JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Huu ni uzinduzi wa maadhimisho ya Haki za Binadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Tukio hili linaangazia masuala muhimu kuhusu haki za binadamu nchini Tanzania, ikiwemo utetezi wa haki za wanawake, watoto, watu wenye ulemavu, na makundi mengine ya kijamii.
UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI ZA BINADAMU MWAKA 2024
Dar es Salaam, Oktoba 17, 2024
Leo tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 2024, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinazindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu itakayoadhimishwa mnamo tarehe 10 mwezi Disemba mwaka 2024.
Kila mwaka, Jumuiya ya Kimataifa inaungana tarehe 10 mwezi Disemba kuadhimisha siku hii muhimu, ikiwa ni kumbukizi ya kupitishwa kwa Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR) na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Azimio hili linaorodhesha katika vifungu 30 haki za msingi ambazo kila mtu anastahili kuwa nazo bila kubaguana kwa rangi, taifa, jinsia, dini, siasa, fikra, asili ya taifa la mtu, mali, kwa kizazi au kwa hali nyingine yoyote.
Sehemu kubwa ya vipengele vya Azimio hili vimeingia katika mapatano ya kimataifa juu ya haki za kiraia na kisiasa ya mwaka 1966 na mapatano ya kimataifa juu ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ya mwaka 1976 na kwa njia hiyo zimekuwa sehemu ya sheria za kimataifa. Mapatano haya ya kimataifa juu ya haki za kiraia na kisiasa ya mwaka 1966 na juu ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ya mwaka 1976 ndio hasa yameingizwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hususani sehemu ya pili ya Katiba inayoelezea malengo muhimu na misingi ya mwelekeo wa shughuli za serikali na sehemu ya tatu inayoelezea Haki na wajibu muhimu.
Kwa kawaida, maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Haki za Binadamu huongozwa na kauli mbiu maalum inayolenga kuchagiza changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa haki za binadamu na kutoa wito kwa mataifa na wadau kuchukua hatua muhimu. Kwa mwaka 2024, kauli mbiu ya maadhimisho ni "Usawa - Kupunguza Ukosefu wa Usawa na Kukuza Haki za Binadamu." Kwa lugha ya kiingereza "Equality - Reducing inequalities and advancing human rights".
Maadhimisho ya mwaka huu 2024 pamoja na kauli mbiu yake yameambatana na kikao cha ngazi ya juu cha viongozi wa Jumuiya ya Kamataifa Kilichofanyika mwezi Septemba mwaka huu 2024 Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani. Kikao hicho kimefanyika ili kupitisha makubaliano ya pamoja ya jinsi ya kuhakikisha hali ya sasa ya haki za binadamu duniani inakuwa bora na wakati huo huo kulinda mustakabali wa Pamoja kwa mataifa yote.
Kwa nchi ya Tanzania, maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu kwa mwaka 2024 yanashuhudia kuongezeka kwa matukio ya kikatili yanayokiuka haki za binadamu nchini, ikiwemo vitendo vya kutishiwa, utekaji na mauaji ya watu wasio na hatia ikiwa ni pamoja na wenza na watoto. Pia hivi karibuni Tanzania imeshuhudia utekelezaji wa Sheria kandamizi zinazominya uhuru wa Habari na vyombo vya habari hususani maudhui ya mitandaoni. Hali hii isipochukuliwa hatua ina hatari ya kuzua hofu, taharuki na kutishia usalama miongoni mwa raia nchini.
Hata hivyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaendelea kuamini katika misingi ya amani na utulivu ambayo nchi ya Tanzania imeijenga kwa kipindi kirefu sasa. Ni wajibu wa Serikali, vyombo vya usalama na wadau wote katika kusherehekea maadhimisho haya ya Haki za Binadamu, kuweka mikakati na kuchukua hatua Madhubuti kurejesha hali ya ulinzi wa haki za binadamu nchini.
Katika kuadhimisha siku hii muhimu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kikiwa pia kinamalizia utekelezaji wa mpango mkakati wake wa miaka sita (2019-2024) ximeandaa matukio mbalimbali yanayolenga Kupunguza Ukosefu wa Usawa na Kukuza Haki za Binadamu nchini kulingana na kauli mbiu ya maadhimisho.
Mambo yafuatayo yatatekelezwa tangu mwezi huu wa Oktoba hadi siku ya Kilele tarehe 10 mwezi Disemba mwaka 2024:
1. Mashindano ya kazi za Sanaa kwa wanafunzi: Kwa lengo la kukuza vipawa, uelewa na kutoa motisha kwa vijana kuhusu Haki za Binadamu na utetezi wa haki za binadamu nchini, kimeandaa Mashindano ya sanaa yatakayohusisha shule zenye klabu za haki za binadamu katika jiji la Dar es Salaam. Washindi watatunukiwa zawadi siku ya kilele cha Maadhimisho ya Haki za Binadamu tarehe 10 Disemba 2024.
2. Kutoa Msaada wa Kisheria kwa wahitaji hususani wanawake: LHRC itapiga kambi maeneo tofauti tofauti ya jiji la Dar es Salaam kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa watu wote hususani wanawake, wanaoishi katika maeneo yenye matukio mengi ya uvunjifu wa haki. Ripoti za LHRC zinaonyesha kuwa wanawake ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio haya, na mpango huu utawalenga hasa wale ambao hawawezi kufika kwenye ofisi za kituo.
3. Kutoa elimu ya kisheria kupitia Mitandao ya Kijamii: Mara baada ya uzinduzi huu hadi siku ya kilele cha maadhimisho, LHRC kupitia mitandao ya kijamii itasambaza maudhui yenye lengo la kuelimisha umma na kujadiliana kwa pamoja na wadau mbali mbali wa haki kuhusu namna bora ya kuboresha utekelezaji wa haki za binadamu nchini kwa kuzingatia usawa.
4. Filamu fupi ya mafanikio ya kukuza Haki za binadamu nchini: Kwa kuhitimisha mpango mkakati wake wa miaka sita (2019-2024), siku ya kilele cha maadhimisho, LHRC itaonesha filamu fupi (documentary) yenye maudhui yanaelezea miaka sita ya mafanikio ya katika kukuza haki za binadamu nchini kwenye maeneo ya elimu ya haki za binadamu kwa umma, huduma za msaada wa kisheria, kesi za kimkakati na maeneo mengine muhimu hususani katika sekta ya haki za binadamu na biashara.
5. Uzinduzi wa Mpango mkakati wa LHRC wa Miaka 6 ijayo (2025-2030): Kwa furaha kubwa kabisa, LHRC inatarajia kuzindua mpango mkakati wake wa miaka 6 ijayo (2025-2030) siku ya kilele cha maadhimisho ya Mwisho, tunapenda kuwakaribisha wadau wote katika kuadhimisha siku hii adhimu ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.
Imetolewa na;
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Dkt. Anna Henga
Mkurugenzi Mtendaji