema LET ZANZIBAR GO, sasa wao wanasuasa sua nini.
Hakuna kitu kero sasa hivi, tumeamua kuachana nao waende kwa amani.
 
Kwa kuongezea, mikopo inachukuliwa kama Tanzania, Zanzibar wanapata share yake lakini ikija kulipa deni ni Tanganyika tu ndio wanalipa.
 
Back
Top Bottom