MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kwanza naanza kwa kutanguliza shukrani kwa Watanzania kukubali kuiga Wakenya kwenye zoezi la kupima kila dereva anayeingia, hiyo sasa imewezesha sote tuongee lugha moja, pima huko na sisi tupime huku, hapo tunakua na uhakika wa usalama wa kiafya kwa watu wetu.
Ingewagharimu sana kama mngeendelea kuruhusu Wakenya walioathirika kuingia huko na kujiachia full bata. Ninachokifahamu ni kwamba madereva wote ukanda huu wanaambukizana kwa kasi maana wengi hulala kwenye magesti uchwara kwa vitanda ambavyo malazi hufuliwa hata mara moja kwa wiki, na huingia wakiwa walevi bila kujali nani kalala humo jana, hivyo lazima tutegemee mamia ya madereva kuathirika.
Kile ambacho labda kifanyike, wataalam wa nchi zote mbili washirikiane na kukubaliana aina gani ya mashini zitumike, kila anayekuja anapimwa, huku zoezi likishuhudiwa na wataalam wa pande zote, ila wa Tanzania akigunduliwa ana kirusi, anapokezwa kwenye mamlaka husika kimya kimya maana hao bado wanahangaika kuweka siri na kuendelea kuaminisha umma kwamba hamna tena corona kwao, hivyo kelele zote hizi zinatokana na hili la Kenya kutaja idadi ya madereva wa Tanzania walioathirika.
Sasa ili kupunguza makelele, upande wao ibaki siri, wawe wanataja kama nilivyoona juzi wakifanya, walitumia maneno kama "raia wa nchi ambayo haitatajwa kwa sasa", ila kwa upande wetu watajwe kabisa idadi yao wangapi waliogunduliwa.
Hapo nina uhakika tutaendana vizuri sana tena tutaongea lugha moja na kuendelea kuitana pumba za "undugu".