Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?


Uwiii I can feel you, pole sana. Hiyo ilikua fedheha na nusu [emoji30].
 
Bonge la aibuu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Duhhh...
 
Dahhhhh
 
Mwaka Fulani nikiwa na ndugu Yangu mtoto wa mama mkubwa tulikua tunaangua maembe eneo fulani la serikali ghafla katokea mlinzi tukatimua mbio yule mlinzi katuungia tela na kuanza kutuitia mwizi mwizi bahati nzuri mitaa yote niliyokua napita nilikua nafahamia ndio ikawa pona Yangu, mlinzi mpumbavu sana yule alikua anaitwa Mkude
 
Nyingine imenikuta kigari Rwanda hiyo nimeingia hotelini, menu imeandikwa kinyaru tu, weita hajui kiswazi anajua kinyaru na French tu mzee mzima ni kiswaz na English robo tu, baada ya lugha gongana ya muda mrefu nikafanikiwa kuagiza maziwa na maandazi.
Akauliza maandazi mangapi swali hili nilitambua nikampa ishara ya vidole vinne nikaona anashangaa sana akasepa jikoni baada ya muda kwa mbali namwona weita wawili wanakuja na kikombe nusu jagi hayo ndio maziwa afu mwingine ana sinia linamaandazi manne yaan ni makubwa hadi kubebea sinia wakaweka mezani kwangu mwana wateja wote wakawa wananicheki kila anaeingia jicho kwangu hadi wengine wanaitana duu.
Mzee nilinyanyuka fasta nikaenda kaunta nikalipa faranga buku2 sikusubiri chenchi nikaingia mitini.

Ndio niligundua kwa nini weita alishangaa kumpa ile ishara na pia nikajua wanyaru hawana vikombe na viandazi kama vyetu vya kupunjana tu
 
Hakuna siku ilikua mbaya kwangu kama siku nimepanda daladala kumbe sikua na nauli maana nlisahau wallet yangu bahat mbaya, aisee nlitukanwa na konda pamoja na dereva wake changanya na abiria naambiwa mbona simu hukusahau, mbona nguo hukusahau, tapeli mkubwa daa nliumia sana ile siku sitasahau.
 
Poyeee bibi3 ungenipigia simu nije kukulipia
 
Daah hii ni hatari
 
Kuna siku ndo nimetoka kireport kazini kama siku mbili 3 hivi nmebaki ofisini mwenyewe si nikaachia hewa chafu pale mara paap Boss huyu hapa ofisi inanuka balaa hakika nilipata fedhehea ya kufa mtu
. Hii kali mkuu.
 
Duuuuh pole kama nakuona ulivopata shida ko ikaweje..daaah Leo nimecheka sana
 
Aiseee hii nayo Kali. Kwa nini hakutokea palepale alipoingilia?
 
Pole mkuu hizo ndo habari za mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…