Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Niliwahi kwenda migahawa koko maeneo flani ivi nikakuta contena la kunawia mikono wameweka pembeni na nyumba ya mtu alafu mgahawa wenyewe uko mbali kidogo mi niliponawa nikaingia nyumba iliyokuwa jirani nikidhani ndio mgahawa wenyewe kumbe nimeingia kwenye geto la Mmama flani ivi.

Sasa mda naingia alikuwa bize anakula alafu kageukia upande wapili wala hakusikia vishindo mda naingia kwa akili za kitoto nilipogumdua kuwa nimeingia kusipo nikapata akili ya kutoka kimyakimya tena...! Kumbe mda natoka ndani yule mama akashtuka nikajifanya kuchomoka mule ndani kwa haraka ndio akaniitia mwizi..mwizi...mwizi asee nikajifanya kukimbia nikaishia mikononi mwa wanainchi wenye hasira kali aisee sitakaa nisahau kilichonipata yaani kuna watu bongo hii hata ukiwa unatoa maelezo hawayazingatii wao ni kupiga tu na kutafta petroli.... Hadi leo nikikuta mwizi anapigwa huwa napenda kusikiliza maelezo yake kama yanaleta logic....Maana ningechomwa moto na sijawahi kuiba wala kutapeli cha mtu!

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Na mm kuna matukio kama mawil matatu hivi dah kila nikikumbuka nacheka[emoji23][emoji23][emoji23]

Mwaka jana 2020 nilipita pale Be Forward posta karibu na ocean road,wakati naendelea na kilichonipeleka pale nilibanwa na haja ndogo baada ya kuuliza wenyeji wangu wakanielekeza chooni..
Nimefika chooni nmekuta mtu kaacha zigo juu hajaflash,dah kwa sababu na mm nlikua na haja nkajaribu kuflash bila mafanikio kwa sababu hapakua na maji,nikaona bora nikojoe nisepe,nmemaliz natoka napishana na mdada flani hivi aisee nlijisikia vibaya mno,nlitamani nimwambie usiingie au huo mzigo si wangu ila sikuweza... nilisikia bonge la sonyo na "kuna watu sio wastaarabu"[emoji23][emoji23][emoji23]basi yule dada nlikua na coincidence nae nikawa naonana nae mara kwa mara mpka kuna siku nilipanda nae mwendokasi na kukaa nae seat moja,nilitamani nmuelezee mzigo haukua wangu ila ndo hivo naanzaje
Hahah! Dah Mkuu umetisha
 
Nilikua na tabia ya kujamba mbele ya katoto kangu kalikua bado hakajalewa kenyewe kalikua kanacheka tuu kanajua nafanya hivyo kumfurahisha...sasa nilipoanza kukafundisha kutumia potty sijui ndo kagagundua ukijamba ni dalili ya haja, siku nimekaa sina hili wala lile nikaachia bomu kakakurupuka kaenda kutafuta potty eti "kunya mama, mama mama kunya" halafu nilishatoka mbele za watu jamani nilifedheheka japo wengine hawakumuelewa wakawa wanamshangaa tu mie nilimchunia kama simjui Ila niliona aibu na nikakoma hiyo tabia.
Duh htr
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuna vyoo vya kushare jinsia zote? Au mie ndo sijui. Lol
 
