Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

Barubaru, nakiri kuwa umerudia rudia sana maneno yale yale isipokuwa hujajibu swali la msingi (na ndio hoja ya Mzee Mwanakijiji): iweje BLW liweze kutunga sheria zinazovunja katiba ya JMT lakini lishindwe kujitoa kwenye muungano? Kama Wanzibari hawaridhiki na muungano wanashindwa nini kujitoa ukitilia maanani kuwa muungano wenyewe hauna nguvu ya kisheria (kwa mujibu wa madai kuwa the union articles were never ratified by any competent authority in Zanzibar)?

Na hata mkataba wa muungano ungekuwa halali kisheria, ina maana hauwezi kuvunjwa? Mkataba unatakiwa ama kubadilishwa au kuvunjwa endapo kuna upande usioridhika iwe na kipengele kimoja au zaidi ndani ya mkataba, na initiator ni yule asieridhika!
Mtoboasiri
Ukipindua hii hoja yako.
Je Bara/Tanganyika inaridhika na muungano?
Kama hairidhiki na Muungano huu kwa nini hatutaki kuuvunja?
Wabara/watanganyika 40 milioni tunasubiri watu laki 9.5 wauvunje ?
Je muungano una maslahi kwa watanganyika? Kama hauna kwa nini hatuchukui hatua kuuvunja?

Kuhusu katiba ya Zanzibar, nafikiri wengi hata mwanasheria kama Lissu anashindwa kuelewa.
Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar zina uzito sawa. Kila moja inajitosheleza. Kila katiba ina mamlaka yake na mipaka yake. Kwa kukosekana katiba ya Tanganyika ndio mambo yote yanakuwa hayaeleweki.
Kiufupi, Tanzania ina mamlaka tatu kisheria, mamlaka ya mambo ya Bara(Tanganyika), mambo ambayo si ya muungano. Kuna mamlaka ya mambo ya Zanzibar, mambo ambayo si ya muungano na kuna mamlaka ya mambo ya muungano, mambo ya pamoja ya Tanganyika na Zanzibar(mambo ya muungano). Kila katiba hapo inajitosheleza.

Imeshasemwa sana hapa kuwa wanaonufaika na Muungano ni viongozi wa pande mbili za muungano ambao ni chini ya 1%. Wananchi wa Tanganyika na wananchi wa Zanzibar wanafanywa mhanga tu wa viongozi kugawana keki ya Taifa.Watanzania wanagawiwa umaskini tu.
Wananchi wa Zanzibar ambao hawana uwezo wa kutamka kisheria kuwa wanauvunja Muungano wanapiga mayowe, wanapiga kelele kuwa wameshachoshwa na mazingaombwe ya Muungano.Na hakuna ambaye hajasikia kelele hizo.

Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mkandara, Nonda wanajitahidi kutuamsha(kutoa UAMSHO) kwa sisi wabara/wadanganyika tuamke kama wenzetu wa Zanzibar ili tumfunge paka kengele, tuondokane na mazingaombwe ya muungano. Lakini wadanganyika bado tunapiga usingizi, usingizi mnono.usingizi fofofo.

Tunajisifia tuna madini, gesi, almasi,mafuta lakini shule zetu,shule za kata na walimu fasta fasta, nyumba za nyasi na kuishi "kimjini"(ubabaishaji na ulaghai). Utajiri wetu umetusaidia nini? Sisi ni maskini, fukara kiasi ambacho tunapohongwa kofia na fulana wakati wa kampeni hujiridhisha kuwa mungu ametukumbuka.

Watanganyika tupige kelele kuwa muungano unatunyonya ili wabunge wetu nao waanze kupiga kelele bungeni kama Raza. Huenda viongozi wa Serikali waliotia pamba masikioni, kama kelele hizo zitakuwa kali, masikio yatazibuka.

Kwa nini haibukii G55 nyingine? Ili kuibuka G110 inabidi sisi wadanganyika tuanze kupiga mayowe ,kama kupiga kelele hatuwezi...anyway, mtu aliyelala hawezi kupiga kelele, tuamke kwanza!

Tudai Tanganyika yetu and this mess will sort itself out!
 
....
Katika mambo 11 yaliyoongezwa kufikia 22 ni lipi au yapi unadhani yameongezwa na yanaiumiza Zanzibar.
Nina maana ni yapi ya hila za kuihujumu Zanzibar
....

