Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Kwenye masuala yanayohusu mikopo, Leverage ni neno linalomaanisha ‘getting more from less’, maana yake unaweza ukawa na shilingi elfu kumi mfukoni mwako halafu ukaitumia hiyo elfu kumi yako kupata elfu kumi na mbili kutoka kwenye taasisi ya fedha kwa njia ya mkopo.
Kunufaika na ‘Leverage’ kutakuhitaji uwe na biashara imara. Nikizungumzia biashara imara namaanisha ni ile yenye mzunguko wa kueleweka na mapato yake yanaenda yakikuwa mwaka hadi mwaka (sustainable business).
Changamoto nyingi ambazo nakutana nazo kama mshauri wa masuala ya kibiashara na mikopo, ni pale unapokuta mtu ana biashara yenye mzunguko (cash flow) mzuri ambao unaifanya kuwa na uwezo mkubwa wa kulipa mkopo wa benki lakini unakuta tatizo ni kwamba mfanyabiashara au kampuni hiyo haina mali isiyohamishika ambayo itatumika kama dhamana ya mkopo benki.
Na tukienda kwenye uhalisia wa nchi yetu ya Tanzania, bila dhamana ni vigumu sana kupata mkopo, japo najua kuna aina fulani za mikopo ambayo mfanyabiashara anaweza kupata bila dhamana lakini ni mikopo migumu sana kuipata, kwa aina ya taasisi za fedha tulizonazo.
Lengo la mada yangu ya leo ni kutoa mbinu ambayo inaweza kusaidia wafanya biashara kuweza kuendeleza biashara zao na wakati huo huo kuwa na msingi wa mali isiyohamishika ambayo itamsaidia mfanyabiashara au kampuni kuitumia kama dhamana wakati wa kwenda kukopa.
Na mbinu nzuri ya biashara kuweza kufanya hivo ni kuwa na utaratibu wa kutoa kiasi kidogo cha fedha (kuwekeza) kutoka kwenye mzunguko wa biashara katika kipindi cha kila miezi sita au mwaka mmoja. Kwa mfano: Biashara ya uchuuzi yenye makusanyo ya milioni 50 kila mwezi maana yake ina profit potential ya milioni 6 kila mwezi ambayo ni kama wastani wa 72 millioni kwa mwaka, hivo kwa msingi huo biashara ina uwezo wa kutenga walau milioni 20 kila baada ya miezi sita na kuiwekeza kwenye mali ya muda mrefu. Na kwa kufanya hivo, ndani ya miaka 2 kama itaendelea na utaratibu huo, maana yake mfanyabiashara au kampuni itakuwa imewekeza kwenye kiasi cha milioni 80.
Mali nzuri ya muda mrefu ni ipi?
Mali zipo za aida nyingi sana, nitaorodhesha baadhi ya mali zinazoweza kununuliwa (kuwekezwa) na kwenye kila moja nitaweka faida zake na namna biashara inavoweza kunufaika nayo kuitumia kama dhamana.
Faida ya nyumba kwenye dhamana ya mikopo
Hivyo kwa mahesabu hayo ya kuwekeza mfano (milioni 20 kila miezi sita kwa miaka 2), ikiwa mfanyabiashara amefanya maamuzi mazuri ya kuwekeza kwenye nyumba kwa kuangalia location nzuri, akaijenga nyumba yake vizuri kiasi cha kutoa fursa za ile nyumba kuvutia wapangaji ambao watafanya kuwe na uhakika wa kodi kupatikana kutoka kwenye nyumba ile, maana yake ni kwamba anaweza kutumia milioni 80 kuijenga ile nyumba lakini ukakuta thamani ya ile nyumba ni milioni 150 pindi inapofanyiwa valuation. Hapa tuelewane kitu kimoja, kwenye mambo ya kifedha kuna tofauti kubwa sana kati ya ‘price’ na ‘value’. Huwa tunasemaga, ‘price is what you pay, value is what you get’.
Sasa kwa mfanyabiashara mjanja ukishakuwa na biashara yako nzuri inayotengeneza mzunguko mzuri (cashflow), hapo ukienda kwenye taasisi ya fedha na mkononi una nyumba yako yenye thamani ya milioni 150, maana yake huwa ni rahisi sana kuweza kupatiwa mkopo wa hadi milioni 120 au milioni 100 ambayo ni kubwa Zaidi ya ule uwekezaji wako wa milioni 80. Hivo unajikuta kwa kutumia mahesabu hayo, unaweza kuirudisha kwenye mzunguko hiyo milioni 120 au milioni 100 na hapo utakuwa umenufaika pakubwa.
