Licha ya kwamba nami nashangaa kama wengine lakini namuamini Rais Samia

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Siku za karibuni watanzania wamekuwa wakishangazwa na yanayoendelea, ni kama walikuwa kwenye usingizi mzito wasijue ni nini kinachoendelea lakini kadiri usingizi unavyoisha ndivyo wanabaki kufurahi.

Baadhi ya vitu vinavyoshangaza na vimekuwa kama ndoto ya kutisha ni kama:

I) Iliwezekanaje January na Nape kurudi uongozini baada ya yale yote waliyofanya?

II) iliwezekanaje Rugemalira akawa nje licha ya yote tuliyosikia juu yake?

III) Imewezekanaje mwenye kesi ya kujibu mahakama( Makonda) kuwa mshtaki?

IV) Iliwezekanaje Lawewnce Mafuru na Nehemia mchechu kurudi ?

V) Imewezekanaje Polepole ambaye suala lake la utovu wa nidhamu likiwa bado linajadiliwa ateuliwa ubalozi?

V) Imewezekanaje mtu aliyefunguliwa kesi ya ugaidi kuachiwa huru ?

VI) Inawezekanaje watu wasio wanachama wakaendelea kuwa wabunge?

Hayo ni baadhi ya mambo yanayoshangaza sana kuyatafakari. Ni mambo magumu sana kueleweka.

Licha ya ugumu wake, bado namuamini sana Rais Samia kuendelea kuwa mpambanaji na mwendelezaji mzuri wa mipango wa serikali iliyopita. Kwenye suala la usalama na ulinzi, ujenzi wa miundombinu, usimamiaji wa rasilimali zetu ,usawa wa kijinsia na ukuzaji wa demokrasia amefanya vizuri sana.Pongezi kwake
 
Haya mambo yanaumiza Sana kichwa siasa za Tanzania sitaki hata kuziwaza...me nachotaka nipate TU hela NI spend hela ndani ya Nchi nzuri Tanzania yenye mabonde yanayofaa kwa nafaka...mengine haya yabaki Kama stori TU na wadau ila siyatilii Tena maanani
 
Elimu ya bongo ni hovyo sn inawezakana wewe hapo ulipo una masters yako lakini ulichoandika ni bora ya PhD Musukuma
 
Haya mambo yanaumiza Sana kichwa siasa za Tanzania sitaki hata kuziwaza...me nachotaka nipate TU hela NI spend hela ndani ya Nchi nzuri Tanzania yenye mabonde yanayofaa kwa nafaka...mengine haya yabaki Kama stori TU na wadau ila siyatilii Tena maanani
Siasa ndiyo inayoamua maisha yako kwa 80%
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Nakubaliana na wewe maana hata maofisini mambo ya kazi yanategemea Sana watunga sera wanachukuliaje uzito Jambo husika..mfano akiingia rais mpenda uvuvi Basi sekta ya samaki lazima ai push unakuta ujenzi utapunguzwa bajeti...ndo hivo sometimes.

NI kucheza TU na upepo wao ma boss.nisichotaka Mimi NI kushindana na mtu ambae huwezi kumshinda....Kama Mimi siamini Tena Kama upinzàni utawaweza ccm kwa jinsi walivyojitanua ktk kila Kona ya Nchi...dakika ya mwisho Bora niungane nao tu ili niwe na amani ya moyoni.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nakubaliana na wewe maana hata maofisini mambo ya kazi yanategemea Sana watunga sera wanachukuliaje uzito Jambo husika..mfano akiingia rais mpenda uvuvi Basi sekta ya samaki ...
Maumivu ya CCM unaweza wewe usiyaone akaja kuyaona mjukuu wako, lengo la CCM ni kukubana usalimu kama ulivyofanya hivyo
 
Siku za karibuni watanzania wamekuwa wakishangazwa na yanayoendelea, ni kama walikuwa kwenye usingizi mzito wasijue ni nini kinachoendelea lakini kadiri usingizi unavyoisha ndivyo wanabaki kufurahi.

Baadhi ya vitu vinavyoshangaza na vimekuwa kama ndoto ya kutisha ni kama:

I) Iliwezekanaje January na Nape kurudi uongozini baada ya yale yote waliyofanya?

II) iliwezekanaje Rugemalira akawa nje licha ya yote tuliyosikia juu yake?

III) Imewezekanaje mwenye kesi ya kujibu mahakama( Makonda) kuwa mshtaki?

IV) Iliwezekanaje Lawewnce Mafuru na Nehemia mchechu kurudi ?

V) Imewezekanaje Polepole ambaye suala lake la utovu wa nidhamu likiwa bado linajadiliwa ateuliwa ubalozi?

V) Imewezekanaje mtu aliyefunguliwa kesi ya ugaidi kuachiwa huru ?

VI) Inawezekanaje watu wasio wanachama wakaendelea kuwa wabunge?

Hayo ni baadhi ya mambo yanayoshangaza sana kuyatafakari. Ni mambo magumu sana kueleweka.

Licha ya ugumu wake, bado namuamini sana Rais Samia kuendelea kuwa mpambanaji na mwendelezaji mzuri wa mipango wa serikali iliyopita. Kwenye suala la usalama na ulinzi, ujenzi wa miundombinu, usimamiaji wa rasilimali zetu ,usawa wa kijinsia na ukuzaji wa demokrasia amefanya vizuri sana.Pongezi kwake
Jiulize wale watawala waliotuambia JPM yupo anachapa kazi na kuchekiwa chekiwa ni kawaida leo ndiyo waombolezaji mahiri wa kifo cha JPM!Bado wapo madarakani wale waliopora mchakato wa uchaguzi 2020 na walioongopa wazi juu ya mauti ya JPM,walitunyima haki ya hata kumuombea wakati wake wa mwisho.
Mimi sidhani kama JPM alifariki ghafla lakini hawasemi alianza kuugua lini na kwa nini atibiwe Mzena wakati Muhimbili ipo na Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete pia ipo?
Leo wamekunyata sura wakiomboleza ingawa labda kimoyo moyo wanatuzomea,Kufa Kufaana!
Sitaka maishani mwangu kuwaamini CCM,kunena uongo kwao ni kawaida sana na ukweli kwao ni matusi
 
Mi naona ni mambo madogo sana.na shishangai.na Mama yuko vizuri sana,tumpe miaka mingi kama kumi tutakuwa mbali.
 
Back
Top Bottom