The initial “Union Matters” included the following eleven
areas as Union matters:

·
The constitution and government of the United
Republic;

· External affairs;

· Defense;

· Police;

· Emergency powers;

· Citizenship;

· Immigration;

· External trade and borrowing;

· The Public service of the United Republic;

· Income tax, corporation tax, customs and excise duties,

and

· Harbours, civil aviation, posts and telegraph.

Between 1964-1977
: through an amendment of the Interim
Constitution which had reproduced the list of union matters and not

an amendment of Acts of Union, new items were added to the list of

Union matters giving the Union parliament and executive more

powers.

ADDITIONAL ARTICLES OF UNION
Other issues added to the list to make the Union matters
22 were
:· All matters concern coinage, currency for the
purposes of legal tender (including notes), banks

(including savings banks) and all banking business;

foreign exchange and exchange control

·
Industrial licensing and statistics
·
Higher education
·
Mineral oil resources, including crude oil and natural
gas

·
The National Examinations Council of Tanzania and
all matters connected with the functions of that

Council

·
Civil Aviation
·
Research
·
Meteorology
·
Statistics
·
The Court of Appeal of the United Republic
·
Registration of political parties and other matters
related to political parties

This watermark does not appear in the registered version -
http://www.clicktoconvert.com
·
Zanzibar retains jurisdiction over issues which
include:

·
Information, Agriculture, Natural Resources,
Environment and Cooperatives, Trade, Industry,

Marketing, Tourism, Education, Culture and Sports,

Health and Social Welfare, Water, Construction,

Energy and Land, Communication and Transport and

finally, youth, employment, women and children

development, etc

Salaam Bar baru
Nimekusoma hapo juu lakini bado hujajibu swali kwa maana ya kutaja tu haitoshi, je ni kwa vipi yanaiumiza Znz.
Labda nichukue mawili tu tuliangalie katika yale 11 yaliyoongezwa.
1. Elimu ya juu 2. National exam council. Tutolee ufafanuzi wa haya ili nasi tuelewe dhulma inayotendeka
 
Hilo Baraza la mate wangu Joyce lina tuhuma nyingi sana na nyingine lenyewe limekiri kuwa ni sahihi.
Mfano. Mwaka huu ilizoeleka wanafunzi wanaofanya mtihani wa Islamic Knowledge walikuwa wanafanya paper 3. Lakin mwaka huu ilibadilishwa na kufanya paper 2 Tu. Mama huyu chini ya uongozi wake na watu wa IT wakafanya kwa makusudi kabisa kutoondoa ile formula waliokuwa wakiitumia yya kugawanya kwa 3. Na hivyo kufelisha zaidi ya 70% ya waliofanya mtihani huo ambao zaidi ya 90% ni wanatoka Zanzibar,

Hilo nafikiri walirekebisha na baraza hilo Kuomba Radhi.

Lakin vile vile baraza hilo halina sura ya Muungano. Tokea kuanzishwa kwake wenyeviti wa baraza hilo wote ni wakristo. Na vile vile Makatibu na manaibu katibu wa baraza hilo toka linaanzishwa ni wakristo na wote wanatoka Bara.
Kumbuka kuwa baraza la mitihani ndio kigezo cha uchaguzi wa vilana wanaokwenda Chuo kikuu au Vyuo vingine vya elimu ya Juu. sasa pakiwa na hujuma hapo basi hata ilmu ya juu inakuwa mashaka makubwa sana.

Binafsi nafikiri hili lingeachiwa kila nchi iwe na baraza lake na Mitihani na hata Bodi yake ya mikopo ya Ilmu ya juu . Kwani kwa kufanya hivyo kutatoa fursa watu hawa kurejesha mikopo hiyo kwa nchi zao husika. Isije ikawa kama Kodi wanazolipa mashirika enye sura ya Muungano kama TTCL, Posta ,TRA, makampuni yote ya simu n.k ambapo wanalipa kodi za Tanganyika na Znz hainufaiki na kuwepo kwake huko Visiwani.

Kuna mengi sana nakumbuka nilichambua kwa kina sana kwenye mada ya NINI FAIDA YA MUUNGANO KWA ZNZ/TANGANYIKA. na nlibainisha mengi sana kwako na Ahali yetu Mkandara.

Ijumaa l'karim

Mtoboasiri
Ukipindua hii hoja yako.
Je Bara/Tanganyika inaridhika na muungano?
Kama hairidhiki na Muungano huu kwa nini hatutaki kuuvunja?
Wabara/watanganyika 40 milioni tunasubiri watu laki 9.5 wauvunje ?
Je muungano una maslahi kwa watanganyika? Kama hauna kwa nini hatuchukui hatua kuuvunja?

