Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

BARAZA LA MAWAZIRI LA LOWASSA
  1. h
  2. Waziri Mkuu Professor Juma Kapuya
  3. Waziri Maliasili na Utalii Mghana Msindai
  4. Waziri wa Nishati na Madini William Ngereja
  5. Bunge Sera na Uratibu Hamis Mgeja
  6. Wanawake na Watoto Sophia Simba
  7. Habari Michezo na Utamaduni Beatrice Shelukindo

Jazeni wengine, halafu eti hawa ndio tunategemea kutuletea mabadiliko Tanzania, utani mwingine umepitiliza!

Waziri wa Uchukuzi. Peter Serukamba
 
I cry for my beloved country, Loawasa akiwa rais nchi hii itaangamia na sijui kama uoinzani wata survive manake jamaa ni udikteta kwa mbele
 
Lowassa ni mwizi hafai kuwa kiongozi. Lowassa ni fisadi hafai kuwa kiongozi, huko kupendwa na wengi siyo bali ananunua kupedwa

Mtoa mada naye kanunuliwa kuyasema aliyoyasema. Kupendwa kupi anakopendwa Lowasa kama sio pesa yake?
 
lowassa bear the hit! ona jinsi muhongo alivyokomaa ona tibaijuka alivyokuwa mbishi but "enl kwa hekima alistepdown na hii ni heshima kubwa sana kwa lowassa!
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, hivyo kumchinjia rasmi baharini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingu huko nyuma na labda ni kweli ndicho walichopanga kukifanya mwaka huu!, yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Pasco

Team UKAWA nao kwenda MONDULI kumshawishi ili agombee! KAZI IPO MWAKA HUU, TETESI NI NOMA
 
ujanja wa samaki ni majini tu huyu lowasa aka mwizi mkuu wa taifa anatapa tapa tu kama yeye mwanaume atoke nje ya ccm
ramon kwani kapewa ule ubunge wa dr mrema huyu mwanamme na ameenda jando hashwa karibu mfano chukua nigeria
 
Mpaka sasa bango chafu la Lowassa ni ufisadi, ambalo limeshindwa kuthibitishwa uhalisia wake. Hiyo inawafanya makada na wananchi kuamua kumkumbatia baada ya kugundua mchezo mchafu unaoendelea. Wananchi wanafurahishwa na maamuzi magumu na sahihi aliyo nayo Lowassa kwa Taifa.

Wameshindwa kumfungulia mashtaka bado wanalia kuwa ni mwizi.Wana tume ya maadili walishindwa kumtupa nje ya chama ,lakini wanabweka kama mbwa asiye na meno japo wana meno yenye ncha kali.Lakini wanaimba kwa sauti kubwa eti wanatawala nchi kwa haki na utawala bora na kisheria.Labda zipo chuki binafsi na kuendekeza majungu kama mbinu za kupakana matope.Je mwananchi wa kawaida asiye na rungu ya serikali au mahakama au kigogo kwenye chama chao CCM achukue lipi na aache lipi?Mchezo huu hausaidii taifa au CCM.Tunataka maelezo kwa kina sio vichwa vya habari tu.Mwisho wa siku tunataka kuchagua raisi bora sio bora rahisi.
 
Wameshindwa kumfungulia mashtaka bado wanalia kuwa ni mwizi.Wana tume ya maadili walishindwa kumtupa nje ya chama ,lakini wanabweka kama mbwa asiye na meno japo wana meno yenye ncha kali.Lakini wanaimba kwa sauti kubwa eti wanatawala nchi kwa haki na utawala bora na kisheria.Labda zipo chuki binafsi na kuendekeza majungu kama mbinu za kupakana matope.Je mwananchi wa kawaida asiye na rungu ya serikali au mahakama au kigogo kwenye chama chao CCM achukue lipi na aache lipi?Mchezo huu hausaidii taifa au CCM.Tunataka maelezo kwa kina sio vichwa vya habari tu.Mwisho wa siku tunataka kuchagua raisi bora sio bora rahisi.

Umenifilisi maneno yote ..... Waambie bhaelewee
 
Pasco, Pasco, Pascooooo! Kamwe, Lowasa hawi rais wa Tanzania. Na hata kama akipitishwa na CCM hatakuwa rais. Alikosea kuto kuwaunga mkono watanzania wanaoitaka serikali ya Tanganyika.
 
Heshima mbele mkuu.Lowasa ni kweli kabisa anapendwa na wengi lakini kwa mimi mwaka huu sijaona mgombea mahususi toka vyama vyote.Lakini kuna baadhi ya masuali huwa najiuliza,Ni mgombea gani ndani ya CCM hana kashfa ya ufisadi?.Je baada ya EL kuenguliwa kutokana na ufisadi hatujaona tena au kuthibitisha ufisadi mwingine baada ya yake?.Je kama viongozi wote ni wachafu ndani ya ccm itabidi wawapitishe kuangalia nani mchapakazi zaidi ingawa ana makandokando?.Je ccm itakapo acha kumpitisha kuwania uraisi ana ujasili wa kuhama chama?.Na nini kitakachotekea ndani ya ukawa baada ya EL kuacha kupitishwa ndani ya CCM?.Na je hatuoni kwamba baadhi ya wagombea wa UKAWA kila mtu atahisi kuishinda ccm imeyobaki dhaifu baada ya EL kuondoka?.Je hao mashekhe na Maaskofu wanao mpigania EL kuwa raisi wanahitaji nini kutoka kwake?.Mimi nafikili ccm wawe makini sana na uamuzi wowote ule watakao fanya.Na pia Ukawa wawe makini sana kama EL akihama chama mana kila mgombea wa ukawa anaweza hisi anazo nguvu za kuishinda ccm dhaifu baada ya EL kuondoka na kundi kubwa na hivyo ikawa ni mwazo wa UKAWA kusambaratika.
Hawataweza kukata jina la EL sababu ndiye pekee ndani ya ccm mwenye uwezo wa kuwashinda wapinzani hata wabaya wake wanalijua hilo kukata jina lake itakuwa sawa na ku commit suicide yaani watakuwa wametoa nafasi kwa mara ya kwanza ktk Tz upinzani kutoa raisi.
 
Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mbebaji. Nyie mpigeni EL chini, UKAWA tunapetaaaaaaa tu!
 
MTU timamu hawezi kumshabikia Huyo mwizi eti awe rais.Toka mini ukawakabidhi fisi bucha eti wailinde? lowasa ni mwizi na mtoa rushwa Mkubwa. Ameshawanunua wengi akiwemo mleta mada lakini hana uwezo was kuwanunua watz zaidi ya mil 20 tunaotaka mabadiliko na tunaojiandikisha ili Oct tupige kura
 
Kuongozwa au kumpa uongozi mwizi litakuwa ni kosa ambalo mungu hawezi kutusamehe kamwe....lowassa mwizi!
 
Kuongozwa au kumpa uongozi mwizi litakuwa ni kosa ambalo mungu hawezi kutusamehe kamwe....lowassa mwizi!

Dhibitisha wizi wake kwanza.Pammoja na hilo nani mwanasiasa kati hao msafi?Labda malaika.
 
Back
Top Bottom