Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

We boya sana yani unakata mikucha yako na nail cutter za mtu mwingine magonjwa yote haya.

Mimi ilinikuta miaka kadhaa iliyopita ndio nimeajiriwa kwenye kampuni flani hapa dar.jioni nimekaa na mabosi zangu kupata wine kidogo na kujuana vizuri.tulikua tumeweka simu zetu mezani,bahati mbaya nikachukua simu ya bosi mmoja nikatia mfukoni nikijua ni yangu .mara kidogo jamaa akaanza kuulizi simu yake mimi nimetulia tu nikiamini iliyopo mfukoni ni yangu.

Dah ilivyobipiwa ikaita kwangu halafu hata hawakunipa nafasi ya kujieleza zaidi ya kila mtu kutunza simu yake kwa umakini,nilijisikia fedheha haielezeki

Uwiii I can feel you, pole sana. Hiyo ilikua fedheha na nusu [emoji30].
 
We boya sana yani unakata mikucha yako na nail cutter za mtu mwingine magonjwa yote haya.

Mimi ilinikuta miaka kadhaa iliyopita ndio nimeajiriwa kwenye kampuni flani hapa dar.jioni nimekaa na mabosi zangu kupata wine kidogo na kujuana vizuri.tulikua tumeweka simu zetu mezani,bahati mbaya nikachukua simu ya bosi mmoja nikatia mfukoni nikijua ni yangu .mara kidogo jamaa akaanza kuulizi simu yake mimi nimetulia tu nikiamini iliyopo mfukoni ni yangu.

Dah ilivyobipiwa ikaita kwangu halafu hata hawakunipa nafasi ya kujieleza zaidi ya kila mtu kutunza simu yake kwa umakini,nilijisikia fedheha haielezeki
Bonge la aibuu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kitambo flani nilikuwa na mpenzi mmoja matata sana na uzuri tulikaa mtaa mmoja ila yeye aliajiriwa shirika binafsi na ni karibu na ofisini kwangu.

Binti akawa na tabia akitoka kazini kwake anakuja kunipitia tunakwenda home na gari ya ofisi (serikalini) kwangu. Ambapo ilikuwa ni kawaida coz watu wengi walifanya hivyo hata kwa watoto wao washule pia witumia fursa hiyo kwa kupanda gari za hapo ofisini kurahisisha usafiri.

Mara chache sana Bosi alikuwa anapanda gari za Utawala coz yeye alikuwa na VX lake!! Na gari za utawala zilikuwa cruiser mkonge sita na zilikuwa zinabeba watumishi kwa idara. Idara yangu tulikuwa watatu so gari ilikuwa na nafasi kibao tu.

Kumbe katika hizo mara chache Boss akamuona binti wangu na akamuelewa ila pa kumpatia hana!! So, akawa anabanana nasi kwenye gari ya wasaka tonge na hataki kukaa siti ya mbele ambayo tulikuwa tunamuachia kwa heshima yake (sisi tukajua Boss anapenda sana gari ya idara yetu [emoji23][emoji23][emoji23] kumbe ana yake)!

Kitendo cha kukaa siti za nyuma na wavuja jasho akafanikiwa kupata contact za binti wangu mrembo na akawa anaimbisha mi bila kujua! Bahati mbaya sana, binti akampa cha mbavu Boss kubwa!!

Bosi akajawa na hasira, akaona njia ya pili baada ya ile ya kwanza kufeli ili kumpata Binti ni kunidhalilisha mbele ya binti ili kunishushia status!

Siku hiyo sina hili wala lile, muda wa kutoka umefika nikasogea garini na mrembo wangu. Kuna staff mwenzangu akachelewa kuja garini dereva akawa anapiga honi asikie aje.

Dereva alipoona jamaa haji akaamua kushuka amfuate ofisini! Lilikuwa kosa kubwa sana!! Aliibuka Boss from nowhere akaanza kunitukana kwanini napiga honi nasumbua na pia si kazi yangu kufanya hivyo!!

Alinitukana sana japo nilijitahidi kumwelewesha kuwa dereva ndiyo kapiga honi hakunielewa! Na kesi zikawa zinahama, zinatoka kwenye honi zinakwenda ofisini zinarudi zinakwenda mtaani zinarudi zinakwenda kwenye umalaya zinarudi huuuuh!!

Dereva akimwambia ni mimi nilipiga honi mkuu, anahamisha kesi inakuja madai ya umalaya mradi matusi na dharau zimtoke!! Niliyakoga siku hiyo sitasahu kabisa!! Dereva akitaka kutoa gari anamwambia ondoa gari langu na wewe nikuonyeshe!!

Nilikaa kimya, nachezea nokia ya tochi zile toleo la kwanza kabisa!! Ilikuwa ndiyo simu hot kabisa kabisa wakati huo!!

Aliporidhika akaondoka zake, garini hakuna mtu aliongea mpaka tunashuka!! Staff zote walitoka nje kuona kunani huko parking!!

Baadae ndiyo Binti ananiambia inawezekana kaamua kufanya hivyo sababu anamtaka kimapenzi, na sms zake akanionyesha!! Pia baada ya kutukana sana akamtumia Binti msg "si ndiyo kibwana chako unachoringia, haya ana nini sasa"

Hii kesi hii kwangu haijaisha kabisa!! Kuna siku akajitusua nikafuma kabrasha analipa vibarua hela ndogo kuliko iliyopitishwa na bodi na kuna allowance alikuwa analipa kidogo kuliko iliyopitishwa kwenye bajeti na bodi kisha inayobaki anapiga!

