Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Aisee
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Seven /eleven kiwanja changu hicho kila nikiwa arusha
 
Ungemtetea brother bana... Ukasema anapayuka tu Hana lolote roho inamuuma tu. Sasa kuwaambia wakamuulize broh umepigia jibu mstari... Sijui maza alijisikiaje kusikia baharia anaruka ukuta?

Sent from my GIONEE S11 lite using JamiiForums mobile app
 
Labda ni wewe ulijishitukia, lakini si fedheha.
 
Weee jamaa umenichekesha Sana... Eti Kama shujaaaa.... Laki Tisa ngorongoro

Sent from my GIONEE S11 lite using JamiiForums mobile app
 
siku nimeingia pale cafteria ya coed udom mwafrika asubui tu kwenda kusaka supu...nikaudumiwa fresh tu nikaenda kuweka vitu vyangu mezani nikasema nirudi kunawa....sasa kuna zile ndoo za chuma zinawekwaga maji ya moto me nikaona nikaona kama lile kumbe lile wao wameweka chai bhn ukiitaji unaenda pale unafunguliwa koki unachukua chai...me nikajua ndo lina maji ya kunawa nikaenda nikafungua ili ninawe...asee kelee niliyopigiwa nilpata aibu kubwa sana

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Nilinunua mkanda wa suruali pale kariakoo dar es salaam mida ya usiku usiku huwa wananinginiza ivi kwenye zile henga zao, kwa macho niliuona mzuri sana na strong wa kuvutia kumbe baba ule mkanda ni feki ajabu, umekuja kukatika siku 2 nilikuwa kwenye boti ivi nasafiri kwenda mahali, sasa mule kwenye boti kuna mademu mademu kibao na watu kibao wamekaa kwenye viti na boti inatembea wale mademu wao ndio wamenishtua kaka mkanda wako umekatika nilikuwa nimesimama ivi kwenda huku na kule mle kwenye boti. Yaani niliona aibu aibu aibu fedheha mara elfu1, nikajizoa zoa nikaenda kukaa mahali nikautoa wote tupa baharini., yaani kwa ile aibu ilibidi nijichimbie mahali mule kwenye boti mpaka boti ilipofika niliacha watu wote washuke ndio na mimi nikajikongoja kutoka sikutaka kuonana na mtu yeyote aliyeniona nikipata ile aibu.


Toka siku hiyo pale karikaoo ata kununua chupi naona ntapata feki feki nimejuta sana na nnahasira nao kinyma, tena afadhali huu uzi umekuja ili niwatanabahishe wale walio maeneo ya dar es salaam.
 
mkuu hii ni balaaa
 
Hapa inamaana baada ya mkanda kukatika suruali ilidondoka ama ulikatika tu
 
ungemwambia tu simu umenunua kwa mtu mtaani na namba hukujua Kama ipo kwenye hiyo simu

Na wewe ungejifanya kumuuliza ni yako hiyo namba? Hapo angekuelewa
 
[emoji23][emoji23][emoji23]..Mama.e
 
Dah,wakati uzi huu unaletwa sikuwa online kwakwel
Nina visa vyangu viwili na kingine ni cha mwanafunzi mwenzangu
Kisa no 1
Miaka kadhaa ya nyuma nikiwa form one huko vijijini basi kulikuwepo na utaratbu kila terminal na annual walikuwa wanasoma top ten na wale kumi wa kutoka mwisho basi siku hyo ilikuwa ijumaa tukifunga kwenda likizo ya mwezi disemba siku hyo nilkuwepo period na kipindi hiko tulikuwa tunavaa matambala hata pedi nilkuwa sizijui basi mida ya sa nane tukaa skuli balaza mawaidha yakaendelea mara nasikia damu zinatiririka mithili ya maji yaani nasikia sehemu nilyokaa kama imejaa hivi najiuliza niombe ruhusa kabla sijajifikiria vizuri nasikia wanaanza kusoma majina ya top ten mara jina langu linaitwa ,wa kwanza darasani ni fulani(sasa inabidi ninyanyuke niende kupewa mkono na meza kuu na kupewa zawadi)aseee!nildata pale chini kwa sekunde kadhaa,theni nkasimama ,nilihisi damu zinachuruzika hadi miguuni(but haikuwa hivo ni hisia tu) bahati nzuri sketi ilikuwa nyeusi afu ndefu basi nkapata akili nkavua sweta nkajifunga kiunoni ikabid niende mbele kuchukua zawadi(unapoenda mbele wanafunzi unawapa mgongo )japo sijui sikugundulika lakini niliona aibu sana yaani kama wiki nzima nilkuwa nikifikiria hicho kitu

Kisa no 2
Hii ni miaka ya hivi karibuni,kawaida mimi pombe nakunywa,lakini ni zile za kureflesh na ni mara chache mno na mara nyingi huwa nakunywa wine na konyagi ikitokea basi bwana siku hyo nimejisikia kunywa nimeenda glossary nkaulizia wine hakuna,konyagi hakuna nkaambiwa imebaki k,vant tu sijawahi kunywa kivant ila uwa nasikia wanaisifia basi nkasema wacha nichukue kivant ndogo maana sina namna,nkabeba zangu nkaenda home nkanywa but naona radha yake siyo nzuri nkajikaza nkanywa nilivomaliza nkaenda kulala,nimelala usingizi mzuri mara kama naota hivi nasikia mme wangu ananiamsha anasema umekuwaje????aseee kumbe natapika mashuka yote na blanket yashakula matapishi fasta usingizini(ikumbukwe sijawahi tapika tangu nakunywa pombe)haraka niliamka nkaenda chooni tapika wee mpaka nyongo aseeee siku hiyo niliona aibu yaani kutapika kisa pombee??na mme wangu yeye hata hanywiii,naichukia k,vant

Kisa 3
Tukiwa form four miaka hyo wavulana kwa wasichana ilikuwa mida ya sa saba jua kali kipindi cha hesabu darasani kilikuwa kinaendelea,ikumbukwe hii mida ni mida ambayo wanafunzi wengi wanakuwa wamelala basi kuna binti mmoja alikuwa amekaa sehemu ambayo ni katikati ya darasa kama kawaida akauchapa usingizi wake kwenye dawati,mda kidogo akaanza kuota na kukojoa akakojoa mkojo unatiririka kwenye sakafu,hyo nayo ilikuwa aibu kwake hata sisi wasichana tuliona aibu but ni mambo ya kawaida

Nilivokoswa na aibu ambayo nilishaiona mbele yako
2016 nilkuwa natoka gongo la mboto naenda job,kumbe nilvotoka nkabeba mkoba mwingine wa jana ambao ulikuwa na hela nkauacha,tumefika sokota nakumbuka nimebeba mkoba hauna nauli dah nkaona hapa ni hatari,nkimuona konda ni wale micharuko akili akanijia kwamba itabid nimwambie hela yake namtumia m pesa kwani nashukia njiani,nkaanza kuwaza ntakavodhalilishwa nkasema eeh Mungu wangu sijafanya makusudi,huwezi amini konda alinipita wala hakuniuliza nauli nami nkasema hii ndo inaitwa miujiza
But all in all aibu zinakuja vyovote kikubwa ni kuzipotezea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…