Wakati mwingine, ukishakuwa na nyumba ambayo tunai regard kama mali yenye life expectancy kubwa, unaweza ukajikuta unapatiwa mkopo wenye malipo ya hadi miaka 10 kitu ambacho kitakufanya ufanye marejesho kwa kutumia pesa inayopatikana kwenye kodi wala haita athiri mzunguko wa biashara yako.
Hivyo nikihitimisha, kwa wafanyabiashara wenye malengo ya kuja kupata mikopo na kukua kibiashara, kamwe usiwe unawaza kuwekeza faida yako yote ya kibiashara kwa kutanua tu ukubwa wa biashara yako i.e. kuagiza mzigo na kuongeza stocks, ni faida kufikiria na kutengeneza msingi wa kuwa na mali imara isiyohamishika ambayo hapo baadaye itakusaidia kwenye masuala ya mikopo.
Ni mimi,
Mikopo Consultant
I breathe and sniff money, if you, too, follow the money, our roads might cross somewhere!! Tchao

- Hisa: Unaweza kutumia sehemu ya cashflow yako kununua hisa kwenye makampuni ambayo yapo listed kwenye masoko ya fedha. Faida ya hisa ni kwamba kuna uwezekano wa kupata gawio kwenye uwekezaji wako japo sio lazima kupata gawio pia kwasababu gawio hutegemea na faida ya kampuni ulilowekeza. Faida nyingine pia ambayo inaweza kujeuka hasara pia ni kwamba, hisa zinaweza kupanda thamani maradufu na pia zinaweza kushuka thamani maradufu. Uwezekano wa kupanda thamani na kushuka thamani, kunafanya hisa kutokuwa dhamana ambayo inaweza kukubalika kwa urahisi na taasisi za fedha. Japo kuna wateja wanakopeshwa kwa dhamana ya hisa ila sio maamuzi rahisi kufanyika na hufanyika kwa wateja wachache. Hivo kwa mfanyabiashara ninayemlenga, hii sio option nzuri sana ikiwa unalenga kupata mkopo.
- Gari: hii nayo ni mali ambayo unaweza ukawekeza cashflow zako lakini changamoto ya gari ni kwamba kama sio gari ya biashara maana yake yenyewe itakuwa haiingizi pesa bali itakuwa inatumia pesa kupitia operations zake na gharama za matengenezo. Kibaya Zaidi ni kwamba gari hushuka thamani kwa kasi sana, ukinunua gari la milioni 80 leo, kesho ukisema unaliuza kwa milioni 75 unaweza kukosa mteja na baada ya miaka 4 ukiweka depreciation hapo hata milioni 40 huwezi kupata. Hiyo inafanya gari kutokuwa mali nzuri ambayo itakusaidia kama mfanyabiashara kuweza kuitumia kupata mkopo.
- Dhamana za serikali (bonds): Hizi hazipandi thamani japo faida yake ni wewe kuweza kupata malipo ya riba kila baada ya miezi 6. Faida ya bond ni kwamba ni mali ambayo inakubalika kwa urahisi sana na mabenki kama dhamana kwasababu haishuki thamani (japo kwa mazingira Fulani ikitokea crisis au sharp inflation, bei yake inaweza kushuka kwa kasi sana). Ila kwa mfanya biashara ambaye ana shauku ya kufanya leveraging, hii pia sioni kama ni mali sahihi ya kununua kwasababu haiwezi kupanda thamani yake, ile face value ni fixed contract haiwezi kubadilika. Kwahiyo sio uchaguzi mzuri sana.
- NYUMBA: Hii nimeiwekea herufi kubwa kwasababu ni kitu ambacho kwa maoni yangu, kama kitafanya kwa akili kinaweza kukupa faida ambazo hazipatikani kwenye mali nyinginezo hapo juu. Faida ya kwanza ya nyumba ni mali ambayo haishuki thamani (depreciate) kwa haraka kama gari, pili, nyumba kama ikiwekezwa kwa usahihi itakuwezesha kupata kipato kupitia kodi ya upangaji, tatu, nyumba ipo kama hisa inauwezo wa kupanda thamani na kushuka thamani lakini kwakuwa tunaishi kwenye nchi ambayo ina high population growth, uwezekano wa nyumba kushuka thamani ni kama 20% wakati uwezekano wa kupanda thamani ni 80%. Hii inafanya nyumba kuwa mali bora sana ambayo ni ya uwakika na ni mali ambayo taasisi za fedha huiangalia kama dhamana bora ya mkopo.