Nikanyofoa karatasi piga kopi nikamchoma macho makavuu huku anaona!! Kidogo avuliwe ukuu wake kama si kuhonga sana na baada ya hapo nikatafuta ajira kwingine nikasepa!!

Ila bado nikikumbuka naona kama kanidhalilisha jana hivi!! Bado namuwinda, nilimuotea mwanae kwenye harakati flani hivi nikamtosa then nikamwambia kamsalimie baba yako!
Duhhh...
 
Hiyo ilinitokea miaka kama sita iliyopita, Sikh hiyo nimeenda ukweni kwa Mara ya kwanza kabisa, sasa lile wenge la kuonana na babamkwe( Wakati tunafika hakuwepo,alipiga simu yupo njiani anakuja) Basi nikawa naenda chooni kukojoa.

Ile nafika chooni nakuta kuna mzigo haujasukumwa, duh palepale nikaghairi kujisaidia ile nafungua mlango nitoke uso kwa uso na babamkwe,

A see hata domo lilikuwa zito maana lazima angejua ni Mimi ndiyo nimesababisha, ile anaingia naskia anafyonya. Acha kabisaaa.
Dahhhhh
 
Mwaka Fulani nikiwa na ndugu Yangu mtoto wa mama mkubwa tulikua tunaangua maembe eneo fulani la serikali ghafla katokea mlinzi tukatimua mbio yule mlinzi katuungia tela na kuanza kutuitia mwizi mwizi bahati nzuri mitaa yote niliyokua napita nilikua nafahamia ndio ikawa pona Yangu, mlinzi mpumbavu sana yule alikua anaitwa Mkude
 
Nyingine imenikuta kigari Rwanda hiyo nimeingia hotelini, menu imeandikwa kinyaru tu, weita hajui kiswazi anajua kinyaru na French tu mzee mzima ni kiswaz na English robo tu, baada ya lugha gongana ya muda mrefu nikafanikiwa kuagiza maziwa na maandazi.
Akauliza maandazi mangapi swali hili nilitambua nikampa ishara ya vidole vinne nikaona anashangaa sana akasepa jikoni baada ya muda kwa mbali namwona weita wawili wanakuja na kikombe nusu jagi hayo ndio maziwa afu mwingine ana sinia linamaandazi manne yaan ni makubwa hadi kubebea sinia wakaweka mezani kwangu mwana wateja wote wakawa wananicheki kila anaeingia jicho kwangu hadi wengine wanaitana duu.
Mzee nilinyanyuka fasta nikaenda kaunta nikalipa faranga buku2 sikusubiri chenchi nikaingia mitini.

Ndio niligundua kwa nini weita alishangaa kumpa ile ishara na pia nikajua wanyaru hawana vikombe na viandazi kama vyetu vya kupunjana tu
 
Hakuna siku ilikua mbaya kwangu kama siku nimepanda daladala kumbe sikua na nauli maana nlisahau wallet yangu bahat mbaya, aisee nlitukanwa na konda pamoja na dereva wake changanya na abiria naambiwa mbona simu hukusahau, mbona nguo hukusahau, tapeli mkubwa daa nliumia sana ile siku sitasahau.
 
Poyeee bibi3 ungenipigia simu nije kukulipia

Daah hii ni hatari
 
Kuna siku ndo nimetoka kireport kazini kama siku mbili 3 hivi nmebaki ofisini mwenyewe si nikaachia hewa chafu pale mara paap Boss huyu hapa ofisi inanuka balaa hakika nilipata fedhehea ya kufa mtu
. Hii kali mkuu.
 
Duuuuh pole kama nakuona ulivopata shida ko ikaweje..daaah Leo nimecheka sana
dah kuna nchi fulani ya nje nilienda mgahawani bahati nikashikwa na haja kubwa,nimefika chooni baada ya kujisaidia kila nikitafuta maji hakuna,naona toilet papers tu nikaona isiwe tabu nikakata tu lile bomba linalopeleka maji kwenye kile kidumu kwa ajili ya kuflash baada ya kujisafisha kimbembe kwenye kurudisha bomba sasa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kulikuwa na mama mmoja amepanga jirani na nyumbani kwetu, ni MTU mzima alishaolewa na akaachika, alikua na uhusiano na kijana mdogo ambaye umri wake haumfikii hata mmoja kati ya watoto wake, na alikua akilalanae kwa siri, basi siku moja yule kijana alikuja kwa yule mama hakumkuta,alimsubiri kwa muda lakini hakutokea, ndio alipoamua kuparamia dirishani na kuingia ndani akitegemea sugar mummy wake atarudi. kwa bahati mbaya yule mama hakurudi na hakua na taarifa kumhusu Dogodogo wake. shida ilianza palipo kucha yule kijana anataka kutoka kuparamia kwa ndani Kashindwa, ndipo alipoanza kugonga mlango, wapangaji wa vyumba vingine wakaenda, kilichowashangaza ni kwamba mlango umefungwa kwa kufuli kwa nje, ndio wakaanza kumuuliza wewe nani? na uliingiaje humu ndani? ikabidi jamaa afunguke tu hakua na jinsi. baada ya kujieleza, wale wapangaji wakakubalia wamwite balozi, na balozi akashauri waende polisi kwanza kabla hawajamsaidia, walipokuja polisi ndipo mlango ukavunjwa na hapo watu walishajazana kibao. aibu kiasi gani ndugu yangu!?
Aiseee hii nayo Kali. Kwa nini hakutokea palepale alipoingilia?
 
Pole mkuu hizo ndo habari za mjini

Back
Top Bottom