Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Mkuu chukua hii
Usipost picha ya mtu bila ridhaa yake
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahahahaaaaaa jamaa umenichekesha kinoma.
 
Mhh kipindi ndio nimefika hapa mjini basi katika harakati zangu kuna bro wangu akanitumaga nikamchukulie tiketi ya ndege kwenye jengo moja town ebhana weee pale pana milango ile ya kuzunguka mm na ushamba wangu nikajua unaingia unazunguka kidogo unasepa...... Weeee nilijibamiza kwenye kioo pka dada wa mapokezi akacheka nikawa nimepagawa sioni pa kutokea nikazungusha kama narudi nyuma ngoma haiendi kijasho kikanitoka nikasukuma kwenda mbele ndio naona uwazi wa kutokea dah nikapumzika kwanza mapokezi yule dada hana mbavu kwa kicheko mm nae ikabidi tu nicheke ila ni aibu sana asee wakati wa kurudi yule dada akawa ananiangalia mpka nikatoka loh sitakaa nisahau lile jengo
 
Nawe ushamba ulikuzidi,tabia za kike

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah mkuu pole sana,nadhani mimi ningefariki siku hiyo hiyo,unajua watu walichokuwa wanakuwazia hakikuwa kizuri .
 
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Miaka hiyo 2001 nipo form 2 mida ya jioni tunapiga misele mimi na rafiki yangu, mitaa ya kijenge juu Arusha,
Nikamuona mama mmoja anauza mihogo ya kukaanga, nikasogea karibu nikampa 200 ili anipe kipande cha muhogo
yule mama alikuwa anaongea na mtu mwingine wakati huo mi nasubiri muhogo, yule mtu alivyoondoka yule mama akaniuliza nikusaidie nini? nikamwambia nimekupa 200 nipe muhogo,
Aisee yule mama aligeuka mbogo, yani kijana mzuri unataka kunitapeli si afadhali ungeomba, niliona aibu kishenzi ikabidi niondoke kinyonge, sijasahau hadi leo. Nimejifunza kutotanguliza pesa mbele kabla ya kuhudumiwa.
 
Waliona wameajiri kibaka[emoji1787][emoji1787]
 
Dah, hii ngumu sana hapo lazima ulionekana mwizi / una nia ovu
 
Shukuru Mungu upo hai kaka na labda hiyo mitaa sio ya matukio sana, tungeshakusahau
 
Sidhani kama kutokujua ku scan ni aibu sema ulijishtukia tu, hii ilinikuta pia kigamboni pale kivukoni na zile kadi zao ila mi niliuliza na hakuna aliyenishangaa
 

Same as me
Nakushauri ukimaliza jitahidi uende law school mapema masharti yanaenda kuwa magumu mbeleni wameanza na kupandisha ada wanahamia kwenye mtihani ndio uwe admitted wataongeza jingine ili iwe ngumu kusoma usiogope kwamba watu wanafeli first sit

Kwenye sheria jitahidi kujichanganya na hasa mawakili wazoefu hata kama bado haujawa wakili utapata njia

Muzahula yupo?
Katabalo vipi?
Sr ngonyani yuko hapo?
Je Jiniazi masoud yupo?
Wanangu kina Mwita, kawiche, mwasi mbegu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Luhigo yupo?
Lutechura yupo?
Je mnoko sunga?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bro code 101 Never trust a fart.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…