Mwaka flani hv nimeenda zangu maeneo kumtembelea sister,siku hyo sister kasafiri nimebaki na anko 2,ilikuwa wikiend nikaenda zangu kucheki mpira narudi zangu mida kama ya saa 5 hv uck,narudi geti limefungwa,namgongea anko nae kalala kinouma nimekaa kama nusu SAA hv nagonga hakuna kufungua,nikaamua kufungua dirisha nipitie hapo,vile vidirisha vya zamani vinakuwa na nondo katikati aisee,so nikapiga hesabu nikaona kupita na nguo haiwezekani so nikavua nguo nikaziingiza ndani nikabaki na chupi 2 nikajua si napita fasta, ile kuanza kupitisha kichwa hakipiti kumbe ni padogo ,kasheshe likaanzia hapo,hangaika wapi, hangaika wapi nikaona jau hili,nikamkumbuka jamaa yangu anakaa mtaa wa pili,ikabidi nitoke pale kwa spidi kali nipo na kichupi 2 nakatiza mtaaan,wikiendi ile mitaa watu wanacjelewa sana kulala so nilikutana na watu wanacheka walijua nimetoka kufumaniwa so nakimbia soo,ile nafika kwa jamaa,jamaa kafungua kunikuta vile anacheka kishenzi,kwa soo lile sikukaa sana ilibidi nirudi home 2
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilikua na tabia ya kujamba mbele ya katoto kangu kalikua bado hakajalewa kenyewe kalikua kanacheka tuu kanajua nafanya hivyo kumfurahisha...sasa nilipoanza kukafundisha kutumia potty sijui ndo kagagundua ukijamba ni dalili ya haja, siku nimekaa sina hili wala lile nikaachia bomu kakakurupuka kaenda kutafuta potty eti "kunya mama, mama mama kunya" halafu nilishatoka mbele za watu jamani nilifedheheka japo wengine hawakumuelewa wakawa wanamshangaa tu mie nilimchunia kama simjui Ila niliona aibu na nikakoma hiyo tabia.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] alikukomesha lol
 
Na mm kuna matukio kama mawil matatu hivi dah kila nikikumbuka nacheka[emoji23][emoji23][emoji23]

Mwaka jana 2020 nilipita pale Be Forward posta karibu na ocean road,wakati naendelea na kilichonipeleka pale nilibanwa na haja ndogo baada ya kuuliza wenyeji wangu wakanielekeza chooni..
Nimefika chooni nmekuta mtu kaacha zigo juu hajaflash,dah kwa sababu na mm nlikua na haja nkajaribu kuflash bila mafanikio kwa sababu hapakua na maji,nikaona bora nikojoe nisepe,nmemaliz natoka napishana na mdada flani hivi aisee nlijisikia vibaya mno,nlitamani nimwambie usiingie au huo mzigo si wangu ila sikuweza... nilisikia bonge la sonyo na "kuna watu sio wastaarabu"[emoji23][emoji23][emoji23]basi yule dada nlikua na coincidence nae nikawa naonana nae mara kwa mara mpka kuna siku nilipanda nae mwendokasi na kukaa nae seat moja,nilitamani nmuelezee mzigo haukua wangu ila ndo hivo naanzaje
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Tukio lingine ninalo likumbuka ilikua miaka ya nyuma kidogo, nmemaliza kidato cha nne pale nasubiri kwenda A level,hivyo nikasafiri kwenda Moshi kwa ajili ya likizo hiyo ndefu.... Basi bwana,pale mtaani kukawa na sherehe za kipaimara cjui ubarikio sikumbuki vizuri ambae mdogo ake jamaa angu ndo alikua muhusika so nikaalikwa na huyu mshkaji wangu,ukafika muda wa msosi na utaratibu ni kupanga foleni,yule jamaa angu akawa na mishe mishe hivyo na mimi ikanibidi nipange foleni,imefika zamu yangu basi kuna mama wa kipare alikua ana "save" msosi pale,alinifananisha akaniwakia "kaka umeshachukua chakula pisha wenzio nao wapate kama hujashiba utaongeza mwishoni"...aisee nilijisikia vibaya,kwanza watu wengi,alafu mimi ni mgeni pale tena "kutoka Dar" sa kadri nilivyokua nakataa ndio yule mama anapaza sauti na kuzua taharuki pale,ilibidi niondoke kitendo kilichoaminisha kweli nlikua narudia,nilidhalilika sana na roho iliniuma sana japo yule jamaa angu aliniomba radhi haikusaidia... nilijifungua ndani muda wote na nikahama na mtaa kabisa nikaenda kuishi Moshi mjini kutoka NewLand[emoji24][emoji24]
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
We boya sana yani unakata mikucha yako na nail cutter za mtu mwingine magonjwa yote haya.

Mimi ilinikuta miaka kadhaa iliyopita ndio nimeajiriwa kwenye kampuni flani hapa dar.jioni nimekaa na mabosi zangu kupata wine kidogo na kujuana vizuri.tulikua tumeweka simu zetu mezani,bahati mbaya nikachukua simu ya bosi mmoja nikatia mfukoni nikijua ni yangu .mara kidogo jamaa akaanza kuulizi simu yake mimi nimetulia tu nikiamini iliyopo mfukoni ni yangu.

