Licha ya nchi kuwa na umasikini, wapo wenye afadhali lakini bado wanapigwa gepu na Waarabu/ Wahindi, tatizo nini?

Licha ya nchi kuwa na umasikini, wapo wenye afadhali lakini bado wanapigwa gepu na Waarabu/ Wahindi, tatizo nini?

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Pamoja na nchi kusumbuliwa na umasikini, zipo familia ambazo zinaishi fresh, tunaziita mambo safi.

Licha ya hali hii lakini bado wageni na Watanzania wachache wenye asili ya nchi za nje wanakimbiza.

Ukicheki listi ya matajiri, ambae aliwahi kujitahidi labda kwa mbali ni Marehemu Mengi angalu aliweza kuwemo kwenye Top 10 ya matajiri lakini bado hakufua dafu kuwapita hao wengine.

Ukianiambia kwamba shida ni kwamba hatuna ushirikiano ni kweli hili tatizo lipo makabila mengi watu kuoneana wivu na kurogana ila yapo makabila machache watu wanasaidiana sana na kupeana connections.

Shida iko wapi kwa hawa watanzania wenye asili ya hapa kwetu kutoweza kuwapiku hao wachache?
 
Sisi ngozi nyeusi wengi wetu hatuna ushirikiano, ukitoboa unatoboa peke yako sana sana unakuwa na harrier nanihii la nyani au brevis, una nyumba yako moja mjini na watoto wanaenda English medium basi inatosha na wala hauhitaji kushirikiana na ndugu/koo kuongeza kipato na ukiwashirikisha lazima wakunyooshe, hao wahindi na waarabu wengi wao wanapambania mafanikio ya kutoka kizazi kimoja kwenda kingine na wanashikana mkono sana
 
Hilo nakataa mkuu, kuna familia na koo zinasaidiana sana.

labda uniambie ni vipi huko kusaidiana hakufikii hao wengine
 
Pamoja na nchi kusumbuliwa na umasikini, zipo familia ambazo zinaishi fresh, tunaziita mambo safi.

Licha ya hali hii lakini bado wageni na Watanzania wachache wenye asili ya nchi za nje wanakimbiza.

Ukicheki listi ya matajiri, ambae aliwahi kujitahidi ni Marehemu Mengi angalu aliweza kuwemo kwenye Top 10 ya matajiri.

Shida iko wapi kwa hawa watanzania wenye asili ya hapa kwetu kutoweza kuwapiku hao wachache?
Threads zako zote huwa hazikamiliki bila kusifia wachagga, moshi au arusha 🤣🤣🤣🤣
 
Threads zako zote huwa hazikamiliki bila kusifia wachagga, moshi au arusha 🤣🤣🤣🤣
Mkuu naomba basi wewe uwe muwazi, kuna tajiri mtanzania wa asili ambae kwenye top 10 kapenya ukiachana na Marehemu Mr Mengi ?
 
- Hauwezi kuishi ugenini kama kwako : kwa hiyo Waarabu na Wahindi Ni rahisi kupambana kufa kupona.

- Ulimwengu wa kiroho unahusika . Hao wahindi na waarabu wanavitu vya ajabu : kama majini

- Jinsi ya kufikiri : Kufikiri kwa mtu mweusi Ni tofauti kabisa na watu weupe . Mbongo akipata Crown na nyumba basi anaridhika hadi kitambi. Hawazi katika fikra kubwa ambazo hazijawahi kufikika
 
Hao matajiri unaowaongelea ni self made au kurithishwa kwenye familia???
Mi naona wahindi wabadilisha mboga tu na vile wanaishi mjini basi aaaah.
 
The bottom line ni akili na life style. Ngozi nyeusi hata ukiwashirikisha mambo ya msingi hawazingatii na sanasana watataka kukuangusha ufanane nao au wakumalize .

Pile lifestyle ya kibongo ni ya kilimbukeni kupenda starehe na show off sanaaa. Mtu akiweza tu kubadiri mboga Kila siku anashinda bar na kuongeza idadi ya wanawake wasioweza kuzalisha kitu Bali kutumia tu .
 
Tangu uhuru mpaka sasa ni kizazi cha ngap?
wengi wa wapambanaj ni kizazi cha pil tangu uhuru na hakuna cha maana ambacho wamerithi toka kwa wazaz

anae fanikiwa unakuta ndio wa kwanza kuanza kukusany utajir ndan ya familia huk ndug kibao wanamtegemea
 
Tanzania wahindi na waarabu hawafiki laki 3...

Halafu wao Wana connection ya kimataifa...Wana ndugu Kenya.,Oman , India etc...
Wana culture ya biashara na discipline needed kwenye biashara
 
Back
Top Bottom