The bright one
JF-Expert Member
- Jul 17, 2018
- 272
- 565
Nakumbuka mwaka 2004 Mimi bishoo kinoma sasa kipindi kile zilikuwa zimetoka jinsi Fulani tulikuwa tunaita mikasi,maana zilikuwa nyeupe mixed mikasi mikasi rangi nyeusi!,sasa bana dukani zilikuwa bei juu kinoma,Mara kuna mshkaji wangu mmoja hivi nilikuwa na rap nae kipindi hicho akaniambia anauza jinsi hiyo mikasi kwa 7000tsh nikaona kama ndoto vile sikuamini ,nikachomoa fasta pesa ya ada ambayo nilikuwa natakiwe nilipe kesho yake nikampa jamaa 7000tsh akaniletea ukali,fasta Mzee mzima nikaingia kuoga kwanza nikatupia vitu vikali na ile jinsi nikaanza kunesa kitaani sikufika hata mbali ni kama mita 200 tu kutoka home mama mmoja alikuwa na wanae kama wa nne hivi wakubwa kimtindo akanisimamisha,nilivyosimama baada ya salamu akaniambia mwanangu samahani Nina wasiwasi na jinsi uliyovaa ni ya mwanangu huwa anaibiwa sana jinsi kwahiyo nikaamua nikimnunulia mpya huwa kuna sehemu naweka alama,kwahiyo kama huamini alama ni Fulani na nimeweka sehemu Fulani tukikuta sio usijali mwanangu nakurudishia jeans yako!
Kwa vile home ilikuwa ni mita 200 tu kutoka pale hao mpaka ghetto nikavua suruali tukakuta ni kweli zile alama zipo,nikamwambia mama Mimi nimeuziwa na MTU Fulani na bahati nzuri ni jirani yake alikuwa anamjua vizuri, Mzee nikaachia jeans kesho yake nikamtokea mshkaji aliyeniuzia kimya kimya ghettoni kwake nikamweleza kisanga jamaa kumbe ndio ilikuwa ndio zake bila hiyana akanipa jinsi nyingine sikuipenda sana lkn nilikuwa sina namna na akanisisitizia hiyo sio ya wizi Mimi nikasepa zangu na urafiki ukaishia hapo
[emoji81]🤣[emoji81]🤣