MtoboasiriBarubaru, nakiri kuwa umerudia rudia sana maneno yale yale isipokuwa hujajibu swali la msingi (na ndio hoja ya Mzee Mwanakijiji): iweje BLW liweze kutunga sheria zinazovunja katiba ya JMT lakini lishindwe kujitoa kwenye muungano? Kama Wanzibari hawaridhiki na muungano wanashindwa nini kujitoa ukitilia maanani kuwa muungano wenyewe hauna nguvu ya kisheria (kwa mujibu wa madai kuwa the union articles were never ratified by any competent authority in Zanzibar)?
Na hata mkataba wa muungano ungekuwa halali kisheria, ina maana hauwezi kuvunjwa? Mkataba unatakiwa ama kubadilishwa au kuvunjwa endapo kuna upande usioridhika iwe na kipengele kimoja au zaidi ndani ya mkataba, na initiator ni yule asieridhika!
Ukipindua hii hoja yako.
Je Bara/Tanganyika inaridhika na muungano?
Kama hairidhiki na Muungano huu kwa nini hatutaki kuuvunja?
Wabara/watanganyika 40 milioni tunasubiri watu laki 9.5 wauvunje ?
Je muungano una maslahi kwa watanganyika? Kama hauna kwa nini hatuchukui hatua kuuvunja?
Kuhusu katiba ya Zanzibar, nafikiri wengi hata mwanasheria kama Lissu anashindwa kuelewa.
Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar zina uzito sawa. Kila moja inajitosheleza. Kila katiba ina mamlaka yake na mipaka yake. Kwa kukosekana katiba ya Tanganyika ndio mambo yote yanakuwa hayaeleweki.
Kiufupi, Tanzania ina mamlaka tatu kisheria, mamlaka ya mambo ya Bara(Tanganyika), mambo ambayo si ya muungano. Kuna mamlaka ya mambo ya Zanzibar, mambo ambayo si ya muungano na kuna mamlaka ya mambo ya muungano, mambo ya pamoja ya Tanganyika na Zanzibar(mambo ya muungano). Kila katiba hapo inajitosheleza.
Imeshasemwa sana hapa kuwa wanaonufaika na Muungano ni viongozi wa pande mbili za muungano ambao ni chini ya 1%. Wananchi wa Tanganyika na wananchi wa Zanzibar wanafanywa mhanga tu wa viongozi kugawana keki ya Taifa.Watanzania wanagawiwa umaskini tu.
Wananchi wa Zanzibar ambao hawana uwezo wa kutamka kisheria kuwa wanauvunja Muungano wanapiga mayowe, wanapiga kelele kuwa wameshachoshwa na mazingaombwe ya Muungano.Na hakuna ambaye hajasikia kelele hizo.
Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mkandara, Nonda wanajitahidi kutuamsha(kutoa UAMSHO) kwa sisi wabara/wadanganyika tuamke kama wenzetu wa Zanzibar ili tumfunge paka kengele, tuondokane na mazingaombwe ya muungano. Lakini wadanganyika bado tunapiga usingizi, usingizi mnono.usingizi fofofo.
Tunajisifia tuna madini, gesi, almasi,mafuta lakini shule zetu,shule za kata na walimu fasta fasta, nyumba za nyasi na kuishi "kimjini"(ubabaishaji na ulaghai). Utajiri wetu umetusaidia nini? Sisi ni maskini, fukara kiasi ambacho tunapohongwa kofia na fulana wakati wa kampeni hujiridhisha kuwa mungu ametukumbuka.
Watanganyika tupige kelele kuwa muungano unatunyonya ili wabunge wetu nao waanze kupiga kelele bungeni kama Raza. Huenda viongozi wa Serikali waliotia pamba masikioni, kama kelele hizo zitakuwa kali, masikio yatazibuka.
Kwa nini haibukii G55 nyingine? Ili kuibuka G110 inabidi sisi wadanganyika tuanze kupiga mayowe ,kama kupiga kelele hatuwezi...anyway, mtu aliyelala hawezi kupiga kelele, tuamke kwanza!
Tudai Tanganyika yetu and this mess will sort itself out!