Kuhusu katiba ya Zanzibar, nafikiri wengi hata mwanasheria kama Lissu anashindwa kuelewa.
Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar zina uzito sawa. Kila moja inajitosheleza. Kila katiba ina mamlaka yake na mipaka yake. Kwa kukosekana katiba ya Tanganyika ndio mambo yote yanakuwa hayaeleweki.
Kiufupi, Tanzania ina mamlaka tatu kisheria, mamlaka ya mambo ya Bara(Tanganyika), mambo ambayo si ya muungano. Kuna mamlaka ya mambo ya Zanzibar, mambo ambayo si ya muungano na kuna mamlaka ya mambo ya muungano, mambo ya pamoja ya Tanganyika na Zanzibar(mambo ya muungano). Kila katiba hapo inajitosheleza.

Imeshasemwa sana hapa kuwa wanaonufaika na Muungano ni viongozi wa pande mbili za muungano ambao ni chini ya 1%. Wananchi wa Tanganyika na wananchi wa Zanzibar wanafanywa mhanga tu wa viongozi kugawana keki ya Taifa.Watanzania wanagawiwa umaskini tu.
Wananchi wa Zanzibar ambao hawana uwezo wa kutamka kisheria kuwa wanauvunja Muungano wanapiga mayowe, wanapiga kelele kuwa wameshachoshwa na mazingaombwe ya Muungano.Na hakuna ambaye hajasikia kelele hizo.

Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mkandara, Nonda wanajitahidi kutuamsha(kutoa UAMSHO) kwa sisi wabara/wadanganyika tuamke kama wenzetu wa Zanzibar ili tumfunge paka kengele, tuondokane na mazingaombwe ya muungano. Lakini wadanganyika bado tunapiga usingizi, usingizi mnono.usingizi fofofo.

Tunajisifia tuna madini, gesi, almasi,mafuta lakini shule zetu,shule za kata na walimu fasta fasta, nyumba za nyasi na kuishi "kimjini"(ubabaishaji na ulaghai). Utajiri wetu umetusaidia nini? Sisi ni maskini, fukara kiasi ambacho tunapohongwa kofia na fulana wakati wa kampeni hujiridhisha kuwa mungu ametukumbuka.

Watanganyika tupige kelele kuwa muungano unatunyonya ili wabunge wetu nao waanze kupiga kelele bungeni kama Raza. Huenda viongozi wa Serikali waliotia pamba masikioni, kama kelele hizo zitakuwa kali, masikio yatazibuka.

Kwa nini haibukii G55 nyingine? Ili kuibuka G110 inabidi sisi wadanganyika tuanze kupiga mayowe ,kama kupiga kelele hatuwezi...anyway, mtu aliyelala hawezi kupiga kelele, tuamke kwanza!

Tudai Tanganyika yetu and this mess will sort itself out!

Raisi kahongwa suti, naye akaona watanzania ni wa kuhongwa tu nguo, labda na vijisenti kidogo.....
 
Baru baru,
bado unakwepa hoja muhimu. Nimeuliza katika mambo ya muungano 11 yaliyoongezwa Elimu ya juu ni mojawapo. Hilo limeiumizaje Zanzibar? Hili ndilo basic question.

Umejibu hoja kwa kuzunguka lakini mimi nitakwenda moja kwa moja. Unaposema baraza halina sura ya muungano kwasababu lina wakristo nadhani hiyo ni dhana potofu sana, ni dhana inayosikitisha. Hivi mkuu wa NECTA akiwa wa dini fulani inasaidiaje? Lakini kumbuka katika madai ya mitihani Kighoma malima R.I.P anatajwa sana.
Ikumbukwe kuwa mkurugenzi huteuliwa kwa mapendekezo ya waziri, sijui kama hili hakuliona.

Kuhusu kufelishwa nakubaliana kuwa kama yapo makosa wahusika wawajibishwe, lakini najiuliza Islamic knowledge haipo katika masomo yanayompa mwanafunzi nafasi katika elimu ya juu. Sasa kwanini wafelishe Islamic knowledge na si Physics, history au Biology!

Unachosahau hapa ni kuwa unataka maziwa bila kujua ng'ombe analishwa vipi. Ni lazima uangalie maandalizi ya wanafunzi kwa ujumla. Wilayani Kilwa kuna shule imefungwa kwasababu wanafunzi wamekimbia wenyewe(hakuna wanafunzi) sasa miaka 10 au 20 down the road unategemea kuwa na Mwalimu, Engineer au Dokta kutoka eneo hilo. Katika miaka hiyo ijayo si hadithi ya kuonewa itaendelea!