Dah ilivyobipiwa ikaita kwangu halafu hata hawakunipa nafasi ya kujieleza zaidi ya kila mtu kutunza simu yake kwa umakini,nilijisikia fedheha haielezeki
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] mbavu zangu
 
Dah kunasiku gari ya mshua ilikodiwa kwenda njombe... Ilibeba wanakwaya wanaenda kweny harusi ya mwwnzao
Sasa kufika kule wakawa kanisani wanasherekea...mim nipk ndan ya gar nimelala daaaaaaaaaaah!!!! NILIJAAMBAAA KWANGUVU KAMA MALA3 AFU KWA UHURU NIKIJUA NIPO PEKEANGU NDANI.... baada ya dk mbili hivi nikashituk kuangalia hiv kuna mmama kakaa pembeni daaaaaaaah!!!!!!
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Bro wangu ameoa sasa.Alikuwa na demu lake lina msambwanda kinyama.Basi lilivyosikia jamaa anaoa alienda kumfanyia fujo home wote tulikuwepo.Likaanza kubwatuka kuwa jamaa kamla ndogo miaka mingi kwa nini amuoi yeye.Tuliona noma sana.Washua wananiuliza kweli?Nikawaambia mkamuulize bro.Noma sana.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Ndio akome kutembea na mashangingi

Daahhh nimecheka Sana [emoji3]
 
Nakumbuka miaka ya nyuma tulitoka kwenye kwaya jamaa mmoja akawa amekula vyakula vingi kwa kuchanganya wakati tukiwa safarini jamaa akabanwa na haja kubwa akaomba gari isimame ili ajisaidie,jamaa alikuwa amepiga bonge ya suti mbaya zaidi alikuwa mwalimu wa kwaya,,mzee baba alivyorudi akarudi amechafua koti la suti kwa pembeni na kinyesi bila yeye kujua,watu ilikuwa ni kucheka tuu [emoji23].nikamwambia jamaa umechafua koti yeye hakujua kama ni uchafu gani akashika ile kushika watu wakacheka gari zime jamaa akakunguta mkono ule mzigo ukiangukia kichwani nikikumbuka hiyo siku nachekaga wenyewe tuu.[emoji23]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nikiwa form 2 kwenye miaka ya 2000 kuendelea..nikiwa kama kijana sharp kabisa kwenye extended family yetu hapa Dar..Mshua akanipa pesa shilingi milioni moja za ujenzi nipeleke moshi kwa bibi yangu mlokole asilimia (100%)Basi laki tano nikaweka mguu wa kushoto tano nyingine mguu wa kulia...
Nikapewa ticket ya Bus moja nakumbuka likiitwa Amazon na fedha taslimu elfu 70 nauli ya kurudi na pesa ya kijikimu na zawadi za njiani kupeleka kwa bibi na simu ndogo ya kufunua aina ya Bird kwa ajili ya mawasiliano.
Nikatoka zangu kinondoni studio mpaka ubungo terminal, bus nikaliona nikaenda kwenye kibanda nikanunua pombe pakti 3 aina ya Tyson nakumbuka walikua wanauza 650 kwa pakti moja nikaipiga pale pale mbili nikapanda nazo kwenye bus...Nilikua nimekaa kwenye siti ya 2 by 2 dirishani ghafla wakapanda wadada wawili na mkaka mmoja ...dada mmoja mweupe mwenye shepu.. yani ni mkubwa kabisa kuliko mimi akaja akakaa akanisalimu wenzake wakakaa siti ya mbele yetu...Sasa mm nina pombe yangu nilikua napenda apande hata msela akae na mm ili niwe huru kukata na kunywa pombe yangu[emoji23]Basi nimejikaza mpaka maili moja kibaha nikasema hapana wakati nafikiria nn cha kufanya wale wa mbele wakampa mwenzao katoni ya castle lager za kopo akatoa moja akafungua akaanza kunywa akaniambia karibu kaka nikachukua kopo ...zikaisha tokaongeza...mara nimetoa kisimu nijifanye kumbeep bibi ilimradi vurugu nikatoa na yale mapomve makali ya viroba nakumbuka tuliwaka sana...To make the long story short nilitakiwa kushuka Kiboriloni nikajikuta niko hoteli moja arusha inaitwa Seven Eleven kama sikosei....niko uchi niko na yule dada[emoji23][emoji23] kumbe nilikata moto simu nimezima sipatikani yule demu kumbe kwenye milioni akadai eti nilinwambia tutumie laki tu zinazobaki tutaenda ngorongoro pakikucha akawa anezihifadhi..kweli kuhesabu nina laki 9[emoji23][emoji23]Nikawasha simu nikapiga kwa bibi nikamwambia nimejikuta asubuhi nyuma ya bus nililotoka nalo dar nimelala na kwenye pesa baba alizonipa imechukuliwa laki moja akapiga vigelegele kanisa lao lina branch arusha akawaelekeza wakaja kunichukua nikapewa shemasi anirudishe Moshi kama shujaaa.....Sijahi muhadithia mtu...yani hapa kwenyewe nlikua naandika nafuta naandika nafuta....kama yule dada yupo humu hata anipM jamaniii[emoji23][emoji23]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Huyo dada mtu Safi Sana mshukuru mno
 
