Gam2
Member
- Aug 20, 2017
- 33
- 13
Niliwahi kwenda migahawa koko maeneo flani ivi nikakuta contena la kunawia mikono wameweka pembeni na nyumba ya mtu alafu mgahawa wenyewe uko mbali kidogo mi niliponawa nikaingia nyumba iliyokuwa jirani nikidhani ndio mgahawa wenyewe kumbe nimeingia kwenye geto la Mmama flani ivi.
Sasa mda naingia alikuwa bize anakula alafu kageukia upande wapili wala hakusikia vishindo mda naingia kwa akili za kitoto nilipogumdua kuwa nimeingia kusipo nikapata akili ya kutoka kimyakimya tena...! Kumbe mda natoka ndani yule mama akashtuka nikajifanya kuchomoka mule ndani kwa haraka ndio akaniitia mwizi..mwizi...mwizi asee nikajifanya kukimbia nikaishia mikononi mwa wanainchi wenye hasira kali aisee sitakaa nisahau kilichonipata yaani kuna watu bongo hii hata ukiwa unatoa maelezo hawayazingatii wao ni kupiga tu na kutafta petroli.... Hadi leo nikikuta mwizi anapigwa huwa napenda kusikiliza maelezo yake kama yanaleta logic....Maana ningechomwa moto na sijawahi kuiba wala kutapeli cha mtu!
[emoji28][emoji28][emoji28]