Kuhusu kila nchi kuwa na baraza lake, hii italeta mtafaruku sana. Wanafunzi wa ZNZ ambao ndio kwanza watatahiniwa na baraza lao itabidi wafanyiwe mtihani ili kuona kama wanakidhi sifa za NECTA kujiunga na elimu ya juu bara ili kupta haki kwa wote. Hatujui na hakuna ajuaye hilo baraza la ZNZ lina tahini vipi na kwa sifa zipi.
Hili pia litaondoa sifa ya wanafunzi wa ZNZ kupewa upendeleo maalumu na pengine kuwafanya walipe kama wanafunzi wa nchi zingine. Ni suala la muda tu utasikia kilio!

Kuhusu bodi ya mikopo hilo ZNZ wanaweza kuanzisha tu hawahitaji ruhusa. Majuzi kuna mwakilishi ametaka wapewe hela za buree kwa elimu ya juu! haa! Wao wanachotaka ni kupewa tu ukiuliza wanachangia nini katika muungano jibu ni zero.

Unaposema kuna makusanyo ya TTC, Posta n.k unashindwa kuelewa kuwa katika mikopo ZNZ hailipi hata senti tano,hilo ni jukumu la Mtanganyika. Lakini pia lazima uelewe kuwa huduma hizo ni pesa za Tanganyika kwasababu kuendeshwa kwake ni kodi za Tanganyika.

Sidhani kuna taabu kuanzisha shirika la Posta ZNZ. Unakumbuka Zantel walikuja wakasema wao ni ZNZ, kwa taarifa yako wamehamia bara tena kwa kusaidiwa na SMZ kuwa hi sehemu ya muungano. Soko la ZNZ ni dogo sana baru baru, kwa kila hali mwenye akili timamu anaangalia mbali na hapo.

Yote hayo yasikusumbusue tuanchokiata ni wewe utujibu kuhusu elimu ya juu kama nilivyouliza hapo juu.
 
Baru baru,
bado unakwepa hoja muhimu. Nimeuliza katika mambo ya muungano 11 yaliyoongezwa Elimu ya juu ni mojawapo. Hilo limeiumizaje Zanzibar? Hili ndilo basic question.
Mkuu Nguruvi3

Hili swali mbona wewe na pacha wako,M.Mwanakijiji mlishalitolea jibu.

iii)Tuwape vijana wetu waliokosa ajira nafasi zao zilizochukuliwa na Wazanzibar
Tunawaambia kuwa wakiwa maofisini wamekaa na Wbar wakumbuke kuwa wao ni makafir mbele ya Mzanzibar. Kwamba nafasi ya Mzanzibar ni ya vijana wao....

Njia ya kwanza na nyepesi .....watendaji wote wa Muungano wenye asili ya Zanzibar kuachia nafasi zao mara moja na kurudi Zanzibar!

Hii ni pamoja na majaji, wabunge, mawaziri, maafisa wa polisi na vyombo vingine vya usalama, na wantedaji wengine ambao wako kwenye Muungano.....waanzishe mihadhara ya kuwataka Wazanzibari wenzao ambao wanatumikia Muungano waachilie nafasi hizo.

Sasa hawa wote wakikubali kuondoka kwenye nafasi zao za Muungano Zanzibar itapata wataalamu wengine wengi ambao wamekuwa wakitumikia Muungano na hivyo kujiongezea hazina ya wataalamu mbalimbali. Lakini pia itafungua ajira za Watanganyika wengi ambao wangeweza kushika nafasi zinazoshikiliwa na Wazanzibari hasa kwa vile Wazanzibari hao wako kimya na hawajitokezi kuutetea Muungano ambao wanautumikia.

Maandiko yenu yanakubaliana kuwa wasomi wenye asili ya Zanzibar wamejaa huku Tanganyika.
M.Mwanakijiji anawaita wataalamu, Nguruvi3 unasema hawa wazanzibari wanafanya kazi maofisini.
Ninachokiona hapa ni kuwa Tanganyika ndio inanufaika kwa kupata wataalamu,wafanyakazi na kwa upande wa Zanzibar wamepoteza wataalamu, wafanyakazi (massive brain drain).

Tuvunje Muungano na hawa jamaa na tuwarudishie hazina ya wataalamu wao na nguvukazi yao.Itakuwa vyema pia tuwatake radhi kwa kosa tunalolitenda.