Kulikuwa na mama mmoja amepanga jirani na nyumbani kwetu, ni MTU mzima alishaolewa na akaachika, alikua na uhusiano na kijana mdogo ambaye umri wake haumfikii hata mmoja kati ya watoto wake, na alikua akilalanae kwa siri, basi siku moja yule kijana alikuja kwa yule mama hakumkuta,alimsubiri kwa muda lakini hakutokea, ndio alipoamua kuparamia dirishani na kuingia ndani akitegemea sugar mummy wake atarudi. kwa bahati mbaya yule mama hakurudi na hakua na taarifa kumhusu Dogodogo wake. shida ilianza palipo kucha yule kijana anataka kutoka kuparamia kwa ndani Kashindwa, ndipo alipoanza kugonga mlango, wapangaji wa vyumba vingine wakaenda, kilichowashangaza ni kwamba mlango umefungwa kwa kufuli kwa nje, ndio wakaanza kumuuliza wewe nani? na uliingiaje humu ndani? ikabidi jamaa afunguke tu hakua na jinsi. baada ya kujieleza, wale wapangaji wakakubalia wamwite balozi, na balozi akashauri waende polisi kwanza kabla hawajamsaidia, walipokuja polisi ndipo mlango ukavunjwa na hapo watu walishajazana kibao. aibu kiasi gani ndugu yangu!?
Aisee [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nyingine imenikuta kigari Rwanda hiyo nimeingia hotelini, menu imeandikwa kinyaru tu, weita hajui kiswazi anajua kinyaru na French tu mzee mzima ni kiswaz na English robo tu, baada ya lugha gongana ya muda mrefu nikafanikiwa kuagiza maziwa na maandazi.
Akauliza maandazi mangapi swali hili nilitambua nikampa ishara ya vidole vinne nikaona anashangaa sana akasepa jikoni baada ya muda kwa mbali namwona weita wawili wanakuja na kikombe nusu jagi hayo ndio maziwa afu mwingine ana sinia linamaandazi manne yaan ni makubwa hadi kubebea sinia wakaweka mezani kwangu mwana wateja wote wakawa wananicheki kila anaeingia jicho kwangu hadi wengine wanaitana duu.
Mzee nilinyanyuka fasta nikaenda kaunta nikalipa faranga buku2 sikusubiri chenchi nikaingia mitini.

Ndio niligundua kwa nini weita alishangaa kumpa ile ishara na pia nikajua wanyaru hawana vikombe na viandazi kama vyetu vya kupunjana tu
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hakuna siku ilikua mbaya kwangu kama siku nimepanda daladala kumbe sikua na nauli maana nlisahau wallet yangu bahat mbaya, aisee nlitukanwa na konda pamoja na dereva wake changanya na abiria naambiwa mbona simu hukusahau, mbona nguo hukusahau, tapeli mkubwa daa nliumia sana ile siku sitasahau.
Pole Sana [emoji26]
 
Kubanwa haja kubwa na tumbo la kuhara safarini. Nikalazimisha gari isimame. Nikashusha nikamaliza shughuli hapo hapo nikarudi ndani ya basi nikalala
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] ukajisaidia njiani !?
 
Back
Top Bottom