Sasa naelewa kwa nini hatutaki kuuvunja Muungano. Tutakosa wataalamu na watendaji.

Rai: Tuishauri serikali iwatilishe mkataba wanafunzi watakaopata ufadhili wa serikali kwa elimu ya juu kuwa baada ya masomo wanaahidi kurudi Zanzibar na kujenga nchi yao.

Elimu ya juu katika mtazamo huu inaumiza Zanzibar kwa kukosa wataalamu wake ambao wanabakia Tanganyika. Kwa upande mwingine Tanganyika inafaidika na hazina ya wataalamu wazanzibari.

Let Zanzibar go!
 
Mkuu Nguruvi3
Maandiko yenu yanakubaliana kuwa wasomi wenye asili ya Zanzibar wamejaa huku Tanganyika.
M.Mwanakijiji anawaita wataalamu, Nguruvi3 unasema hawa wazanzibari wanafanya kazi maofisini.
Ninachokiona hapa ni kuwa Tanganyika ndio inanufaika kwa kupata wataalamu,wafanyakazi na kwa upande wa Zanzibar wamepoteza wataalamu, wafanyakazi (massive brain drain).

Tuvunje Muungano na hawa jamaa na tuwarudishie hazina ya wataalamu wao na nguvukazi yao.Itakuwa vyema pia tuwatake radhi kwa kosa tunalolitenda.
Sasa naelewa kwa nini hatutaki kuuvunja Muungano. Tutakosa wataalamu na watendaji.
Rai: Tuishauri serikali iwatilishe mkataba wanafunzi watakaopata ufadhili wa serikali kwa elimu ya juu kuwa baada ya masomo wanaahidi kurudi Zanzibar na kujenga nchi yao.

Elimu ya juu katika mtazamo huu inaumiza Zanzibar kwa kukosa wataalamu wake ambao wanabakia Tanganyika. Kwa upande mwingine Tanganyika inafaidika na hazina ya wataalamu wazanzibari.Let Zanzibar go!
Wanaoobaki Tanganyika ni kuogopa dhiki iliyopo visiwani. Wote wapo huku wanakula mishahara kwa wakati. Wenzao waliorudi ZNZ wanasubiri fungu la hazina kutoka Dar. Kuna nyakati mishahara hakuna miezi 3

Mbona maalimu seif na wenzake wote wapo huku?Waliostaafu akina Karume, Mwinyi, Jumbe n.k. wapo huku wanakula raha zao.

Kama ZNZ ingetaka wataalamu kwanini iweke sheria ya kuzuia watu kupata ajira?

Hebu nikupe mfano, Hospitali ya VI Lenin inaweza kuwa na wataalam wangapi? Na hili ndilo linawatisha WZNZ wasithubutu kusema muungano basi! hawana uthubutu huo! BLW, La Mapinduzi na SMZ hawana uthubutu.
Soko la ZNZ ni dogo sana Nonda, ZNZ itaendelea kuishi katika kivuli cha Tanganyika kila siku ya mwenyezi mungu

Tunachosistiza waondoke ili watu wetu wapate ajira, hawa walioko huku wapo kwa upendeleo wa muungano kama walivyo wabunge wa ZNZ wanaowakilisha watu 2,500 kila mmoja.
Lakini pia kuna shida gani wakiishi na kulipa kodi bara. Wamesomeshwa bureee! na wazazi wao wanakula 11% ya pato la taifa bila kuchangia kitu, umeme wa bure kuanzia Darajani, ndani ya BLW hadi Ikulu.
Sasa tunasema basi kila mtu kwake, LET ZNZ GO!

Sisi hatuna haja ya kuvunja muungano kwasababu ndio nchi yenyewe. Nimewahi kukuuliza, ZNZ imewahi kufanya uchaguzi mara ngapi?
 
Sisi hatuna haja ya kuvunja muungano kwasababu ndio nchi yenyewe. Nimewahi kukuuliza, ZNZ imewahi kufanya uchaguzi mara ngapi?
Mkuu
Uchaguzi upi unaokusudia hapa?
Uchaguzi mkuu? au uchafuzi mkuu?
 
Wanaoobaki Tanganyika ni kuogopa dhiki iliyopo visiwani.

Nguruvi3,

Unajua kuwa kuna watanganyika wenzetu wanavuka bahari kuelekea Zanzibar?
Je hawa wanafuata dhiki huko? Kwa hiyo watanganyika tunapenda dhiki?
 
ZNZ itaendelea kuishi katika kivuli cha Tanganyika kila siku ya mwenyezi mungu

Sisi hatuna haja ya kuvunja muungano kwasababu ndio nchi yenyewe.
Nguruvi3,
Ukweli ni huu. Tanganyika inaishi katika kivuli cha Tanzania kila siku ya mwenyezi mungu.
Tanganyika iliishi bila ya kivuli cha Zanzibar na Zanzibar iliishi bila kivuli cha Tanganyika kabla 1964.
Baada ya 1964, Tanganyika inaishi katika kivuli/mwevuli wa Tanzania na Zanzibar inalazimishwa kubaki katika muungano na CCM.

Lakini unaweza kuelezea umma kwa nini wewe na M.Mwanakijiji mnapendelea twende kwenye serikali moja?
Mnapenda kuona Zanzibar inaingia tumboni mwa Tanganyika badala ya kuishi katika kivuli tu?
 
Last edited by a moderator:

Nonda, labda nirudie mtazamo wangu kama hujawahi kunisoma yapata miaka 2 sasa. Ukirejea mada zote za mwaka jana hasa tukijadiliana na akina Takashi, Baru baru, alsahfu, Juma Contena n.k swali ninalouliza ni kuwa Tanganyika itaathirikaje na kutokuwepo kwa Zanzibar. Hakuna anayenijibu bali kuzunguka zunguka tu. Kinyume chake mimi ninawaweleza wazi bila kumung'unya maneno, ZNZ inanufaika na muungano mara 10 ya Tanganyika,sababu ninazo na hakuna anayezipinga.
Nitafurahi ukinipa nafasi nikuulize swali moja tu na ukishindwa kulijibu kama alivyoshindwa Baru baru upishe wenye hoja wasemezane.

Mtizamo wangu ni LET ZNZ GO! period! Kama nikiongelea serikali moja basi nitapendekeza hivyo kama njia ya kuwalazmisha WZNZ wajiondoe katika muungano kwasababu njia za ustaarabu kupitia Baraza lislo na kazi la mapinduzi, BLW, SMZ zimeshindwa kuwasaidia WZNZ wanaoitaka nchi ya maziwa na asali.

ZNZ ya mwaka 1963 ilikuwepo na haikutegemea kivuli cha Tanganyika kwasababu ilikuwa ZNZ ya Oman. Mwafrika alikuwa dhalili na hivyo kulishwa tende na mabaki ya sadaka za zaka kama Ngamia. Hilo ndilo lilipelekea watu kubeba mapanga na mashoka kumondoa Sultan. Pengine kivuli cha Tanganyika hakikuonekana kwasababu ya Ubwana na utwana.

Kwa hali ya sasa dunia ya mwaka 1963 siyo ya 2012. Unajua karafuu inalimwa kila mahali, samaki wanavuliwa kila mahali na utalii ni shughuli kila mahali. Lakini pia iangalie ZNZ kwa eneo na population kabla hujakiangalia kivuli kinachoiandama.

Kivuli cha Tanganyika kipo si kwa kupenda ni kwa sababu za asili. Ni kwasababu hiyo leo Tanganyika ina Wazanzibar wengi kuliko nchi nyingine duniani. Nusu yao wanaishi Tanganyika, wanapata mapato yao Tanganyika, na wala si Kenya, Uganda, Msumbiji au Sychelles.

Kama si kivuli mwanana cha Tanganyika, basi uchungu walionao WZNZ kuhusu nchi yao wangeshafunga virago na kurejea makwao. Hilo halijatokea mitaani, Dodoma, Ofisi ya makamu wa Rais, Buguruni kwa Seif au Ilala kwa wapemba.
Kwa kuogopa kukikosa kivuli maridhawa cha Tanganyika, kila siku tunasikia nyimbo za serikali 3, mkataba au mahusiano.

Tanganyika wanasema enendeni kwa amani, ninyi mnasema serikali 3 n.k. Ni kitu gani kinawakwaza kama si kivuli burdani cha nchi Tanganyika!

Kivuli mwanana kinapatikana kwa kila MZNZ aliye bara au visiwani kuanzia mtaani, BLW hadi Ikulu.

LET ZNZ GO!
 
Nonda, ZNZ inanufaika na muungano mara 10 ya Tanganyika,sababu ninazo na hakuna anayezipinga.
Nitafurahi ukinipa nafasi nikuulize swali moja tu na ukishindwa kulijibu kama alivyoshindwa Baru baru upishe wenye hoja wasemezane.

ZNZ ya mwaka 1963 ilikuwepo na haikutegemea kivuli cha Tanganyika kwasababu ilikuwa ZNZ ya Oman. Mwafrika alikuwa dhalili na hivyo kulishwa tende na mabaki ya sadaka za zaka kama Ngamia. Hilo ndilo lilipelekea watu kubeba mapanga na mashoka kumondoa Sultan. Pengine kivuli cha Tanganyika hakikuonekana kwasababu ya Ubwana na utwana.

Kivuli cha Tanganyika kipo si kwa kupenda ni kwa sababu za asili. Ni kwasababu hiyo leo Tanganyika ina Wazanzibar wengi kuliko nchi nyingine duniani. Nusu yao wanaishi Tanganyika, wanapata mapato yao Tanganyika, na wala si Kenya, Uganda, Msumbiji au Sychelles.

Kama si kivuli mwanana cha Tanganyika, basi uchungu walionao WZNZ kuhusu nchi yao wangeshafunga virago na kurejea makwao. Hilo halijatokea mitaani, Dodoma, Ofisi ya makamu wa Rais, Buguruni kwa Seif au Ilala kwa wapemba.
Kwa kuogopa kukikosa kivuli maridhawa cha Tanganyika, kila siku tunasikia nyimbo za serikali 3, mkataba au mahusiano.

Tanganyika wanasema enendeni kwa amani, ninyi mnasema serikali 3 n.k. Ni kitu gani kinawakwaza kama si kivuli burdani cha nchi Tanganyika!

LET ZNZ GO!
Nguruvi3

Muungano umeinufaisha Tanganyika?
Muungano unainufaisha Tanganyika?
Kama jibu ni hapana kwa nini Tanganyika haichukui hatua ya kuifukuza Zanzibar/ wazanzibari?

Wewe unatumia kauli mbiu ya kuleta serikali moja kama njia ya kuwashajihisha Zanzibar kujitoa katika Muungano. Je unafikiri CCM waliposema kuwa wanatoka serikali mbili kuelekea moja walikuwa na mawazo kama yako? Walitaka/wanataka wazanzibari/ Zanzibar ijitoe katika muungano?

Kwa nini itumike njia ya mzunguko kama hii ya kauli "twende serikali moja" kama Tanganyika/ watanganyika hatutaki muungano au kama tumeshachoka/ tumeshatosheka na kelele za Zanzibar? Kwa nini hatugawi fito?

Umetaja idadi ya watu wazanzibari kuwa ni kubwa kulingana na eneo walilonalo.
Umewahi kusikia kuwa iko nchi inaitwa Singapore? link singapore linganisha ukubwa wa eneo lake na wakazi wake.

Je Sychelles inaishi katika kivuli cha nchi ipi? link seychelles Je Sychelles wanafanya shughuli zipi za kiuchumi ambazo wengine hawafanyi?

Kuna Mauritius pia link mauritius

Zanzibar wana kila sababu kupiga kelele kuwa wanabanwa na Muungano.Sera za kuibana Zanzibar katika Muungano na siasa za CCM zilizochochea ubaguzi huko Zanzibar kwa miongo kadhaa ndizo zilichochea wazanzibari kuhamia Tanganyika kwa sababu hawakuwa na njia nyengine ya kufanya. Sera za kibabe za Muungano chini ya uongozi wa Mwalimu ziliviza maendeleo ya Zanzibar katika kila nyanja kama zilivyoviza maendeleo kwa upande wa Tanganyika.Mwalimu aling'atuka huku nchi ikiwa fukara,wananchi hoi, taabani.

Kwa Muungano wa Tanzania kuwa ni Muungano wa baadhi ya mambo na si muungano kwa baadhi ya mambo. Je kweli Tanzania ni nchi moja?
Vipi Tanganyika inashughulikia mambo yake ambayo si ya Muungano? Inatumia kivuli cha nani?

Je unajua kuwa kuna watanzania-watanganyika wamepiga kambi Afrika Kusini? Botswana, UK,USA, Zanzibar,Namibia, Zambia. Je hawa hawakukiona kivuli mwanana cha Tanganyika?

Muungano unatumika kama kiini macho cha kusema Tanganyika haipo,hivyo watawala kujinufaisha kimafao huku wananchi tunaambia sababu ya umasikini haijulikani ,pia kwa upande wa Zanzibar viongozi wanasema m-bano/kibano kimekuwa kikali hawana njia ya kuwasiliana moja kwa moja na mataifa mengine kutafuta wabia wa maendeleo.
Muungano ni kiini macho tu.

Kivuli mwanana cha Tanganyika kimetuletea usingizi wa pono.Wajanja wanakula nchi, watanganyika tunagawiwa umaskini.

Nguruvi3
Kwa sababu gani tuliacha kutumia neno Tanganyika?
Kwa nini hatukumuunga mkono Rev. Mtikila kama tuna uchungu na Tanganyika yetu?
 
Nimekuwa mtetezi wa Muungano kiasi kwamba nimegundua nimebakia peke yangu. Wengine wanautetea Muungano kwa kutumia vitisho na wengine wanautetea kwa kutumia dharau.
Muungano huu wa kero umeandika historia ya kutetewa na wanaCCM, sijui wewe M:Mwanakijiji unautete kwa sababu ipi?
Kama muungano huu unaitia Tanganyika hasara ni kusema wewe huna uchungu na Tanganyika yetu?

Lakini historia inajirudia, huko peke yako katika kutetea Muungano wa kero ambazo wewe umekiri hazitatuliki.
NITAUTETEA MUUNGANO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema ataendelea
kuutetea Muungano na hakuna atakaemlaghai wala kumchezea katika uongozi wake.

Hata hivyo alisema kuwa Muungano upo na utaendelea kuwepo na kwani yeye ndiye rais ambaye anatokana na
chama cha mapinduzi na pia ameingia madarakani chini ya ilani ya chama chake hivyo lazima afuate ilani ya chama
chake ambapo alisema changamoto zilizomo zinahitaji kujadiliwa ili kuweza kuziondoa na sio kuvunja muungano.

“Hakuna mtu asiyejua kuwa kuna kero za Muungano hivyo ni vizuri tukajitokeza kwa wingi katika kutoa maoni yetu
juu ya katiba..."
Link hukopekeyako
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, Muungano uliridhiwa bara tuu na sio Zanzibar!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!
.
Katika pita pita yangu humu jf, nimekutana na hii copy and paste
Na mimi nimebainisha wazi kuwa Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.
Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!.

Nafikiri umenielewa hapo.

Cc; Nguruvi3, Joka kuu, Mkandara, Bobuk, Gombesugu, Ritz, The Big show,Mohamed said.

Hakuna ubaya ku copy na ku paste mawazo ya memba yoyote, tatizo ni pale mtu unapochukua mawazo ya mtu mwingine, pari materiale (word for word) na kuyaita yako, bila hata attribution or just mention mawazo hayo ni ya nani au just to mention the source kuwa ni thread hii ya Mkuu Mzee Mwanakijiji!.

Japo hili sio lile kosa la jinai la plagiarism, ila hata michango ya jf, ni literacy job, itendee haki jf, watendee haki wana jf!. Ila pia its such an honour, pale michango ya wana jf, inapotumika kama citation na authority na wasomi wa vyuo vikuu vya Bara Arab!.

Pasco
 
Serikali Mbili: wanotaka muundo huu ni CCM kwa sababu ambazo umeshazielezea - yaani wana hofu kubwa ya kupoteza madaraka na sio kwa sababu nyingine yoyote.
 
MMKJJ,
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, hoja yoyote ya kuuvunja muungano ni uhaini!.

Angalieni jf tusije nyooshewa vidole tuu wachochezi!.

Tukiamua kufuata sheria, taratibu na kanuni, muungano ni kwa bara tuu, kwa Zanzibar hauna legitimacy, hivyo kuuvunja from that side ni haki yao.

Naunga mkono hoja!.

Pasco.
Najikumbusha tuu kuwa niliunga mkono hoja hii, lakini sasa nataka tuudumishe muungano wetu ila uwe ni muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!

Pasco
 
Najikumbusha tuu kuwa niliunga mkono hoja hii, lakini sasa nataka tuudumishe muungano wetu ila uwe ni muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!

Pasco

Maajabu ya mwaka haya!
 
Najikumbusha tuu kuwa niliunga mkono hoja hii, lakini sasa nataka tuudumishe muungano wetu ila uwe ni muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!

Pasco
Iitwe zantania na raisi atoke zanzibar,pia makao makuu na shughuli zote za serekali zifanyike pemba.
 
Najikumbusha tuu kuwa niliunga mkono hoja hii, lakini sasa nataka tuudumishe muungano wetu ila uwe ni muungano kamili wa nchi moja, serikali moja na rais mmoja!

Pasco

nakuunga mkono
 
Back
Top Bottom